Mimba Ya Siku Tatu: Kuna Uwezekano Wa Kujua Mapema Hivi!

Mimba Ya Siku Tatu: Kuna Uwezekano Wa Kujua Mapema Hivi!

Muda kati ya kupevushwa kwa yai hadi kujipandikiza waweza kuchukua kati ya siku tisa hadi 12. Hivyo Kukosa hedhi ni dalili ya awali ya ujauzito.

Ujauzito kwa wanandoa ama waliokalia kabla ya kujifungua huwa jambo la furaha. Lakini kwa wasiotarajia linaweza kuwa jambo la kutamausha sana. Hili husukuma mtu kujua ni mambo yepi yanayoashiria ujauzito ukiwa mchanga kabisa. Hili husaidia kuondoa wasiwasi na  kutuliza akili awali kabisa. Iwapo njia ya uhakika zaidi ni kupima ujauzito, kuna dalili zingine zinazoashiria mimba ya siku tatu.

Jambo la kuelewa ni kuwa, wanawake huwa na dalili tofauti. Vile mwanamke mmoja ni tofauti na mwingine pia ndivyo dalili za mimba za awali. Pia mwanamke mmoja anaweza kuwa na dalili tofauti kutoka kwa ujauzito mmoja hadi mwingine. Jambo lingine la kutia akilini ni kuwa dalili za awali za mimba zinaoana na zile za kabla ya kupokea hedhi. Kwa hivyo ni rahisi usitambue kuwa una ujauzito.  Hii inamaanisha kuwa njia pekee ya kujua hali yako ni kupimwa ujauzito.

Dalili za mimba ya siku tatu:

mimba ya siku tatu

  • Maumivu ya tumbo la uzazi na kutokwa na matone ya damu kwenye uke

Baada ya yai kupevuka, yai lililorutubishwa hujipandikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi. Hii kwa wanawake wengine husababisha kutokwa na matone ya damu ambayo huwa ishara ya awali ya ujauzito. Pia huku kujipandikiza huwa kuna uchungu hivi kusababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu.  Haya maumivu huwa sawia na maumivu wakati wa hedhi. Hivyo kuna uwezekano mtu kufikiria ni uchungu wa hedhi.

  • Ute mwepesi ulio mweupe

Ni jambo la kawaida kuona ute mweupe ukitoka kwenye uke kipindi chote cha ujauzito. Huu ute hufanana maziwa. Huwa hauna harufu na pia hakuna kuwashwa. Iwapo una ute unaosababisha kuwashwa inaweza kuwa bakteria au fangasi na ni vyema kuona daktari. Baada ya yai kujipandikiza kwenye ukuta wa uterasi, seli za ukuta huweza kuongezeka kwa unene. Hili husababisha ute huu kutoka kwenye uke.

  • Mabadiliko kwenye matiti

Wakati yai linapopevuka huwa kuna ongezeko la kichocheo mwilini. Hili huyafanya matiti kujaa, kuwa na vitu vinavyohisi kuchoma choma. Pia kuhisi uchungu yanaposhikwa.  Sehemu  ya chuchu iliyo nyeusi  huwa nyeusi zaidi.

  • Uchovu

chumvi kupima mimba

Hii ni dalili ya awali sana ya mimba ya siku tatu, kwani huanza pindi mtu anapotungwa mimba. Machovu husababishwa na ongezeko la kichocheo progesterone mwilini. Uchovu wa kupindukia huwa jambo la kawaida kwenye kipindi chote cha ujauzito. Kwa hivyo ni vyema kuratibisha mapumziko ya kutosha na pia kula vyakula vingi vyenye protini na madini ya chuma. Hivi husaidia kuondoa au pia kupunguza machovu.

  • Kichefuchefu

Hii ni dalili iliotambulika sana lakini sio kila mwanamke. Kichefuchefu  hudhaniwa kusababishwa na ongezeko la vichocheo mwilini. Huweza kutokea wakati wowote ule ila kwa mara nyingi hupatikana asubuhi.  Pia kubadilika kwa homoni/ vichocheo mwilini hufanywa wanawake wengine kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine. Hali ya kichefuchefu inaweza kuwa kubwa sana kiasi cha kutafuta matibabu.

  • Kukosa kuona siku za hedhi

Muda kati ya kupevushwa kwa yai hadi kujipandikiza waweza kuchukua kati ya siku tisa hadi 12. Hivyo Kukosa hedhi ni dalili ya awali ya ujauzito. Hii ni dalili iliyozoeleka mno ambayo huelekeza wengi kupimwa ujauzito.

Ongezeko la  vichocheo mwilini ndio chanzo kuu la mabadiliko mengi mwilini. Mengine ni kama vile:

  • Kukojoa mara kwa mara
  • Mabadiliko katika uchangamfu
  • Maumivu ya kichwa na mgongo
  • Kizunguzungu na kuzirai

Chanzo: healthline

Soma Pia:Sababu Za Kipimo Hasi Cha Mimba Bila Kuwa Mjamzito

Written by

Risper Nyakio