Wakati wa kufanya mapenzi manii ya mwanamume hutoka ikiwa na mbegu nyingi ila ni moja tu hufanikiwa kufika kwenye yai la mwanamke na kusababisha ujauzito. Baada ya kupenya, yai hujifunga na kukamilisha tendo la uchavushaji na hapa mama anakuwa ametungwa mimba. Hii mimba huzidi kukua wiki baada ya nyingine. Jinsi ya kufahamu mimba yangu ina wiki ngapi.
Hatua za Ujauzito Wiki Hadi Wiki

Siku za kwanza baada ya kutungwa mimba , yai lililochavushwa hujigawa kwenye chembe nyingi hai. Hii hupitia kwenye mirija ya fallopian na kupanda hadi kwenye mfuko wa uzazi ama uterasi na kujibadika hapo. Wakati huu plasenta huwa inatengenezwa.
Mtoto anaanza kutengeneza muonekano wa sura pamoja na shingo. Moyo na misuli ya damu huanza kujengeka. Kwa hii wiki, unaweza kutumia vipimo vya nyumbani na kupata matokeo halisi.
Kwa hii wiki mtoto huwa na ukubwa wa nusu inchi(1.27cm). Ngozi inayofunika macho na masikio huanza kutengenezeka. Pia alama ya pua huanza kutokea kwa umbali. Mikono na miguu huwa kwisha imetengenezwa kwa huu wakati. vidole navyo huanza kukua na kuonekana vyema.
Kwa hivi sasa kijusa anakaribia sentimita tano. Unaanza kuhisi ukubwa wake juu ya mji wa uzazi. Hivi sasa daktari anaweza kusikia mapigo ya moyo kwa kutumia kifaa maalum. Huu wakati pia sehemu za siri za mtoto huwa zimejengeka vyema.

Ukubwa wa mtoto kwa hii wiki huwa kati sentimeta 11na 12 na uzito wa gram 100. Kwa hii wiki mtoto ana uwezo wa kuchezesha macho . Moyo na mishipa ya damu huwa imekwisha kamilika. Vidole kwa hivi sasa huwa vimekwisha tengenezeka michirizi (fingerprints).
Uzito wa mtoto kwa hivi sasa ni gram 285. Pia ana uwezo wa kunyonya vidole, kujinyoosha na pia kuchezacheza. Kwa wakati mwingine, ultrasound hufanyika hii wiki. Daktari ukakikisha kuwa plasenta iko salama na ina afya njema. Na pia uhakikisha kuwa mtoto ana kua vizuri. Pia kupitia ultrasound utaweza kuona mipigo ya moyo ya mtoto na pia kuona viungo kama vile mikono ,miguu na pia muenendo wa mwili wake. Pia unaweza kutambua jinsia ya mtoto.
Mtoto ana uwezo wa kufuata sauti. Unaweza kumsikia akizunguka kufuata sauti inapotokea. Jenga tabia za kuongea naye kuanzia sasa, maana watoto hujenga mazoea na sauti wanazozisikia na huzitambua pindi wanapozaliwa. Katika hii wiki, mfumo wa masikio unakuwa umekamilika. Pia ana uwezo wa kuhisi uelekeo wake ndani ya plasenta.
Huweza kubadilisha sana uelekeo akiwa kwenye wiki hii. Kwa wale waliojifungua watoto kabla ya wakati, waliozaliwa kwa hii wiki huwa na nafasi bora ya kuishi.
Katika hii wiki utamskia mtoto akizunguka sana. Hii wiki pia ngozi ya mtoto huonekana kama imejikunja kunja kwa sababu tabaka la fati huanza kutengenezwa.
Ubongo sasa unajengeka kwa haraka zaidi. Mapafu nayo yanaelekea kukamilika na mtoto anageuka na kichwa kinaelekea chini kwenye njia(pelvis).
Hatua za mimba kwa kila wiki huwa kama kipimo katika kukua kwa mtoto. Ni ishara tosha kuwa mimba inaendelea inavyohitajika. Unaweza kujua mimba yangu ina wiki ngapi kwa kufuata vidokezo vya makala haya.
Chanzo: healthline
Soma Pia:Kutoa Mimba Kinyumbani Kuna Hatari Nyingi Kwa Mama, Tazama!