Mimba Ya Bahati Mbaya Ama Usiyo Tarajia: Huenda Likakufanyikia

Mimba Ya Bahati Mbaya Ama Usiyo Tarajia: Huenda Likakufanyikia

Mbinu za kukinga dhidi ya mimba ni nyingi na kuna elimu bila gharama kwenye vituo vya hospitali. Ikiwa hauko tayari kupata mimba, hakikisha kuwa unatumia kinga.

Mimba isiyo pangiwa ni maarufu sana kuliko unavyo dhania. Nambari kubwa ya mimba nchini huwa mimba isiyo pangwa ama wengine huenda waka iita mimba ya bahati mbaya. Ikiwa wewe ni mwanamke ambaye hajafikisha umri wake wa ugumba, una nafasi kubwa ya kupata mimba wakati wowote. Ila pale ambapo una matatizo ya kiafya ambayo huenda yaka tatiza uwezo wako wa kupata mimba kwa kirahisi.

Mtoto ni gharama na anahitaji vitu vingi. Unapaswa umtunze, umpe mahitaji yake ya kimsingi (nyumba, mavazi na elimu) na mahitaji mengine. Ni vyema kwa wanandoa kuwa maksudi na nia yao ya kupata mimba. Ikiwa unahisi kuwa hauna uwezo wa kifedha na wa kihisia wa kumlea mtoto, una shauriwa kungoja hadi pale utakapo hisi kuwa uko tayari kumpata na kumlea mtoto.

Mimba ya bahati mbaya: Inavyo tendeka

mimba isiyo pangwa

Mimba isiyo pangwa hufanyika pale ambapo watu wawili; wa kike na kiume huji husisha katika tendo la ngono bila kutumia kinga ama vidhibiti uzalishaji. Kuna mbinu nyingi za kuji kinga kutokana na mimba. Hizi ni kama vile, kutofanya ngono, kutumia kondumu, kutumia IUD, ama tembe za kudhibiti uzalishaji.

Njia ya kipekee iliyo na asilimia 100 ya kinga ni kujitenga na kufanya ngono. Mbinu zingine bado zitakukinga ila, ajali hutendeka na huenda ukapata mimba. Mbinu kama ya kutumia kondomu, huenda ika pasuka na manii kupita kwenye uke wa mwanamke, na kumfanya apate mimba. Unaweza kunywa tembe za asubuhi kudhibiti mimba baada ya kondomu kulipuka. Hakikisha kuwa umechukua tembe hizo kabla ya siku tatu kupita kutoka mlipo fanya kitendo kile. Kutoka hapo, nafasi za kinga zina pungua na unakuwa na nafasi zaidi za kupata mimba.

Kwa nini mimba isiyo pangwa huwa maarufu

kudhibiti mimba, kondomu

Sababu kuu kwa nini kuna mimba ya bahati mbaya ni kwa wanandoa kuto tumia kinga yoyote dhidi ya mimba. Kuna baadhi ya wanawake wasio na maarifa tosha kuhusu mbinu za kujikinga dhidi ya mimba. Elimu kuhusu mbinu za kudhibiti uzalishaji ni bure katika vituo vya afya. Ni vyema kwa kila mwanamke na mwanamme kupata elimu hii ili afahamu mbinu zinazo mfaa kuji kinga dhidi ya kupata mimba na maambukizi ya kingono.

Kumbuka kuwa, hata kama umetatizika na uzalishaji hapo awali, bado una nafasi za kupata mimba unapo jihusisha katika tendo la kingono bila kinga. Kuna baadhi ya wanawake ambao hupata vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida, kumbuka kuwa hata kama una tatizika na jambo hili, huenda pia ukapata mimba. Hakikisha kuwa, kama huko tayari kupata mimba kuwa unatumia kinga.

Vyanzo: WebMd, NHS

Soma Pia:Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Kitunguu

Written by

Risper Nyakio