Bila shaka mitandao ya kijamii ina athari kubwa kwa watoto. Ina athiri nyanja tofauti za maisha yao na jinsi wanavyofanya mambo tofauti. Wanavyo valia, wanavyo husiana na watu wengine na wanavyo jitazama. Utafiti uliofanyika kuhusu uhusiano wa mitandao ya kijamii na ukuaji wa watoto umedhihirisha ukweli ambao hatukuwa tayari kuukubali. Kulingana na utafiti, mitandao ya kijamii ina athiri wasichana zaidi ikilinganishwa na vijana. Mitandao ya kijamii na ukuaji wa watoto huambatana
Mitandao Ya Kijamii Ina Athiri Wasichana Zaidi Ikilinganishwa Na Vijana

- Utumiaji wa mitandao kati ya jinsia mbili
Wasichana walipatikana kutumia mitandao ya kijamii zaidi ikilinganishwa na vijana na kuathiri furaha yao na ustawi wao. Katika umri wa miaka 10, asilimia 10 ya wasichana walitumia mitandao ya kijamii kwa lisaa limoja kwa siku. Ikilinganishwa na asilimia 7 ya vijana wa umri huo waliotumia mitandao kwa wakati sawa. Katika umri wa miaka 15, asilimia 43 ya wasichana walitumia mtandao kwa lisaa limoja kwa siku, huku asilimia 31 ya vijana wakitumia mtandao kwa wakati tosha.
Furaha na ustawi kati ya jinsia hizi
Utafiti ulivumbua haya:
Katika umri wa miaka 10, watoto wa kike waliripotiwa kuwa na viwango duni vya furaha ambavyo viliongezeka walivyozidi kuzeeka. Kwa upande wa watoto wa kiume, viwango vya furaha na ustawi havikuwa chini hivyo.
Katika ripoti hii, watafiti waliripoti kuwa, viwango vya juu vya utumiaji wa mitandao ya kijamii katika umri mchanga uliathiri ustawi katika maisha ya baadaye japo watoto hawa walivyozidi kuzeeka. Hasa katika watoto wa kike. Watoto wa kike wanatumia mitandao zaidi na kuwaweka katika hatari ya kujilinganisha na wasichana wengine kwenye mitandao. Wavulana kwa upande mwingine hawakuonekana kutumia mitandao kwa sana. Ni vyema kukumbuka kuwa utumiaji wa mitandao ya kijamii ni kawaida na ni vigumu kuepuka watoto wanapofika umri fulani, lakini kupata uraibu wa kuitumia kuna athari hasi kwao. Swali kuu ni: Je, utadhibiti kivipi utumiaji kwa watoto wako?
Jinsi ya kudhibiti utumiaji wa mitandao ya kijamii kwa watoto

Unapogundua kuwa watoto wako wako kwa simu zao wakati wote, nafasi kubwa ni kuwa wanatumia mitandao ya kijamii. Kwa hivyo, hivi ndivyo unavyoweza kuwasaidia.
Himiza mawasiliano wa kijamii. Unapodhibiti utumiaji wa mitandao ya kijamii, lazima uwape njia mbadala. Wahimize kuzungumza na watu, uso kwa uso na kutengeneza marafiki zaidi.
Kuwa mfano wa kuigwa. Huwezi mlazimisha mtoto wako kutofanya kitu unachopenda kufanya mwenyewe. Kwa hivyo punguza utumiaji wako wa simu hasa katika wakati wa familia.
Patia familia kipau mbele. Tengeneza mazingira nyumbani mwako yanayo kubalisha kuwa na wakati zaidi na familia yako. Hata kama ni kusoma kitabu ama kutizama vipindi vya watoto kwa pamoja. Iweke kwenye ratiba yenu.
Chanzo: Forbes
Soma Pia: Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?