Hongera mama, huu ni mwezi wako wa nne katika safari ya ujauzito. Sababu tosha kwako kusherehekea, hasa kwa sababu kukosa starehe uliko shuhudia kumepungua, kuhisi kichefuchefu na ugonjwa wa asubuhi. Katika mwezi huu, mimba imeanza kuonekana na watu wanakuuliza maswali na kukupongeza kila mara. Je, nini unachotarajia katika mimba ya miezi 4? Soma zaidi!
Ishara za Mimba ya Miezi 4

- Mimba kuanza kuonekana
- Kiungulia na kutatizika kuchakata chakula
- Kukosa pumzi
- Kuvimba mapua ama kuwa na homa mara kwa mara
- Kuvimbiwa
- Alama za kunyoosha kuanza kuonekana
- Ufizi kuvuja damu
- Maumivu ya mgongo
Matatizo kama kushikana mapua yanasababishwa na damu nyingi kupita kwenye mishipa. Mwili wako unaongeza damu inayotengenezwa mwilini kutoka mwezi huu hadi wiki 35 ya ujauzito. Huku matatizo kama kiungulia yakisababishwa na kukua kwa uterasi kunako songesha baadhi ya viungo mwilini.
Uzito wa mwili
Katika mwezi wa nne, utakuwa umeanza kushuhudia ongezeko la uzito mwilini. Utakuwa na hamu ya kupindukia ya kula vyakula fulani huku ukivichukia vyakula vingine. Daktari wako atakushauri uzito unaopaswa kuongeza katika kila mwezi. Ikiwa una shaka kuwa unaongeza uzito kwa kasi sana, wasiliana naye.
Ukuaji wa fetusi katika mwezi wa nne

Katika mwezi wa nne, mtoto ana urefu wa nchi nne ama tano na uzito wa ounsi 5. Ngozi yao pia ni nyepesi. Viungo vya fetusi kama vile macho na maskio vimekua pamoja na vya uzalishaji vilivyoanza kukua kwa kasi.
Mwendo wa fetusi kwenye uterasi
Huenda ukaanza kuhisi mwendo wa fetusi tumboni katika mwezi wa nne. Usiwe na shaka usipohisi, huenda mtoto wako ataanza mwezi ujao.
Fanya haya katika mwezi wa nne wa mimba
Nunua mavazi ya ujauzito. Kadri siku zinavyozidi kupita ndivyo unavyozidi kuongeza uzito na mimba yako kukua. Ni muhimu kwa mama kuwa na mavazi mapya yasiyo mbana na yanayomwezesha kutembea kwa urahisi na kwa starehe zake.
Kuzingatia lishe bora. Lishe yako ina umuhimu mkubwa kwa afya yako na ya mtoto. Hakikisha kuwa unakula lishe bora iliyo na virutubisho muhimu mwilini. Hakikisha kuwa sahani yako ina wanga, protini, fiber, madini, vitamini na maji.
Ishara za hatari katika mimba
Katika mimba ya miezi 4, umetoka kwa kipindi cha hatari. Hata hivyo, unahimizwa kuzidi kuwa makini na afya yako. Unapogundua mojawapo kati ya ishara hizi, usisite kutembelea kituo cha afya.
- Kuvuja damu inayojaza pedi
- Maumivu makali ya mgongo
- Kuvuja damu inayoongezeka kwa kiwango
- Joto jingi
- Uchungu mwingi unapokojoa
- Maumivu makali ya kichwa
- Kuharisha na kutapika
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kuboresha Nafasi Ya Kupata Mimba Kwa Kasi Kwa Kutumia Staili Hizi