Mimba Ya Nje Ya Mirija Ya Uzazi (Tubal): Sababu, Dalili na Matibabu

Mimba Ya Nje Ya Mirija Ya Uzazi (Tubal): Sababu, Dalili na Matibabu

Mimba ya tubal ni jambo ambalo lina wakumba wana jamii. Mimba ina anza kukua nje ya mirija ya uja uzito. Na kuadhirisha maisha ya mama. Na kushuhudia uchungu upande mmoja wa mwili wake.

Kutoka kutunga kwa mimba hadi kujifungua, uja uzito unafuata hatua kadhaa mwilini mwako. Mojawapo ya hizi ni safari ya yai baada ya kutungwa hadi kwa uterasi. Wakati mwingine jambo hili halitendeki. Kwa kisa cha uja uzito wa nje ya mirija ya uzazi, yai lililo tungwa haliji ambatanishi kwa uterasi. Ila, linajigusisha kwa mirija ya uzazi, cavity ya tumbo ama kwenye zalio. Mimba ya nje ya mirija ya uzazi ni mimba ambayo inakua nje ya uterasi kwa mara nyingi, kwa mirija ya uzazi. Ni nadra lakini zina adhari hatari na zinahitajika kutibiwa. Pia zina julikana kama mimba ya tubal.

 

Je, mimba ya tubal (nje ya mirija ya uzazi) ni nini?

Watoto wa kawaida hukua ndani ya uterasi, baada ya yai lilo tungwa kupitia kwa mirija ya uzazi na kujipanda katika ukuta wa uterasi. Ila mimba ya nje ya mirija ya uzazi, yai hujipanda mahali tofauti mwilini na wakati mwingi hukuwa kwa mirija ya uzazi. Kwa hivyo jina, uja uzito wa nje ya mirija ya uzazi. Wakati mwingine, uja uzito unaweza jipanda katika ovari ama sehemu nyengine tumboni mwako.

Kati ya mimba 100 ni 2 peke yake hukuwa za aina hii, kuzifanya nadra sana. Walakini, linaweza sababisha kifo lisipo tibiwa mapema, wakati mirija ya uzazi inapo pasuka, kwani imenyooshwa na mimba inayo kua. Hii inajulikana kama mimba ya nje ya mirija ya uzazi iliyo pasuka. Na inaweza sababisha kutokwa kwa damu kwa undani, maambukizo ama kifo wakati mwingine.

 

Nini dalili za mimba ya nje ya mirija ya uzazi?

ectopic pregnancies

Kwa wakati mwingi, mimba ya aina hii, inakua katika wingi chache za kwanza za uja uzito. Unaweza kosa kufahamu kuwa una mimba na ukakosa dalili zote za kuwa na tatizo lolote. Dalili zake pia ni kama za uja uzito wa kawaida kwa hivyo unaweza fanya kosa la kufikiria kuwa ni uja uzito wa kawaida.

Kutokwa na damu kidogo kutoka uke wako na pia uchungu kwa pelvic ni dalili za kwanza, ila zingine zinaweza kuwa:

 • Kichefu chefu na kutapika kwa uchungu
 • Kufura na matiti mzito
 • Uchungu mkali sehemu ya tumbo
 • Kutoka damu chache kwa uke wako
 • Mhemko wa chini wa damu- pia inasababishwa na kupoteza damu
 • Uchungu kwa sehemu ya chini ya mgongo
 • Uchungu upande mmoja ya mwili wako
 • Kizungu zungu ama kukosa nguvu- unasababishwa na kupoteza damu
 • Uchungu kwa mabega, shingo na mjiko

Nani ako katika hatari ya uja uzito wa nje ya mirija ya uzazi?

Wanawake wote wanao jihusisha na ngono wako kwa hatari ya kupata uja uzito huu. Ila hatari ni zaidi unapo jaribu kupata mtoto katika umri wa miaka 35 na zaidi. Pia unapo vuta sigara: unapo tunga mimba licha ya ligation ya tubal ama IUD; ama kutunga mimba kutumia dawa za uzazi. Uko kwa hatari pia unapokuwa na historia ya zifuatazo:

 • Operesheni ya pelvic, operesheni ya tumbo ama kutoa mimba mara nyingi
 • Magonjwa ya uchochezi wa pelvic (PID)
 • Endometriosis 
 • Mimba ya nje ya mirija ya uja uzito
 • Magonjwa ya ngono kama vile kisonono ama chlamydia
 • sexually transmitted diseases (STDs), such as gonorrhea or chlamydia

Je, mimba ya nje ya mirija ya uzazi inagunduliwa vipi?

