Kujaliwa mtoto huwa jambo la furaha isio na kifani. Ila pia huwa ni safari iliyo na panda shuka nyingi. Dalili kuu ya mimba ya wiki 36 ni machovu nyingi. Machovu yamekuzidi unachofikiria tu ni siku ya kujifungua itawasili lini.
Mambo Ya Kutarajia Katika Mimba Ya Wiki 36

Pamoja na kuwa mtoto wako amekomaa na yuko tayari kuwasili duniani, mwili wako pia unajiandaa kujifungua. Mambo ya kutarajia:
- Maumivu kwenye mgongo. Hii ni kwa sababu ya ile kazi ambayo umefanya ya kubeba mtoto kwa miezi nane. Uzito mwingi uko kwenye tumbo hivyo kuna kazi nyingi kuzuia kuanguka nyuma
- Mkazo kwenye nyonga. Kichwa cha mtoto kinaelekea chini na mtoto anazidi kuwa mkubwa
- Usingizi uliokatizwa. Hili hutokea wakati mtoto anapiga teke kwa nguvu
- Hili kwa kuwa umekuwa unabeba kiumbe kwa miezi tisa
- Vimbizi. Hutokana na kuwa mtoto anakua na kuzuia utaratibu wa chakula kusagika
- Kujisaidia kwa kila dakika. Hii ni kwa sababu ya homoni wakati wa ujauzito. Pia mtoto amekalia kibofu chako
- Kubadilika kwa hamu ya chakula. Ila hili huwa tofauti kwa kila mtu. Unaweza kuhisi njaa ama kupunguka kwa hamu ya chakula. Hii ni kwa kuwa kuna nafasi kubwa iliyochukuliwa na mtoto
Kukua Kwa Mtoto Katika Wiki Ya 36

Katika wiki za mwisho za ujauzito, kukua kwa mtoto wako kunaongezeka. Hii inamaanisha kuwa wewe pia unakua. Kutoka mwezi uliopita mtoto wako ameweza kuongeza kilo 1 au 2 na pia inchi 1 hadi 2.5. Mbali na haya mtoto wako anapiga hatua kubwa katika kukua kwenye kipindi hiki.
Kwa mfano mapafu yao yanajengeke kuweza kupumua nje ya tumbo la uzazi. Pia misuli yao inatimilika ili waweze kupepesa macho na kugeuza kichwa chao.
Mwendo Wa Mtoto Katika Wiki Ya 36
Unapokaribia mwisho wa ujauzito, mtoto ataweza kusongea chini ya tumbo. Pia mwelekeo wa mtoto wako unafaa kubadilika ili kichwa kiangalie chini kujitayarisha kwa kuzaliwa. Watoto wengi hugeuka na kukaa hivi katika wiki ya 36.
Iwapo mtoto wako hajakaa hivi, daktari wako atakuelezea njia mtakazotumia. Wanaweza kushauri njia za kubadilisha vile mtoto amekaa ama C-section. Kuna uwezekano uhisi mtoto wako hasongi sana katika huu wakati kwa sababu nafasi yake imepunguka.
Kazi Wakati Wa Ujauzito Ya Wiki 36
Vile tarehe yako ya kujifungua inakaribia, unaweza gundua kuwa hauna hamu ya kufanya kazi. Wengine hawatahisi haja ya kupunguza mambo au kupumzika. Lakini ni vyema kuusikiza mwili wako na kupata mapumziko unapohisi machovu.
Pia unaweza kudumisha mazoezi yako ya kawaida. Hakuna haja ya kupunguza ama kusitisha ila iwapo daktari ameelekeza hivyo. Lakini si vyema kuanza aina mpya ya mazoezi. Kama bado unajihisi unaweza endelea na kufanya mapenzi ni sawa. Ila kama daktari hajaeleza wasiwasi wowote.
Ata kufanya mapenzi kunaweza kuharakisha uchungu wa mimba. Kama una hatari ya uchungu wa mapema, daktari anaweza kushauri kuweka mapenzi kando kwa huu wakati. Pia iwapo maji yako yatavunja utashauriwa kuacha kufanya mapenzi kukinga dhidi ya maambukizi.
Kwa kweli ujauzito ni safari ya furaha ila kuna mengi utakayoweza kupitia. Ila usitie shaka kwa hauko peke yako. Pia familia na daktari wako watakuwa nawe hadi mimba ya wiki 36 ili kujihisi salama.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Ya Kushika Mimba Kwa Urahisi Katika Miaka Ya 30’s