Ishara kama kichefuchefu kingi, uchovu na maumivu kwenye chuchu huwa zimepungua katika mwezi wa sita. Tarajia kuona haya katika mimba ya miezi 6!
Ishara Za Mimba Ya Miezi 6

Katika trimesta ya pili, ugonjwa wa asubuhi huwa umeisha kwa wanawake wengi. Mbali na idadi ndogo ya wanawake wanaotatizika na kichefuchefu na kutapika hadi mwezi wa tisa. Ishara za mimba katika mwezi huu ni:
- Maumivu. Katika mwezi huu, tumbo limekuwa kubwa na nzito pamoja na uzito wa mama. Uzito ulioongezeka utamfanya mama ahisi maumivu kwenye miguu na mgongo.
- Kuvimbiwa. Mimba imekua na kushinikiza matumbo, hivi basi kupunguza uwezo wa kuchakata chakula kwa kasi.
- Kujikuna. Jinsi tumbo linavyokua ndivyo mama atakavyohisi kujikuna. Kunenepa kwa tumbo kutamfanya mama apate alama za kunyoosha.
- Kufura miguu. Kufuatia uzito ulioongezeka wa mtoto, huenda mama akawa na miguu iliyofura. Mishipa kwenye miguu huenda ikawa inaonekana kwani inafanya kazi zaidi ya kupitisha damu sehemu tofauti mwilini.
- Kiungulia na kuvimbiwa.
- Kuhisi njaa wakati wote na kula chakula kingi.
- Kuchukia harufu fulani.
Mabadiliko katika mwezi wa 6
- Tumbo linaonekana
- Kitovu kimetokea nje
- Ongezeko la uzito wa mwili
- Matiti yamekua
- Mishipa ya damu kuonekana
Hata hivyo, kwa mama ambaye ni mimba yake ya kwanza, huenda tumbo lake likawa ndogo. Wanawake wakonda huenda wakachukua muda zaidi kabla ya mimba yao kuonekana na walio warefu.
Ukuaji na mwendo wa fetusi katika miezi 6 ya mimba
Katika mwezi wa sita, fetusi ina uzito wa poundi 1 ama 2 na urefu wa nchi kati ya 6.5 hadi 12.5. Mafua na mikono yake imekua ipasavyo. Anaweza kusikia sauti nje ya uterasi, kama watu wanaozungumza na mamake. Mtoto huwa na mwendo katika mwezi huu na anaweza kurusha mateke. Mama atafahamu mtoto wake anapokuwa ameamka na akiwa hai ama active zaidi.
Mambo muhimu ya kufanya katika mwezi wa 6

- Anza kutayarisha chumba na kitanda cha mtoto
- Jisajilishe na hospitali ambayo ungependa kujifungulia
- Kuhakikisha kuwa una pesa za hospitali na mahitaji ya mtoto baada ya kujifungua
- Kuwa na wakati tosha na mchumba wako
- Kuendeleza mazoezi. Mazoezi katika kila trimesta huwa tofauti
- Pata mapumziko tosha
Wakati wa kumwona daktari
- Maumivu makali ya mgongo ama tumbo
- Maji kuvuja
- Kuvuja damu nyingi kutoka kwa uke
- Kuhisi uchungu unapokojoa
- Kutapika ama kuharisha
- Kupunguka kwa mwendo wa fetusi
- Joto jingi zaidi ya siku moja
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Manunuzi Muhimu Ya Mtoto Kabla Ya Kwenda Katika Chumba Cha Kujifungua