Kwa mama ambaye hii ni mimba ya kwanza, huenda ikawa mimba yake haionyeshi akiwa na miezi mitatu. Wanawake wengi wenye misuli yenye nguvu huanza kuonyesha kuwa wana mimba katika mwezi wa nne ama tano. Kwa wanaoonyesha mapema pia ni sawa, kwani kila mwanamke huwa na mwili tofauti. Baada ya mimba ya kwanza, mwanamke huanza kuonyesha kuwa ana mimba mapema zaidi. Uzito, urefu na nguvu za misuli za mwanamke huathiri wakati ambapo mimba yake itaanza kuonekana.
Mimba Ya Miezi Mitatu

Ukuaji wa fetusi ya miezi mitatu
Katika mwezi huu, fetusi iko kati ya urefu wa nchi 2 hadi 3 na uzito sawa na limau. Hata kama mama hahisi chochote, kuna mengi yanayofanyika tumboni. Haya yanafanyika mwilini mwa mtoto:
- Mfumo wake wa misuli, kuchakata chakula, na mifupa unakua
- Figo zinaanza kufanya kazi
- Kucha za miguu na mikono zinaanza kumea
- Sehemu za siri zinaanza kumea
- Seli nyeupe zinaanza kutengenezwa mwilini
Mambo muhimu kufanya katika mwezi huu
- Zungumza na daktari wako kuhusu kufanya mazoezi na mazoezi yanayokubalika katika mimba. Kuna baadhi ya mazoezi ambayo sio salama katika mimba na ni vyema kwa mama kujitenga nayo katika kipindi hiki.
- Hakikisha unachukua vitamini za prenatal inavyofaa.
- Zingatia ulaji wa vyakula vyenye umuhimu kwa mwili. Hakikisha kuwa kila lishe ina kiwango tosha cha protini, bidhaa za maziwa, wanga, mboga na matunda. Jitenge na ulaji wa vitamu tamu na vyakula vilivyo kaangwa kwa ufuta mwingi.
- Kunywa maji tosha kwa siku. Maji katika mimba yanasaidia na uchakataji wa chakula na pia kusaidia kutengeneza amniotic fluid inayomlinda mtoto.
Wakati wa kumwona daktari

Miezi ya hatari katika mimba huwa mwezi wa kwanza na wa pili, katika mwezi wa tatu, umetoka kwenye kipindi cha hatari cha mimba. Hata hivyo, ni vizuri kuwa na ufahamu wa ishara za hatari katika mwezi huu. Wasiliana na daktari wako unapogundua una zaidi ya ishara moja kati ya hizi.
- Maumivu makali ya tumbo
- Kuumwa vikali na mgongo
- Joto jingi isiyopungua wala kuisha kwa kipindi kirefu
- Ishara za maambukizi ya uke kama vile harufu kali kutoka sehemu ya uke
- Kuumwa unapopitisha mkojo
- Kutapika mara kwa mara. Na kufanya iwe vigumu kula bila kutapika
Safari ya ujauzito ya kila mwanamke huwa tofauti. Ishara za mimba ya miezi mitatu zitakuwa tofauti kwa kila mwanamke. Mwanamke hapaswi kulinganisha mimba yake na ya mwanamke mwingine. Kilicho muhimu zaidi ni kuwasiliana na daktari unapokuwa na shaka kuhusu chochote kile katika safari yako ya mimba.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji