Je, Mwanamke Aliye Na Mimba Anapaswa Kulala Vipi?

Je, Mwanamke Aliye Na Mimba Anapaswa Kulala Vipi?

Sleeping while pregnant is a different experience. To keep your baby safe and enjoy a relaxing sleep, there are sleeping positions you have to apply.

Huenda ikawa jambo gumu kujua unavyo paswa kulala ukiwa na mimba. kwani mimba na kulala vyema yana ambatana. Mwanamke aliye na mimba anapaswa kulala vipi? Kuna uwezekano uliweza kulala vyema katika trimesta yako ya kwanza ila vitu huenda vikabadilika katika trimesta yako ya tatu. Kuna njia ambazo mwanamke aliye na mimba anapaswa kulala ili apate usingizi mwanana na amlinde mtoto wake.

Tumbo yako inapo endelea kukua, homoni huanza kuongezeka mwilini na, huenda ikawa vigumu sana kupata mbinu ya kulala inayo kufaa ama kupata usingizi. Kuongezeka kwa homoni mwilini huenda kukakufanya ukose usingizi na matatizo mengineyo kama vile uchungu wa mgongo na shida za kupumua.

Kulingana na Christy LeBlanc, mkunga wa Calgary, “Iwapo una tatizika kulala, ninge kushauri kuandika ili uweze kusema unacho waza,” alishauri.” Pia kusoma kitu kisicho sisimua kama vile kitabu chako cha simu- huenda kukasaidia kutoa fikira nyingi na kurejesha usingizi wako.”

LeBlanc pia alishauri kuchukua muda na kutembea dakika 30 ama kufanya mazoezi mengine kama vile yoga ili kutoa fikira nyingi na kuboresha mtiririko wa damu. Matibabu ya misa na ya mifupa husaidia pia.

Je, mwanamke aliye na mimba anapaswa kulala vipi?

Je, mama mja mzito anapaswa kulala kivipi?

Tuna angazia mambo muhimu ambayo mama mja mzito anapaswa kujua kuhusu kulala vizuri.

  • Kulala kwa upande

Njia hii ya kulala inajulikana kama SOS. Njia hii ni bora zaidi ukiwa katika trimesta yako ya pili na ya tatu, haswa kwa upande wako wa kushoto. Inasaidia mtiririko bora zaidi wa damu na kijusi kinacho kua. Kulala kwa upande wako wa kushoto kunasaidia kupeleka virutubisho na damu kwa kondo la nyuma na hatimaye kwa mtoto. Pia nafasi hii inaweza kuliweka kondo lako la nyuma mbali na maini yanayo patika upande wa kulia. Hakikisha miguu na magoti yako yame kunjwa kuepuka kufanyisha roho yako kazi zaidi.

Je, mwanamke aliye na mimba anapaswa kuepuka kulala kivipi?

Unapo kuwa mja mzito, unapaswa kuepuka kulala kwa njia zifuatazo.

  1. Kulala kwa kisogo

Unapo endelea kuongeza kipimo cha kiuno chako na matiti yako kukuwa laini zaidi, kulala kwa tumbo hakuna starehe. Unapaswa kuepuka njia hii ya kulala unapokuwa mja mzito. Hii ni kwa sababu uzito wa uterasi yako huufinya uti wa mgongo wako na huenda lika athiri mtiririko wa damu kwa mwanao ulio mbeba.

Pia kulala kwa mgongo husababisha matatizo mengine kama:

  • Nyusi, kuumwa na misuli na uvimbe.
  • Shinikizo lako damu laweza lika enda chini na kukufanya uhisi Kizungu zungu unapo jaribu kusimama ama kukaa chini.
  1. Kulala kwa tumbo/ ukitizama chini

Unaweza kulala kwa tumbo unapokuwa mja mzito, ila tumbo lako linapo endelea kukua, itakupasa kuwacha kufuatia sababu tofauti.

mimba na kulala vyema

Nini kinacho tendeka ninapo amka baada ya kulala kwa kisogo?

Usiwe na wasiwasi, unapo amka kwa kisogo chako usiku, kuna njia unazo faa kufuata. Unapo jipindua usiku na kulala kwa mgongo, mwili una njia zake za kuhisi Kizungu zungu na kutapika kabla ya mtoto kuwa katika hatari yoyote ile ya kukosa hewa. Na mwili wako uta pinduka hata kama umelala. Jambo hili hutendeka kabla ya mwili wako kuwa mzito sana na kufinya mshipa.

Mimba na kulala vyema: Mbinu za kupata starehe unapo lala

Wana wake wengi waja wazito hawaja zoea kulala kwa upande. Kwa miaka mingi watu wengi huzoea kulala kwa upande mmoja. Hizi ni miongoni mwa mbinu unazoweza kuzingatia kupata starehe unapolala.

Kutumia mito: pitisha miguu yako pande tofauti na uweke mto katikati. Pia unaweza kuwa na mto mmoja nyuma ya mgongo wako. Ama jaribu michanganyiko tofauti ili kupata moja kati ya hizo ambazo Itakupendeza.

mimba na kulala vyema

Mto maalum: unaweza ukanunua mto maalum wa kukupa starehe unayo ikusudia. Lina mwundo wa kabari na lina julikana kama mto wa uja uzito.

Jaribu kutumia recliner: iwapo una recliner, jaribu kuilalia uone utakavyo hisi. Inakusaidia kulala vyema.

Kupunguka kwa pumzi: lala kwa upande na uwekelee mto mahali ambapo mkono wako mmoja utalala. Itasaidia kukiinua kifua chako.

Hitimisho

Huenda ukawa ume jaribu njia hizi za kulala tulizo taja na bado una amka ukihisi kuumwa na mwili kila asubuhi. Huenda unacho hitaji ni godoro ngumu.  Godoro ngumu itasaidia kuipa torso yako msaada na pia miguu, na kukusaidia kuzoea mbinu yako mpya ya kulala. Mimba na kulala vyema ni mambo ambayo yana ambatana. Hakikisha unalala ipasavyo ukiwa na mimba.

 

 

 

 

 

 

Read also: Leg cramps during pregnancy while sleeping

Written by

Risper Nyakio