Ni Mtindo Upi Wa Kulala Bora Kwa Mama Mjamzito?

Ni Mtindo Upi Wa Kulala Bora Kwa Mama Mjamzito?

Kulala na kupata usingizi tosha ni muhimu sana kwa mama mjamzito. Mbali na hayo, anapaswa kuhakikisha kuwa analala kwa njia inayo faa.

Kuna jambo moja  ambalo unapaswa kukubali unapo tarajia mtoto. Kuelewa kuwa kuenda kulala- na kubaki kwa mtindo huo - sio jambo rahisi! Wanawake wamezoea kulala kwa njia ama mtindo wowote ule ambao unawapa starehe na ambao wame zoea. Lakini jambo hili hubadilika katika ujauzito. Tumbo inayo endelea kukua kila siku itafanya iwe vigumu sana kubaki kwa mtindo wa kulala unao starehesha. Na kufanya kulala kuwe na tatizo. Baadhi ya mitindo ya kulala huenda ikawa sio salama kwa wanawake wenye mimba baada ya mwezi wa tano wa ujauzito. Kwa hivyo ni mitindo ipi ya kulala bora ukiwa mjamzito? Soma zaidi.

Hii si mitindo bora ya kulala ukiwa mjamzito

Baada ya mwezi wako wa tano, kulala kwa mgongo sio vyema. Kulala hivi kuna weka shinikizo zaidi kwenye mishipa ya aorta na inferior vena cava. Hii ni mishipa ya damu inayokuwa nyuma ya uterasi na kupeleka damu kwenye moyo kutoka kwa miguu yako. Shinikizo kwenye mishipa hii kunaweza punguza mzunguko wa damu mwilini na kwa mtoto wako.

Huenda ukapata tatizo kupumua ukiwa umelala kwa mgongo. Kwa sababu tumbo yako inasukuma matumbo yako unapo lala kwa mgongo, na huenda ukapata matatizo ya tumbo.

Na je, kulala kwa tumbo? Sio wazo nzuri pia. Unapolala uso ukitazama chini, unalalia tumbo yako inayo endelea kukua, na chuchu zilizo fura.

Mitindo bora ya kulala ukiwa mjamzito: Kushoto ni bora

mitindo ya kulala ukiwa mjamzito

Kwa sasa hivi, kulala kwa pande ni salama zaidi kwa mtoto wako. Pia, unapata starehe zaidi na haukazi tumbo yako. Je, upande mmoja wa tumbo ni bora kuliko mwingine? Wataalum wana shauri kulala kwa upande wako wa kushoto. Kuna imarisha mzunguko wa damu na pia ina virutubisho tosha kutoka kwa roho hadi kwa placenta kulisha mtoto. Kulala kwa pande ya kushoto kuna saidia mwili wako unao endelea kunenepa kuto sukuma kwa nguvu sana maini yako. Wakati ambapo pande zote mbili ni nzuri, kushoto ni bora zaidi.

Vidokezo vya kulala

Hapa kuna vidokezo vichache vya kulala vya kukusaidia kuwa na starehe zaidi na kumlinda mtoto wako unapo lala ukiwa na mimba.

Ni Mtindo Upi Wa Kulala Bora Kwa Mama Mjamzito?

  • Ili kulala kwa starehe na kuegemeza tumbo na mgongo: Weka mto chini ya tumbo na katikati ya miguu yako. Nunua mto specheli mrefu ama utumie wa kawaida ulio nao. Kuweka mto chini ya mwili wako kutakusaidia kubaki kwa njia hiyo na kuepusha kugeuka na kulala kwa mgongo ama tumbo
  • Kwa kupungukiwa na hewa: Weka mto chini ya upande wako ili kuinua kifua chako
  • Kwa kiungulia: Inua kichwa cha kitanda inchi chache kwa kutumia vitabu ama vitu vingine. Kufanya hivi kunakusaidia kuweka asidi tumboni mwako chini, badala ya kuchoma hadi ifike kwenye aesophagus.

Usiwe na shaka ukipinduka kutoka upande mmoja hadi mwingine ukiwa umelala. Ni vyema kuuwacha mwili wako usonge unako kuwa na starehe kuliko kujaribu kujiamsha kila dakika chache kuhakikisha umelala kwa upande. Unahitaji usingizi mwingi uwezavyo wakati huu. Uta thamini kulala zaidi mtoto wako anapo anza kukuamsha kati kati ya usiku kunyonya.

Chanzo: WebMD

Soma Pia:Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Miaka Zaidi Ya 35

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio