Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Miaka Zaidi Ya 35

Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Miaka Zaidi Ya 35

Wanawake wanapo fikisha miaka 30 hushuhudia punguko katika uzazi wao. Na kupata mimba katika umri huu huwa na hatari nyingi.

Kupata mimba ukiwa na miaka zaidi ya 35 sio jambo rahisi. Kupevuka kwa yai hupunguka mwanamke anapo fikisha miaka ya thelathini na saizi ya mayai yake kuanza kupunguka pia. Kupevuka kwa yai huwa kume athiriwa na kusababisha mabadiliko kwenye homoni zake.

Huenda pia kukawa na upungufu katika nambari na afya ya mayai ya mwanamke yanayo pevuka; kwa sababu ya jambo hili, mwanamke hashauriwi kutunga mimba akiwa na miaka zaidi ya 35.

pregnant over 35

Ni matatizo gani yanayo husika na kupata mimba ukiwa na miaka zaidi ya 35?

Hatari zinazo husikana na umri

Ni kweli kuwa sayansi ya matibabu ime imarika na leo wanake wenye umri zaidi ya miaka 35 wana beba mimba salama. Walakini, kuna hatari nyingi zinazo husika na kuchelewesha kujifungua na nafasi za kutunga mimba iliyo ya afya na mtoto aliye na afya hupunguka umri wa mwanamke unavyo zidi kuongezeka.

Kisayansi imedhibitika kuwa wanawake, wanao jifungua watoto wakiwa katika miaka yao ya thelathini, huwa na nafasi nyingi za kupata mtoto aliye na matatizo ya kuzaliwa. Sababu inayo husishwa na tatizo hili mara nyingi ni umri wa mama, yai hugawanyika kwa njia isiyo ya kawaida.

Matatizo mengine huenda yaka ibuka

Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Miaka Zaidi Ya 35

Shinikizo la juu la damu na kisukari ni matatizo ambayo yanaweza tokeo ukiwa na mimba. Kwa hivyo, wanawake wenye umri zaidi ya 30 wako katika hatari zaidi.

Ikiwa una mimba na una umri zaidi ya miaka 35, ni muhimu upate utunzi kabla ya kujifungua wa mapema na mara kwa mara ili upate vipimo vya mapema na matibabu yanayo faa.

Stillbirth (kuzaliwa kwa mtoto aliyekufa kabla ya kujifungua) hushuhudiwa zaidi katika wanawake wenye umri wa miaka 35. Wanawake wazee huwa na nafasi zaidi za kujifungua watoto walio na uzito mdogo (chini ya kilo 2.5). Kujifungua kupitia kwa upasuaji wa C-section kuna shuhudiwa zaidi kwa wanawake wanao pata mtoto wao wa kwanza wakiwa na umri wa miaka 35.

Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Miaka Zaidi Ya 35

Ni jambo la busara kwa wanawake kupatana na madaktari wao kushauriwa. Historia ya kimatibabu ya wazazi wote inaweza saidia kujua matatizo ambayo huenda yaka athiri afya ya mama na mtoto.

Pia ni nafasi ya kuangalia ujauzito wako ulivyo na kupata vipimo vya damu kama vile kinga ya rubella, vipimo vya screening kama vile cervical smear zinazo fanyika kabla upate mimba.

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Roshni Mahtani na kuchapishwa kwa mara ya kwanza kwenye TheAsianparent

Soma pia: Matatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

Written by

Risper Nyakio