Punguza Uzito Wa Mwili Kwa Kufanya Mitindo Hii Ya Ngono

Punguza Uzito Wa Mwili Kwa Kufanya Mitindo Hii Ya Ngono

Mitindo bora zaidi ya kukusaidia kupunguza uzito wa mwili kwako na mchumba wako.

Njia iliyo maarufu zaidi ya kupunguza uzito wa mwili ni kufanya mazoezi na kupunguza kiwango cha chakula unacho kila. Ila watu hawajui kuwa, kupunguza uzito wa mwili hakupaswi kuwa kama adhabu na unaweza punguza uzito wa mwili kwa matendo ya kufurahisha na mchumba wako kwa kufanya mapenzi. Ni vyema kutia akilini kuwa hatusemi ukome kwenda kufanya mazoezi yako ya kawaida, la endelea kufanya mazoezi yako kama kawaida na mzidi kuwa na wakati mwema kitandani na utagundua kuwa uzito wako utapunguka. Utafiti umedhibitisha kuwa baadhi ya mitindo ya ngono inaweza kusaidia katika kupunguza ufuta kwenye tumbo na sehemu zingine za mwili. Tuna kuelimisha kuhusu mitindo ya ngono ya kupunguza uzito wa mwili.

 

Mitindo Tofauti Ya Ngono Ya Kupunguza Uzito Wa Mwili

 1. Mtindo wa makasi (scissors)
 2. Missionary
 3. Mtindo wa doggy
 4. Lotus
 5. Mtindo wa cowgirl
 6. Bridge
 7. Mtindo wa wheelbarrow
 8. Arch
 9. Mtindo wa kusimama
 10. Squatting cowgirl

Makala haya haya fuati utaratibu wowote katika orodha hii, ila hii ni mitindo ambayo mnaweza angazia na mchumba wako mnapo fanya mapenzi.

 1. Mtindo wa makasi

Mtindo huu una ugumu kiasi na si rahisi ukilinganisha na mitindo ingine na hii ndiyo ambayo inakufanya kupoteza uzito wa mwili. Mtindo huu una angazia sehemu ya juu ya mwili na mapaja na utahisi kana kwamba unafanya mazoezi. Unapaswa kuwa na stamina na nguvu za mikono ili kuusitiri mwili wako kwani unakaza sehemu ya mikono zaidi. Mtindo huu una imarisha sehemu ya juu ya mwili wako.

2. Mtindo wa missionary

mitindo ya ngono ya kupunguza uzito

Mtindo huu ni maarufu zaidi hasa mwanamme anapokuwa juu na kufanya kazi zaidi ya mchumba wake wa kike. Una saidia katika mzunguko wa damu. Mtindo huu una imarisha misuli yako. Ili nyote kunufaika na faida za kufanya mapenzi, hakikisha kuwa kila mmoja anachukua awamu yake kuwa upande wa juu.

3. Mtindo wa doggy

Baadhi ya utafiti unadhihirisha kuwa mtindo huu ni maarufu sana na wanaume wanaupendelea zaidi. Inasemekana kuwa unasisimua sana na ni bora kwa wanao taka kupunguza kilo chache. Katika mtindo huu, mwanamke huchuchumaa na mwanamme kuwa nyuma yake.

4. Lotus

sex positions for men with small penis

Huenda mtindo huu uka onekana kana kwamba ni rahisi ili si rahisi. Mwanamke anakalia mapaja ya mwanamme aliye kaa kitako kwenye kitanda ama kiti. Sio vigumu kukaa kwa njia hii ila kuna bidii inayo hitajika. Inasaidia sehemu za mapaja na tumbo ya mwanamke na miguu kuwa na nguvu zaidi.

5. Mtindo wa cowgirl

Ni rahisi kuingia kwa mtindo huu baada ya kumaliza mtindo wa doggy. Kwa mtindo huu, mwanamke hu chuchumaa juu ya mwanamme na anaweza angalia upande wa mbele ama nyuma. Mwanamke ana ongoza na kuna misuli mingi inayo husishwa.

6. Bridge

Hii ni mojawapo ya njia bora zaidi za kufanyisha kazi misuli mingi mwilini mnapo fanya mapenzi na mchumba wako. Mwanamke ata jisitiri kwa kutumia mikono na miguu yake huku akiinua mapaja yake hewani kutengeneza daraja ama bridge. Mchumba wako anakusaidia kujiegemeza kwa kuishika miguu yako. Hii ni njia ya kuipa mikono na misuli yako nguvu.

7. Mtindo wa wheelbarrow

Mojawapo ya mitindo ambapo unachoma kalori zaidi. Kadri unavyo weza kufanya mapenzi kwa njia hii, ndivyo unavyo fanya mazoezi zaidi. Na huenda hata ukakosa kufanya mazoezi yako ya kawaida kwani mtindo huu unafanyisha misuli yako kazi zaidi. Mwanamke anajiegemeza kwa mikono na mchumba wake kushikilia mwili wake. Iwapo mwanamke ana uzito zaidi, mtindo huu hautakua rahisi kwake.

8. Arch

Mwanamke hutuliza mikono yake na uzito kuhamia kwenye mabega yake. Na juhudi nyingi huwa kwenye miguu yako huku mwili wako ukitengeneza arch. Kwa wanawake wengi, hii ni mojawapo ya mitindo inayo wasisimua zaidi.

9. Mtindo wa kusimama

Punguza Uzito Wa Mwili Kwa Kufanya Mitindo Hii Ya Ngono

Mtindo huu unatuliza misuli yako baada ya kuhusika katika mitindo mingi tofauti iliyo ifanyisha misuli yako kazi na kukuchosha. Ili kusisimuliwa zaidi, wanawake wanapaswa kusimama kwa mguu mmoja na kuukunja huo mwingine kwenye wachumba wao. Mwanamke anaweza jiegemeza kwa kutumia meza ama ukuta ili kurahisha mtindo huu. Misuli ya miguu inafanyishwa kazi zaidi katika mtindo huu wa kufanya mapenzi.

10. Squatting cowgirl

Mtindo huu wa kufanya mapenzi una fanyisha miguu yako kazi na kukusaidia kuwa na nguvu zaidi. Ni sawa na cowgirl ila wakati huu unachuchumaa kwa magoti ili kuegemeza uzito wako. mwanzoni, huenda ukahitaji usaidizi hadi pale ambapo magoti yako itazoea. Unaweza tumia mikono yako kujiegemeza. Mapaja, miguu na tumbo yako inafanyishwa kazi katika mtindo huu.

Written by

Risper Nyakio