Mimba Ni Nini? Maana Na Ishara Maarufu Za Mimba

Mimba Ni Nini? Maana Na Ishara Maarufu Za Mimba

Kufahamu mimba ni nini na ishara za mapema za mimba kunamsaidia mama kufahamu wakati anapo stahili kwenda kwenye kituo cha afya.

Mimba ni nini? Mimba ni hali ambapo fetusi huanza kukua tumboni mwa mwanamke na baada ya miezi tisa, hujifungua mtoto. Safari ya mimba huanza na manii kurutubisha yai la mwanamke linapo achiliwa kutoka kwa ovari. Baada ya yai kurutubishwa, yai husafiri kupitia kwa mirija ya ovari hadi kwenye uterasi na kujipandikiza kwenye kuta zake. Yai linapo jipandikiza vyema, mimba hufanyika.

Kuna kesi ambapo yai hujipandikiza nje ya mji wa mtoto. Kama vile kwenye mirija ya ovari ama tumbo ya chini na kusababisha hali inayo fahamika kama mimba ya ectopic.

Kwa wastani, mimba huchukua wiki 40 kabla ya mtoto kuzaliwa. Ili kuwa na mimba yenye afya, mwanamke anapaswa kuanza utunzaji wa kabla ya kujifungua mapema anapo gundua hali yake. Kwa njia hii, ata tunzwa ipasavyo na kuongeza nafasi zake za kujifungua mtoto mwenye afya.

Ishara za mimba

mimba ni nini

Baada ya kujibu swali la mimba ni nini? Kufahamu dalili za mimba kutamsaidia mwanamke kufahamu wakati anapo hitajika kutembelea kituo cha afya.

  • Kukosa kipindi cha hedhi

Kukosa kipindi cha hedhi ni ishara ya mapema ya mimba na iliyo maarufu zaidi. Kuna sababu zingine ambazo zinaweza fanya mwanamke akose kupata kipindi chake cha hedhi. Kuna wanawake walio na vipindi visivyo vya kawaida na huenda vipindi vyao vikachelewa ama kukosa kuja. Kuna hali za kiafya ambazo huenda zikamfanya mama kukosa kipindi chake cha hedhi.

  • Kuvuja damu nyepesi

Yai linapo jipandikiza kwenye kuta za uterasi, huenda matone ya damu yaka toka. Hii pia ni ishara nyingine maarufu ya mimba. Hushuhudiwa wiki mbili baada ya kurutubishwa kwa yai.

Kutoa damu mapema katika ujauzito huenda kukawa kufuatia hali kama vile maambukizi. Ni vyema kufanyiwa vipimo kuhakikisha kuwa mama ako salama.

  • Kiungulia

mimba ni nini

Mimba huambatanishwa na mabadiliko ya viwango vya homoni mwilini. Na kusababisha hali ya kiungulia.

  • Kuumwa na mgongo

Mabadiliko ya homoni mwilini na kushinikizwa kwa misuli ya mwili husababisha maumivu ya mgongo mapema katika ujauzito.

  • Kutapika

Kuhisi kutapika na kutapika huandamana na ugonjwa wa asubuhi. Ishara inayo tokea katika miezi ya kwanza nne. Kudhihirisha kuwa una mimba. Husababishwa na ongezeko la homoni mwilini baada ya yai lililo rutubishwa kujipandikiza kwenye kuta ya uterasi.

Kwa sasa kwani unafahamu mimba ni nini na ishara za mapema za mimba. Kuwa mwangalifu unapo gundua mojawapo ya ishara hizi na uanze kliniki ikiwa una mimba.

Chanzo: WebMD

Soma PiaSababu 3 Kuu Za Matokeo Hasi Ya Kipimo Cha Mimba Hata Baada Ya kuwa Na Ishara

Written by

Risper Nyakio