Dalili Za Mwanamke Mwenye Mimba Ya Mapacha

Dalili Za Mwanamke Mwenye Mimba Ya Mapacha

Kuhisi uchovu mapema katika safari yako ya mimba huenda ikawa ishara ya mimba ya mapacha.

Kujifungua mtoto ni baraka kubwa kwa wazazi, huwa baraka zaidi mama anapo barikiwa na mapacha. Je, ungependa kujifungua mapacha? Kuna uwezekano wa mama kujua anapokuwa na mimba ya mapacha? Dalili za kuwa na mimba ya mapacha ni kama zipi?

Unapo anza kushuhudia dalili za mimba, huenda ukawa na fikira nyingi, na kushangaa ama utakuwa na ishara zilizo kolea ama itakuwa kawaida. Iwapo hakuna ishara hasa ya kudhibitisha kuwa una tarajia mapacha unapokuwa mapema katika safari yako ya mimba, kuna vitu ambavyo huenda vika ashiria kuwa unatarajia watoto wawili na wala sio mmoja.

mimba ya mapacha

Ishara kuwa una mimba ya watoto wawili

Uchovu

Ishara hii ya uchovu hu shuhudiwa mapema katika safari yako ya mimba. Huenda ukaanza kuhisi uchovu hata kabla ya kukosa kipindi chako cha hedhi. Viwango vingi vya homoni mwilini vitakufanya uhisi kuchoka. Kuna imani kuwa unapokuwa na mimba ya watoto wawili, utahisi uchovu sana.

Ugonjwa wa asubuhi

Hii ni ishara maarufu ya kuwa na mimba, hata kama sio wanawake wote ambao hudhibitisha ishara hii. Kwa mara nyingi, huanza kushuhudiwa katika wiki ya nne ya ujauzito, karibu na wakati ambapo una kosa kipindi chako cha hedhi.

mimba ya mapacha

Baadhi ya wanawake walio na watoto zaidi ya mmoja hushuhudia viwango vikubwa vya ugonjwa wa asubuhi ikilinganishwa na wanao tarajia mtoto mmoja. Huenda ishara hii ikawa katika kipindi chao chote cha ujauzito. Huenda ikawa ni vigumu kudhibitisha ugonjwa wa kawaida wa wastani hasa ikiwa wewe ni mama wa mara ya kwanza. Pia kila ujauzito huwa na kiwango chake cha ugonjwa huu wa asubuhi. Iwapo unatapika sana, ni vyema kumtembelea daktari wako kuwa na uhakika kuwa mambo yote yako sawa.

Mpigo wa moyo wa pili

Unapokuwa na mimba, huenda ukaanza kuhisi mpigo wa moyo wa mtoto wako anapokuwa kati ya wiki 8 ama 10 kwa kutumia kifaa spesheli (fetal doppler). Unapo fanyiwa kipimo hiki, huenda daktari wako akagundua mpigo wa pili wa moyo, ishara dhibiti kuwa una tarajia watoto wawili.

Mwendo wa mapema

Huenda mama akaanza kuhisi mwendo wa mtoto tumboni anapokuwa wiki 18. Mtoto huanza mwendo tumboni mapema, ila utaanza kuhisi anapo fikisha wiki 18. Unapokuwa na mimba ya mtoto zaidi ya mmoja,  huenda ukaanza kuhisi mwendo huu mapema kuliko inavyo tarajiwa.

Uzito mwingi wa mwili

Katika trimesta yako ya kwanza, kuongeza uzito wa mwili hutendeka, kwa ongezeko la wastani huwa kilo 2 kwa wiki za kwanza 12. Ongezeko la uzito huzidi unapokuwa katika trimesta ya tatu ya safari ya mimba. Iwapo una gundua kuwa una ongeza uzito kwa kasi, ni vyema kuwasiliana na daktari wako ili kudhibitisha iwapo una mimba ya mapacha ama kuna sababu zinazo fanya hivyo.

Kufanya kipimo cha ultrasound

Dalili Za Mwanamke Mwenye Mimba Ya Mapacha

Iwapo sababu tulizo taja huenda zikawa ishara ya mimba ya mapacha, njia dhabiti na inayo kupatia matokeo sahihi ni kufanya kipimo cha ultrasound. Madaktari wengi wata ratibisha ultra sound unapokuwa katika wiki 6-10 kudhibitisha iwapo una matatizo yoyote katika ujauzito wako. Baada ya kufanya kipimo hiki, itakuwa bayana iwapo unatarajia mtoto mmoja ama zaidi.

Soma pia: Unapata Mapacha Kulingana Na Ishara Hizi Za Hadithi Za Kuambiwa

Written by

Risper Nyakio