“Mimba ya Rihanna”, mada ambayo imekuwa mdomoni mwa wengi kwa mwezi mmoja uliopita. Rihanna ambaye ni mwimbaji na mwanabiashara mashuhuri mwenye miaka 33, anatarajia kifungua mimba chake pamoja na A$AP Rocky ambaye ni mwimbaji pia.
Alionekana kwa mara ya kwanza huko mji wa New York City huku amevalia koti ndefu ya pinki. Ambayo ilikuwa wazi upande wa chini kuonyesha mimba yake inayozidi kukua, huku akiwa amevalia suruali ya buluu na shanga ndefu zilizofika kwenye tumbo.
Mimba ya Rihanna na mavazi katika mimba
Picha: Kurasa ya Rihanna ya Instagram
Sawa na wanawake wengine wajawazito, Rihanna alikiri kuwa, kuna siku ambapo hahisi kufanya chochote, mbali na kulala kwenye kiti siku nzima. Lakini anapovalia lipstick nyekundu na kuvalia mavazi ya kupendeza, anajihisi kuwa anaweza kufanya chochote.
Rihanna ambaye ni mwanzilishaji na mkurugenzi mkuu wa Fenty Beauty katika mazungumzo yake na Refinery29, alikiri kuwa ajenda yake kuu ni kubadilisha ubaguzi uliopo katika mimba. Alisema, “mwanamke anapopata mimba, jamii mara nyingi humfanya ahisi kana kwamba unaficha, unaficha urembo wako, na kuwa hupendezi vya kutosha lakini utarejelea hapo na siamini hayo. Kwa hivyo najaribu vitu ambavyo singekuwa na ujasiri wa kujaribu kabla ya kupata mimba.”
Picha: Kurasa ya Rihanna ya Instagram
Rihanna angependa wanawake wahisi kuwa wanawakilishwa, na wana ujasiri wanapokuwa wajawazito. Kuwa ni sawa kwa mwanamke mwenye mimba kuvalia mavazi yanayoonyesha urembo wake, bila kuficha tumbo inayozidi kukua kila uchao. Hapo awali, wanawake wajawazito hasa nchini kama Kenya huonekana wakificha tumbo zao. Kwa kuvalia mavazi marefu, mapana na mwishowe kuonekana hawapendezi kwani mavazi hayaendani na miili yao. Kupitia kwa Rihanna, wanawake wanapaswa kukumbatia kipindi cha ujauzito. Kwa kuvalia mavazi yanayofanya wapendeze zaidi, hiki sio kipindi cha kuvalia mavazi makubwa kupindukia, la hasha, zidi kuvalia nguo zinazoonyesha urembo wako.
Picha: Kurasa ya Rihanna ya Instagram
Kama usemi wa kimombo maarufu, ‘unapovalia mavazi ya kupendeza, unahisi vyema’. Safari ya mimba huandamana na mabadiliko mengi ya homoni mwilini. Mara nyingi kumfanya mama kuhisi kulegea. Kwa kuvalia mavazi bora, mama anaweza kujitia motisha kufanya kazi hata asipohisi kufanya chochote.
Bila shaka tunatarajia kuyaona mavazi zaidi ya kusisimua kutoka kwa mwimbaji huyu.
Soma Pia: Rais Wa Tatu Wa Kenya Emilio Mwai Kibaki Afariki