Mitindo 5 Ya Ankara Ya Kuwafurahisha Nyanya

Mitindo 5 Ya Ankara Ya Kuwafurahisha Nyanya

Mitindo ya Ankara ya nyanya anayependa nguo za kupendeza.

Unapofikiria mavazi ya ankara, fikira rangi zenye joto, mitindo ya kipekee na kitambulisho. Kitambulisho cha mtindo wa ki Afrika. Ongea kuhusu staili za ankara na utaona aibu kufuatia utajiri wake. Mitindo ya ankara ya nyanya, wamama, wababa, na watoto kwa wingi.

Kwa kweli, Afrika inajulikana kwa mavazi ya ankara. Hata kama hayakutoka Afrika, ila Indonesia. Ilikuwa watumwa wa Afrika Magharibi na wapiganaji walio jiunga na jeshi la Indonesia walio ona nguo hizi na kuzileta nyumbani walipokuwa wakirudi.

Nigeria, Ghana, na Senegal zilikuwa nchi zilizo leta ankara kwenye laini ya kwanza na kujulikana. Wakati ambapo mavazi ya Indonesia ilipo kosa kufurahisha huko Indonesia na sehemu za Uropa, waliitazamia Afrika, ambapo mavazi bora zaidi ya ankara yalikuwa yameanza kutolewa na kuvaliwa.

Miaka ilivyo zidi kusonga, mtindo wa ankara uliendelea kubadilika. Mafundi na wasanii wachoraji walibuni mitindo ya kusisimua zaidi iliyo kuwa sawa kuvaliwa kwa sherehe yoyote. Uliona mitindo hii popote ulipo enda. Mitindo mingi ambayo ingemgeuza chura kuwa mfalme ama malkia. Na kwa hivyo kuwafurahisha watu wa jinsi zote na umri.

Mitindo ya ankara ya nyanya

Ina hitaji kiwango cha umakini cha kuchagua mtindo rahisi na wa kiwango cha juu wa wanawake wa umri zaidi. Mbadala ya wale wachanga, wanawake wenye umri zaidi huenda wakawa makini na starehe ya mtindo. Hapa chini kuna mitindo ya ankara ya nyanya. 

  • Ankara kaftan

Ankara Kaftan Ankara styles for grandmothers

Ankara kaftans kwa ujumla zina toshea na hazi bani mwili. Zina weza valiwa na jinsia zote mbili. Pia, ni nzuri kwa sherehe yoyote. Kihistoria, sultans wa Afrika Kaskazini walipata jina kwa kuzivalia. Ila, mtindo huu ulikumbatiwa kwa dunia ya mitindo ya Afrika, na kubadilika ili yamtoshee kila mmoja hata nyanya zetu. Kwa nini linawatosha nyanya na kuwa la kiwango cha juu, kwa sababu lina kubalisha uhuru wa mwendo. Sehemu za mwili zinaweza songa kwa urahisi.

Pia, na upana wa mtindo huu, nyanya wanaweza chagua. Ankara kaftan inaweza shonwa kwa njia tatu: ndefu, fupi na wastani. Iwapo nyanya hataki kuonyesha miguu ama mikono, anaweza chagua kaftan mrefu na mikono mirefu. Na pia anaweza mwuliza fundi wake kufanya mabadiliko yoyote anayo yataka.

  • Rinda la ankara la peplum 

Ankara styles for grandmothersGrandma would love this for its freedom, simplicity, and versatility. Ankara peplum gown is trending among mature women. If you are not acquainted with Ankara peplum gown as a fashionable mature woman, perhaps it's time to ring your designer. What makes it a peplum gown is that extra material is added around the waist area as the highlight of the style.

Nyanya angependa mtindo huu kwa uhuru wake, urahisi na uwingi wake. Vazi hili la rida la ankara ndilo lina shonwa na kuvaliwa sana na wanawake walio komaa. Iwapo haujui mtindo huu wa peplum ya ankara kama vazi la wanawake walio komaa, ni wakati umpigie simu fundi wako. Kinacho fanya nguo hii iwe rinda la peplum ni kitambaa zaidi kinacho ongezwa kwenye kiuno kusisitiza mtindo huu.

Rinda hili linaweza badilishwa kwa njia nyingi. Na mabega wazi, mikono mirefu, mikono mifupi. Pia, msanii mchoraji wa nyanya anaweza tengeneza rinda refu ama lifupi.

  • Sketi na blausi ya Ankara 

skirt and blouse ankara

Huenda ukawa ulikuwa unataraji hii kwa orodha hii. Mitindo mingi ya ankara na wasanii wachoraji wamekuja na kutokomea, ila sketi ya ankara na blausi zime simama wima ama vile nyumba juu ya jiwe. Mtindo huu umeonekana kuwa mkuu na kuigwa na wengi hasa wanao zipenda nguo za mtindo wa ankara. Kwa kiwango cha kuwatembelea wasanii wachoraji wao, hadi pale wanapo badili mawazo yao. Hiki ndicho kiwango wanacho penda sketi na blausi za ankara.

Cha zaidi, mtindo huu huwapatia nyanya mengi sana kwa pamoja. Unaweza geuzwa na kutengenezwa kwa njia tofauti hadi utosheleza ladha ya mtindo wa nyanya. Pia, iwapo alichagua kumalizia mtindo huu na kitambaa cha kichwa kikubwa ama kidogo, hakuna tofauti. Nguo hizi zitamkalia vizuri.

  • Blausi na mshipi wa ankara

Ankara styles for grandmothers

Iwapo ushai sikia mzaha wa ki Nigeria kuhusu wa mama wa Igbo wanao fanya familia ichelewe kwenye kanisani Ijumaa kwa sababu wamekuwa wakijaribu kufunga vitambaa vyao, blausi za ankara na mshipi. Machoni mwa wana Nigeria, mtindo huu unachukuliwa kuwa ishara ya kukomaa kwa sababu imekuja kuhusishwa na wamama wa mashariki mwa Nigeria kama nyanya. Na mtindo huu, nyanya anapo nyoosha miguu anafunga mshipi chini ya blausi yake. Baada ya hapo anaendelea kufunga mwingine juu ya blausi.

  • Mtindo wa Ankara boubou 

bou bou style

Mtindo huu unajulikana kama Bubu wa baadhi ya wana Afrika. Mtindo huu unatoa jina lake na historia kutoka Senegali. Nyanya anaweza uvaa kwa njia ya adi. Mshipi unafungwa kwenye kiuno, na rinda linalo anguka na kisha kitambaa cha kichwa. Ila, mtindo huu umebadilika siku hizi na unaweza valiwa bila mshipi. Nyanya anaweza mwuliza msanii mchoraji amtengenezee ankara boubou kwa njia ambayo inaukumbatia mwili kwa njia ya heshima ama kutoifanya iwe pana sana. Zote zitamkalia vyema.

Hitimisho

Kama ilivyo na vitu vingi maishani, unaweza fanya majaribio na mitindo ya kuvalia. Nguo za ankara ni nyingi na miundo yake tofauti inazifanya ziwe za kuvutia na kuvaliwa mahali popote. Kwa hivyo kuwa huru kumwacha msanii mchoraji wako kujaribu kitu mpya.

Soma pia: Ghanaian Maternity Dresses: Defining Your Style In Pregnancy

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio