Mitindo Ya Nywele Ya Afro Ya Watoto Wasichana

Mitindo Ya Nywele Ya Afro Ya Watoto Wasichana

Je, unatafuta mitindo ya nywele ya afro ya mtoto wako? Makala haya yata kuongoza kupata mitindo tofauti ya nywele ya mtoto wako.

Ni kweli kuwa unapaswa kutunza nywele ya mtoto wako jinsi unavyo tunza yako. Wakati ambapo huenda nywele ya mtoto wako ikawa na matatizo yake, huwezi tumia kiwango sawa cha bidhaa za nywele unacho tumia kwa nywele zako. Kichwa cha mtoto wako bado kina kua na kiwango kikubwa cha bidhaa za nywele huenda kikafanya nywele zake zikatike. Unataka kitu rahisi, kinacho pendeza na kinacho mstarehesha. Na kupata mitindo ya nywele ya afro inayo timiza malengo haya yote huenda kukatatiza. Kwa bahati nzuri, kuna jambo moja kuhusu nywele za afro litakalo kupendeza. Ina kukubalisha kubadilisha mitindo tofauti kwa nywele za mtoto wako na kuzilinda kutokana na kuharibika. Tuna kusaidia kugundua mitindo tofauti itakayo mfaa mtoto wako.

Mitindo Ya Nywele Ya Afro Ya Mtoto Wako

Hapa chini kuna mitindo ya nywele ya afro ya nywele asili za mtoto wako.

  • Messy side ponytail

Afro baby hairstyles

Mtindo huu wa messy side ponytail ni rahisi na mbio kutengeneza. Mtoto wako anaweza uvalia mahali popote, hata kanisani, shuleni ama kwenye sherehe za kuzaliwa. Chana nywele kuelekea nyuma kisha ufanye ziwe laini. Kisha ushike nywele ulizo chana na uzishike ziwe pony kwenye shingo ya mtoto wako kwa upande wa nyuma.

  • Twist and band
Afro baby hairstyles

Picha: Youtube

Chagua mtindo huu hasa iwapo mtoto wako ana nywele fupi. Unahitaji kuwa na headband na bow ya kupendeza ili kufanya mtindo huu uwe wa kibinafsi kichwani cha mwanao. Mtindo huu ni rahisi, wa kipekee na pia una starehe kwa mtoto wako.

  • Twisted cornrows

Afro baby hairstyles

Twisted cornrow ni mtindo maarufu na hupendeza sana kwa watoto. Anza kwa kugawanya nywele kutoka mbele hadi nyuma, kisha utwist kwa pande utakayo amua. Endelea kuzitwist kutoka mbele ya kichwa hadi nyuma. Kisha ushike kwa kutumia clips ili zisitokane.

  • Funky afro

Afro baby hairstyles

Funky afro ni mtindo unao pendeza kwa mwundo wowote wa uso. Haijalishi iwapo ni wa mviringo, duara ama mwundo wowote ule. Yote unayo hitaji ni tweaks hapa na pale na mtoto wako atakuwa sawa. Mtindo huu unaruhusu nywele za mtoto wako uhuru wowote wa kufanya chochote. Ili kufanya mtindo huu uvutie zaidi, kwanza paka bidhaa ya nywele ili kulainisha. Kisha uchane.

  • Twisted Buns

Twisted buns for girls

Twisted buns zinakupatia chanya cha kuamua ni buns ngapi ungependa kutengeneza na nywele ya mtoto wako. Mtindo huu unakuhakikishia kumfanya mtoto wako apendeze. Gawanya nywele ya mtoto wako kwenye buns nyingi kiasi unacho penda kisha utumie bows kuzipamba. Ni rahisi sana.

  • Mohawks

mitindo ya nywele ya afro

Picha: Youtube

Mtindo wa mohawk ni rahisi kutengeneza. Kuna njia tofauti, zingine rahisi na zingine ngumu. Kusanya nywele katikati ya kichwa na ushike kwa kutumia mipira. Walakini, mitindo migumu zaidi itahitaji mapambo ya nywele zaidi.

  • Bantu knots na buns

mitindo ya nywele ya afro

Bantu knots na buns ni mtindo unao julikana kwa urembo wake na ni rahisi kutengeneza. Mtindo huu ulitengenezwa na Wazulu kutoka South Africa. Ili kufanya mtindo huu upendeze, gawanya nywele kwa vitengo tofauti na kisha kutengenezwa ziwe knot ndogo na kushikwa kwa kutumia mipira. Hakikisha kuwa hujazibana sana ili zisimwumize mtoto kichwa.

Hitimisho

Haijalishi mtindo wa nywele unaochagua wa mtoto wako, hakikisha kuwa hazijambana sana. Pia, epuka kutumia bidhaa za nywele kama kemikali za kulainisha nywele na mapambo ya vyuma.

Soma pia: Mitindo Ya Kusongwa Nywele Ya Kurudi Shuleni Inayo Pendeza

Chanzo: Child Insider

Written by

Risper Nyakio