Huu ndio utakuwa mwezi wako wa kutabasamu. Kichefuchefu na mabadiliko mengine ya mwili inayotokana na homoni za ujauzito yako nyuma yako. Unaweza kutulia na kufurahia ujauzito na mtoto unayetarajia. Ni mambo gani itanukuu mimba ya miezi mitano?
Mimba Ya Miezi Mitano

Hivi sasa tumbo lako limeanza kuwa kubwa lakini si kubwa kukuzuia kufanya kazi zako. Katika hii trimester ya pili, unaweza tarajia kuongeza uzani. Watu wengi huwa hawaongezi uzani kwenye trimestrer ya kwanza sababu ya kichefuchefu.
Katika miezi mitano si tumbo lako tu ambalo linakua mbali pia hamu yako ya chakula. Pia nywele na kucha zako zimekua kwa haraka sana. Utaweza kutarajia:
- kiungulia
- maumivu ya miguu
- kuvimba kwa miguu
- kuvimbiwa
- kizunguzungu
- Kuumwa na kichwa
- Maumivu ya mgongo
- Mabadiliko ya ngovi kama vile chuchu kuwa nyeusi
- Msongamano wa pua
- Kubadilika kwa kitovu chako
Katika miezi mitano mtoto wako ana urefu wa inchi sita ama saba. Hii kumaanisha wanatoshana na ndizi. Wanakua ngozi ambayo hukinga mtoto kutokana na amniotic fluid inayomzingira mtoto. Pia wanajifunza kunyonya vidole, kugeuka, kupepesa macho na kuitikai sauti kutoka nje.
Pia unafaa kuwa unaanza kuskia mtoto akisonga ndani ya tumbo lako. Iwapo hujaskia chochote ni sawa kabisa. Mara nyingi kwenye ujauzito utaweza kuhisi huku kusonga kwa mtoto kunakofahamika kama quickening kati ya wiki 16 hadi 20. Ila kila mtoto ni tofauti.
Saizi na vile mtoto alivyokaa kwenye plasenta inaweza kuwa sababu kuu kama utamskia mtoto wako akisonga au la. Ila kwa huu mwezi unafaa kuwa unahisi kusonga ata kwa umbali.
Mazoezi Na Lishe Katika Miezi Mitano

Iwapo mimba yako haina hatari ni vyema kudumisha ratiba ya mazoezi. Vile unavyofanya mazoezi kwa sasa ndivyo mwili wako utakuwa tayari kwa uchungu wa uzazi na pia kupona baada ya kujifungua. Lakini hili hubadilika kama mimba yako iko hatari. Hivyo ni vyema kupata ushauri wa daktari.
Mazoezi yaliyo sawa na salama kuendelea nayo ni kama vile:
- Kutembea ama kukimbia
- Mazoezi ya yoga
- Kuogelea
- Kufanya hiking
- Kujihusisha na darasa za densi
- Mazoezi ya kujinyoosha na kuinua miguu
Kuzingatia lishe, inashauriwa kula kalori 300 zaidi kwa kila siku katika trimester ya pili. Hii ni kuwa mtoto anahitaji chakula. Haishauriwa kupata hizi kalori kutoka kwa chakula kisicho na lishe bora. Lakini wakati mchache unaeza kula unachotaka ila hakikisha kuwa chakula chako kina:
- Vyanzo vya protini kama vile kuku,samaki
- Maziwa na bidhaa zake kama maziwa ya mgando
- Nafaka zisizokobolewa
- Matunda na mboga
- Mafuta kama inayopatikana kwenye mbegu, karanga na parachichi
Unafaa Kumwona Daktari Lini?
Hivi sasa unafahamu vyema ni mambo gani hatarishi kwa ujauzito wako ama yanayohitaji uangalizi kwa makini. Ila hii orodha itakukumbusha:
- Kuvunja damu kutoka kwa uke
- Uchungu mwingi na maumivu kwenye mgongo
- Kuongezeka kwa joto la mwili
- Uchungu unapoenda haja ndogo, inaweza kuwa ishara ya maambukizi.
- Kutapika ambako ni zaidi ya kichefuchefu
- Harufu kutoka kwenye mkojo ama ukeni.
Hii trimester ya pili haswa mimba ya miezi mitano hufahamika kama honeymoon kwani ni wakati wako wa kujiburudisha. Fanya mazoezi, tarajia kusonga kwa mtoto wako na pia furahia picha ya kwanza ya ultrasound.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kutumia Baking Soda Kudhibitisha Hali Ya Mimba