Sababu 6 Kuu Zinazo Sababisha Mwanamke Kupata Mimba Ya Ectopic

Sababu 6 Kuu Zinazo Sababisha Mwanamke Kupata Mimba Ya Ectopic

Histori ya maambukizi ya kingono, kama vile gonorrhoea kwenye mirija ama viungo vingine vilivyo karibu na uterasi huongeza hatari ya kupata mimba ya ectopic.

Mimba huanza yai lililo achiliwa kutoka kwa ovari linapo rutubishwa na manii. Yai lililo rutubishwa hupandikiza kwenye kuta za mji wa mtoto. Kwa mimba ya ectopic, yai lililo rutubishwa hupandikiza nje ya uterasi kama vile kwenye mirija ya ovari ama fallopian tubes. Jukumu la mirija hii huwa kupitisha yai kutoka kwa ovari hadi kwa uterasi. Mimba ya ectopic ni mimba inayo fanyika nje ya mji wa mtoto. Huenda ikawa kwenye mirija ya ovari, ovari, ama sehemu ya chini ya uterasi ama mlango wa uzazi.

Mimba ya aina hii haiwezi kua kwa kawaida. Isipo vumbuliwa mapema, huenda ikasababisha kuvuja damu na kuhatarisha maisha ya mama.

Ishara za mimba ya ectopic ni nini?

ectopic pregnancies

 • Kuhisi uchungu mwingi tumboni, shingo na mabega
 • Uchungu mwingi kwenye upande mmoja wa tumbo
 • Kuzirai
 • Kuvuja damu nyepesi ama nyingi zaidi

Kichefuchefu na chuchu zilizo fura ni ishara zilizo kawaida katika mimba ya kawaida na ya ectopic. Unapo hisi mojawapo ya ishara hizi, ni vyema kuwasiliana na daktari wako.

Walio katika hatari ya kupata mimba hii

mimba ya ectopic

 • Mimba ya awali ya ectopic. Mama aliye na mimba ya aina hii hapo awali ako katika hatari ya kutunga mimba ya aina hii tena.
 • Wanawake walio na miaka 35 na zaidi. Wanawake wanao jaribu kupata mimba wakiwa na miaka zaidi ya 35 wana hatari ya kupata hali hii.
 • Historia ya upasuaji wa pelviki, kutoa mimba mara nyingi
 • Kuvuta sigara. Utumiaji wa sigara kabla ya kupata mimba kunaweza ongeza hatari ya kutunga mimba ya aina hii.
 • Histori ya maambukizi ya kingono. Maambukizi kama vile gonorrhoea kwenye mirija ama viungo vingine vilivyo karibu na uterasi huongeza hatari ya kupata mimba ya aina hii.
 • Historia ya endometriosis

Kuepuka kupata mimba hii

Mwanamke anaweza punguza nafasi za kupata mimba ya aina hii kwa kufanya mambo yafuatayo:

 • Punguza wapenzi wake na kutumia kondomu kila mara anapo fanya mapenzi. Ili kumsaidia kuepuka maambukizi ya kingono.
 • Koma kuvuta sigara. Wacha uraibu huu kabla ya kuanza kupanga kupata mimba.

Soma Pia: Kutengeneza Uhusiano Na Mtoto Ukiwa Na Mimba Na Manufaa Ya Kiafya

Written by

Risper Nyakio