Tazama Mitindo Hii Ya Mistari Ya Watoto Itakayo Mfaa Mwanao Zaidi

Tazama Mitindo Hii Ya Mistari Ya Watoto Itakayo Mfaa Mwanao Zaidi

Mitindo ya mistari ya watoto huwapa watoto mtindo rahisi, safi na unao weza kusongwa kwa njia tofauti. Mtindo huu ni rahisi kwa sababu ni rahisi kusonga na kuwacha nafasi kati kati ya kichwa, ambayo ni muhimu kuifanya ngozi ya watoto iwe safi wakati wote. Unaweza mpaka mwanao mafuta mara kwa mara kuhakikisha kuwa hapati uchafu kichwani. Mtindo huu ni bora mtoto anapo enda shuleni, kanisani ama hata sherehe. Makala haya yana lengo la kukuelimisha kuhusu mbinu tofauti za kusonga mtoto wako mtindo huu wa mistari.

Mitindo ya mistari ya watoto

Hapa chini kuna baadhi ya mitindo ya mistari ya watoto itakayo mfaa mwanao zaidi.

  1. Mistari yenye kitita
cornrow styles for toddlers

Picha shukrani kwa: Child Insider

Mtindo huu wa mistari utamfaa sana mtoto wako mdogo. Kwa kuanza, gawanya nywele mara mbili hapo katikati, na kuwa na pande mbili. Upande mmoja unaanza na mistari na kuja katikati ya kichwa. Upande huo mwingine unasongwa ukielekea nyuma. Iwapo mtoto wako ana nywele nyingi kichwani, na zinakutatiza kusonga, mtindo huu utamfaa zaidi. Ama iwapo nywele zake hazina upande maalum zinao anguka.

2. Mistari yenye pony ya upande na beads kwenye ncha zake

cornrow styles for toddlers

Picha shukrani kwa: Child Insider

Mtindo huu sio mgumu kama jina lake linavyo ashiria. Songa mistari hii ikienda upande mmoja, wa kushoto ama wa kulia. Mtindo huu unashauriwa iwapo ungependa kichwa cha mtoto wako kiwe kisafi na awe na starehe. Nywele hizi hazigusi uso wa mtoto wako, anaweza songesha kichwa chake bila ya kuwa na nywele usoni. Rembesha ponytail hii kwa kutumia beads za rangi tofauti ili mistari hii ipate rangi zaidi.

3. Mistari ya vipepeo

cornrow styles for toddlers

Picha shukrani kwa: Child Insider

Iwapo wewe ndiye ungependa kumsonga nywele hizi, ni vyema kutafuta msusi aliye na uraibu wa kufanya hivi. Ama iwapo una imani kuwa unaweza fanya hivi, una uhuru wa kumsonga. Mtindo huu wa mistari una ugumu, ila iwapo unaweza songa ipasavyo, mtoto wako wa kike atapendeza sana. Ni kama sanaa, ila wakati huu, mistari hii inafanana kipepeo juu ya sikio lake na nywele zingine kusongwa pamoja kwa mstari mmoja juu ya kichwa chake.

4. Mistari nusu

Tazama Mitindo Hii Ya Mistari Ya Watoto Itakayo Mfaa Mwanao Zaidi

Picha shukrani kwa: Child Insider

Mistari nusu ama half cornrows haihitaji kichwa kizima. Mtindo huu unafaa zaidi hasa iwapo ungependa mtoto wako arembeke bila kuwa na nywele zinazo gusa uso wa mtoto wako. Mtindo huu unakukubalisha kugawanya nywele mara mbili. Songa upande wa kwanza mistari kisha upande wa nyuma, zianguke kwenda nyuma ya kichwa.

5. Cornrows ama mistari ya rangi na box braids

mitindo ya mistari ya watoto

Picha shukrani kwa: Child Insider

Mtindo huu ni maarufu katika sehemu nyingi kwa sababu ni rahisi na pia unafanya watoto wapendeze. Mistari hii ina rudi nyuma na haipiti kumi na miwili, na ncha za mistari hi kuanguka kwenye mabega ya mtoto. Kinacho zifanya zipendeze ni rangi tofauti unazo amua kutumia. Watoto wachanga hupenda rangi tofauti. Kwa kuongeza rangi, tumia chokaa ama spray. Usitumie dye kwa nywele ya mtoto wako kwa sasa bado inakua na huenda kemikali hizi kali zikafanya nywele zikatike.

Epuka kufanya mistari hii imbane mtoto sana. Ina sababisha kuumwa na kichwa kwa mtoto wako. Pia, mistari mikonde huchukua wakati mrefu kusonga, huenda pia ikasababisha nywele kukatika. Kwa hivyo ni vyema kumsonga mtoto wako mistari minene.

Soma pia: Mitindo Ya Nywele Ya Afro Ya Watoto Wasichana

Chanzo: Child Insider

Written by

Risper Nyakio