Dalili za mimba ya mwezi mmoja hutofautiana kati ya wanadada. Wanawake wengi hugundua kuwa wana mimba katika mwezi huu. Wengi wao baada ya kukosa kupata hedhi ya mwezi huo, kisha wanafanya kipimo cha mimba.
Mimba Ya Mwezi Mmoja: Mabadiliko Yanayofanyika Mwilini

Kichefuchefu. Huwa ishara ya mapema zaidi ya ugonjwa wa asubuhi. Mwanamke anaweza anza kuhisi kichefuchefu katika mwezi wa kwanza.
Uchovu. Mwanadada huanza kuhisi uchovu kila wakati hata anapoamka, kufuatia kubadilika kwa homoni mwilini na homoni ya mimba ama hCG kuzidi mwilini.
Maziwa kufura. Maziwa na chuchu za mwanamke huanza kufura na kuwa laini zinapoguswa kufuatia ongezeko la homoni mwilini.
Haja ya kwenda msalani mara kwa mara. Homoni ya mimba humfanya mwanamke kuhisi haja ya kwenda msalani mara kwa mara.
Kuchagua chakula. Kuhisi vibaya anaponusa aina fulani ya chakula.
Mabadiliko ya kisaikolojia katika mwezi wa kwanza wa mimba

Katika mwezi wa kwanza wa mimba, mabadiliko ya kisaikolojia huonekana, hata hivyo, kuna mabadiliko ya kisaikolojia yanayofanyika. Mwanamke huhisi kusombwa na mawazo na kuwa na wasiwasi mwingi katika mwezi wa kwanza wa ujauzito.
Kliniki ya kwanza
Mwanamke hushauriwa kutembelea kituo cha afya punde tu anapogundua kuwa ana mimba. Jambo la kwanza, yeye hufanyiwa kipimo kudhibitisha hali yake ya ujauzito. Kisha historia ya kiafya ya wanafamilia. Ikiwa mwanadada hakuwa amefanya kipimo cha pap smear kwa mwaka mmoja uliopita, anafanyiwa pia. Vipimo zaidi ni kama vile kipimo cha damu, uzito, shinikizo la damu na urefu. Mama hupatiwa vitamini za prenatal katika kliniki yake ya kwanza.
Ukuaji wa fetusi mwezi huu
Mwezi wa kwanza wa mimba huhesabiwa kutoka siku ya kwanza ya kipindi cha hedhi cha mwisho, wiki mbili kabla ya kurutubishwa kwa yai. Katika mwisho wa wiki ya pili, kupevuka kwa yai hufanyika na oocyte kuachiliwa. Inaporutubishwa, inajipandikiza kwenye ukuta wa uterasi. Katika mwezi huu, mwanamke hana uhakika iwapo ana mimba ama la. Kabla ya kukosa kipindi cha hedhi, mama hana uhakika iwapo ishara anazoshuhudia ni za mimba ama la.
Soma Pia: Tendo La Ndoa Katika Ujauzito: Wakati Wa Kuacha Kufanya Mapenzi Katika Mimba