Daktari wako atagundua mimba ya nje ya mirija ya uzazi kwa kwanza kufanya mtihani wa kipelviki kudhibitisha kama kuna uchungu, unyororo ama kitu kinachokua sehemu yako ya tumbo. Pia ataangalia uterasi yako aone mtoto anavyoendelea kutumia ultrasound. Baada ya hapo atapima viwango vya homoni ya HCG. Kipimo hiki ni muhimu sana. Kiwango cha HCG chini ya idadi inayo hitajika ni mojawapo ya sababu ya kushuku mimba ya nje ya mirija ya uzazi. Daktari wako pia anaweza kupima viwango vya homoni ya progesterone mwilini kwani viwango vya chini vya homoni hii ni dalili ya uja uzito ulio nje ya mirija ya uzazi.

La mwisho, daktari wako anaweza kufanya culdocentesis, utaratibu huu unahusisha kuingiza sindano katika nafasi iliyoko katika sehemu juu ya uke wako nyuma ya uterasi na mbele ya mjiko. Kuwepo kwa damu katika sehemu hii ni dhibitisho kuwa una tokwa na damu inayotokana na kupasuka kwa mirija ya uzazi.

 

Jinsi ambavyo mimba ya nje ya mirija ya uzazi inavyo tibiwa

Uja uzito wa namna hii unatibiwa kupitia njia hizi:

 • Unaweza pewa dawa inayo julikana kama methotrexate. Inausaidia mwili wako kunyonya tishu hiyo ya uja uzito na kuokoa mirija ya uzazi,kulingana na umbali ambao uja uzito wako umefika. 
 • Iwapo tubu imenyoshwa ama imepasuka na inatoka damu, sehemu ama tubu yote ita tolewa. Kutokwa kwa damu kuna hitaji kusimamishwa haraka na operesheni ya dharura kufanyika.
 • Operesheni ya kilaparoskopiki chini ya nusukaputi utafanyika. Utaratibu huu una mhusu daktari wa upasuaji chini ya laparoskopi ili kutoa mimba ya nje ya mirija ya uzazi na kutengeneza ama kutoa mirija ya uzazi.

Utunzaji wa nyumbani

Utapata maelezo maalum ya utunzaji wa kidonda chako cha operesheni kuhusu unachofaa kufanya. Lengo lako kuu ni kukiweka kidonda kile kikiwa kisafi wakati wote na pia bila maji hadi kitakapo pona. Kiangalie kila siku kuhakikisha hakina maambukizo yoyote ama dalili zikiwemo:

 • Kutokwa na damu kwa wingi isiyo acha
 • Kutoa harufu mbaya kutoka kwa kidonda
 • Moto kugusa
 • Uwekundu
 • Kufura 

Tarajia kuwa na kutokwa kwa damu kidogo kutoka kwa uke wako na damu kidogo inayotambaa hadi unapo fikisha wiki sita baada ya operesheni.

Baada ya hapo lazima uchukue juhudi za kujitunza. Usiviinue vitu mzito, kunywa maji mingi, epuka kujihusisha na kufanya ngono na kuto tumia tamponi na kujimwagilia 

 

La mwisho, pata mapumziko unapoweza kwa wingi, wiki ya kwanza baada ya operesheni na kwa upole anza kuongeza mambo unayo yafanya kwa wiki zinazo fuata.

Wasaa wote, mjulishe daktari wako, uchungu wako unapo ongezeka ama unapo hisi kuwa kuna jambo lisilo la kawaida.

Maisha baada ya mimba ya tubal (nje ya mirija ya uzazi)

 • Kupoteza kwa mimba, haijalishi ni mapema aje, ni uchungu. Utahitaji mfumo wa msaada ulio na nguvu. Usiogope kuwa uliza marafiki na jamaa wako kwa msaada. Kama kuna vikundi vya msaada katika hospitali yako, kanisa ama msikiti, fanya utafiti na ujiunge nao. Kama kuna ushauri unao hitaji, kwa njia zozote zile, enda ushauriwe. Jitunze kupitia kupata mapumziko ya kutosha, lishe bora, kufanya mazoezi inapo wezekana. Pia jipe wakati wa tanzia.

 • Usisahau kuwa kuna wanawake wengi wanao beba mimba mpaka inakomaa na kupata watoto baada ya mimba ya nje ya mirija ya uzazi. Unapo kuwa tayari, ongea na daktari wako kuhusu njia unazoweza kutumia kuhakikisha mimba yako ya usoni itakuwa na afya.

 

Read Also: Is It Possible to Get Pregnant While You’re Breastfeeding?

Written by

Risper Nyakio