Sababu Zinazo Sababisha Mama Kupata Mimba Ya Mtoto Zaidi Ya Mmoja

Sababu Zinazo Sababisha Mama Kupata Mimba Ya Mtoto Zaidi Ya Mmoja

Mwanamke anaweza tibiwa ili kuchechemua kupevuka kwa yai ama kutoa mayai mengi ya kurutubishwa na kusababisha kujifungua kwa mtoto zaidi ya mmoja.

Unapata hamu ya kupata mtoto unapo ona watoto mapacha? Hauko peke yako. Walakini, ikiwa ungependa kupata watoto mapacha, kufahamu vyanzo vya mimba ya mtoto zaidi ya mmoja ni mahali pazuri pa kuanza.

Vyanzo vya mimba ya mtoto zaidi ya mmoja

mimba ya mtoto zaidi ya mmoja

Vyanzo maarufu vya mama kupata mimba ya mapacha ama zaidi ni kufuatia vyanzo asili kama:

Urithi: Mwanamke aliye na historia ya familia ya watoto mapacha ana nafasi zaidi ya kujifungua mtoto zaidi ya mmoja kwa mara moja

Umri zaidi: Una nafasi zaidi za kupata mapacha ikiwa una miaka zaidi ya 30. Ni rahisi kusikia wanawake wenye umri zaidi wakipata watoto mapacha

Historia ya mimba ya mapacha: Nafasi za kujifungua mtoto zaidi ya mmoja ni nyingi ikiwa umefanya hivi hapo awali.

Kuna sababu zingine za kiteknolojia kama vile:

Matibabu: Mwanamke anaweza tibiwa ili kuchechemua kupevuka kwa yai ama kutoa mayai mengi ya kurutubishwa na kusababisha kujifungua kwa mtoto zaidi ya mmoja

Kurutubishwa kwa vitro: Kusaidia wanandoa kujifungua, wanaweza saidiwa na teknolojia za uzalishaji. Kupevushwa kwa yai kuna chechemuliwa kutoa mayai zaidi, na yanapo rutubishwa, yana rudishwa kwenye uterasi kukua.

Ishara za mimba ya mapacha

mimba ya mtoto zaidi ya mmoja

Kila mwanamke hushuhudia ishara tofauti, lakini unaweza angalia ishara hizi kwa ujumla:

  • Ugonjwa wa asubuhi ulio zidi
  • Hamu ya kula iliyo ongezeka
  • Uterasi kubwa kuliko ilivyo kusudiwa
  • Kuongeza uzito mwingi hasa katika siku za kwanza za ujauzito
  • Mwendo wa fetusi katika sehemu tofauti za tumbo wakati sawa

Mambo muhimu ya kufanya unapo kuwa na mimba ya mapacha

  • Lishe iliyo ongezeka

Utahitaji kuchukua kalori zaidi ya mwanamke aliye na mimba ya mtoto mmoja. Hii ni kwasababu una fetusi mbili ama zaidi zinazo hitaji iron, protini na virutubisho vingine. Huenda ukahitajika kuongeza uzito zaidi kuliko unavyo kusudiwa ili uweze kubeba fetusi hizo hadi zikomae.

  • Kuenda hospitalini mara kwa mara

Huenda ukahitajika kutembelea kituo cha hospitali mara kwa mara kuwasiliana na daktari wako na kuangalia ikiwa mimba yako inakua jinsi inavyo stahili.

  • Kumwona mtaalum

Huenda ikawa muhimu kwako kumwona mtaalum wa afya ya kujifungua na fetusi anaye julikana kama perinatologist. Mtaalum huyu ata kupima kutahini ultrasound yako.

  • Kupumzika zaidi

Ili kudhibiti mimba ya mapacha ama zaidi, utahitajika kupumzika zaidi. Huenda ikawa nyumbani ama hospitalini na mara nyingi huanza katika trimesta yako ya pili, hasa kama unabeba zaidi ya fetusi mbili.

  • Kupima fetusi zako

Fetusi hizi zitahitaji vipimo zaidi kuangalia afya yao, hasa ikiwa kumekuwa na changamoto mahali.

Jinsi ya kutunza watoto hawa baada ya kujifungua

Mara nyingi, kujifungua kwa mapacha hutendeka mapema kidogo kuliko inavyo tarajiwa, yenye maana kuwa wao huzaliwa wakiwa wadogo na wasio weza kujilisha peke yao. Katika kisa hiki, utahitaji kubaki hospitalini kwenye utunzi spesheli hadi pale ambapo wanaweza kula, kukua na kuwa na joto. Walakini, ikiwa watoto wako walizaliwa wakati walio tarajiwa, huenda wakati wako kwenye kitengo cha utunzi spesheli uka punguka.

Baada ya kutoka hospitalini, kuwanyonyesha mapacha wako ni kazi ngumu, lakini inayo wezekana. Utahitaji msaada kutoka kwa wanafamilia na marafiki wako kufanya majukumu ya nyumba ili upate wakati tosha wa kuwachunga wanao.

Soma PiaDalili Za Mwanamke Mwenye Mimba Ya Mapacha

Vyanzo: Daily Post, CHW, Better Health

Written by

Risper Nyakio