Hongera! Una mimba ya mapacha, wanandoa wengi hutamani kupata ujauzito wa mapacha, ilas sio wote wanaobahatika, shukuru Maulana kwa zawadi hii. Kuna wanawake wanaoanza kufahamu kuwa wana mimba katika mwezi wa tatu wa mimba. Kwa wanawake wanaopata mimba ya mapacha sio rahisi kufahamu kuwa wanatarajia mtoto zaidi ya mmoja, ila kuna ishara ambazo zinaweza dokeza hili. Tazama ishara za mimba ya miezi mitatu mapacha.
Vitu Vinavyoongeza Nafasi Za Mama Kupata Mapacha

- Wakati ambapo baadhi ya wakati mimba ya mapacha hufanyika tu, kuna baadhi ya vitu ambavyo huongeza uwezekano wa mama kushika mimba ya mtoto zaidi ya mmoja.
- Historia ya familia. Kutoka kwa familia iliyo na historia ya kupata watoto mapacha kunaongeza nafasi za mwanamke kushika mimba ya watoto mapacha.
- Kutunga mimba mama anaponyonyesha ama akitumia uzazi wa mpango. Mabadiliko ya viwango vya homoni mwilini kunaongeza nafasi za kushika mimba.
- Umri wa mama. Wanawake wanaoshika mimba wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 35 wana uwezo zaidi wa kupata mapacha.
- Matibabu ya uzalishaji. Matibabu ya vichocheo kama IVF (in vitro fertilization) yanaongeza nafasi za mama kupata mimba ya mapacha.
Ishara za mapema za mimba ya mapacha

- Kuwa na viwango vya juu vya hCG
- Kuhisi mwendo wa fetusi tumboni mapema
- Kuongeza uzito kwa kasi
- Tumbo kuwa kubwa kuliko tumbo ya wastani katika mwezi huo wa mimba
- Ishara zilizozidi za mimba. Ishara za mimba za kawaida ni kama vile, ugonjwa wa asubuhi, hamu iliyozidi ya kula, uchovu, na haja ya kwenda msalani mara kwa mara. Sio jambo la kushangaza kuwa mimba ya mapacha itakuwa na ishara zilizozidi. Mama mwenye mimba ya mapacha huenda akawa na hamu nyingi zaidi ya kula, uchovu mwingi na kuchoka sana.
Mimba ya miezi mitatu mapacha
Haya ndiyo yanafanyika kwa mtoto wako tumboni.
- Vidole vya miguu na mikono na kucha zinaanza kuonekana. Katika mwezi wa tatu wa mimba, vidole vya mtoto vinaanza kukua kisha kucha kumea.
- Maumbile ya uso kuanza kuonekana. Mapacha wanapofikisha miezi mitatu, uso wao unaanza kuonekana vyema. Sehemu kama mapua, macho na ulimi zitaanza kumea katika mwezi huu.
- Katika mwezi huu, fetusi huwa zimeanza kuwa na mwendo tumboni hata mama asipohisi kinachoendelea kwenye uterasi. Wanarusha mateke na kunyoosha misuli yao. Kope zinaanza kufunika macho. Katika mwezi huu, kichwa huwa nusu ya saizi yao.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Je, Kuna Kipindi Bora Cha Kupata Mimba? Siku Bora Za Kupata Mimba