Mitindo Ya Kusongwa Nywele Ya Kurudi Shuleni Inayo Pendeza

Mitindo Ya Kusongwa Nywele Ya Kurudi Shuleni Inayo Pendeza

Shule zinapo funguliwa tena, wazazi huwa na kazi ya kununua vitu vya shule ambavyo watoto wanahitajika kurudi navyo. Nyumba zilizo na mabinti zinafahamu changamoto za kujaribu kuchagua mitindo ya kusongwa nywele ya kurudi shuleni.

Kuhakikisha kuwa binti yako mchanga anarudi shuleni na sare ya shule iliyo safi na nywele ambazo zitadumu mhula wote. Kuna maana ya, kuanza shule kwa njia ipasavyo na ni muhimu sana, huenda kuka athiri jinsi kipindi hicho kingine cha mhula huo kitakuwa.

black girl back to school hairstyles

Chanzo cha picha: cooleasyhairstyles.com

Hapa ni baadhi ya mitindo ya kusongwa nywele unaweza chagua mtindo utakao kufaa zaidi.

Mitindo ya kusongwa nywele ya kurudi shuleni

1. Mistari (Shuku ama all-up cornrows)
black girl back to school hairstyles

Shuku hairstyle. chanzo cha picha: Pinterest

Shuku ni mojawapo ya mitindo ya nywele iliyo maarufu zaidi nchini Nigeria. Wanawake wa Nigeria wamesongwa mtindo huu wa nywele kwa miaka mingi hata kabla ya kupata uhuru nchini. Ni mojawapo ya mitindo ya kusongwa nywele inayo faa zaidi ya kurudi shuleni na ni rahisi kusuka.

Binti yako anaweza kuwa makini kwa kazi yake ya shule badala ya kuwa na wasi wasi kuhusu nywele zake wakati wote. Huenda ukachagua kumsonga matuta mawili badala ya moja.

2. Jumbo box braids
hairstyles for kids

Box braids. Chanzo cha picha: pinterest

Jumbo box braids sio mtindo unao pendeza tu, ila unakuhakikishia kuwa binti yako hata tumia wakati mrefu akisongwa na msusi wake. Msusi mwema na anaye ijua kazi yake atamaliza mtindo huu kwa masaa machache. Pia, unaweza shika nywele kwa mitindo tofauti baada ya kusongwa.

3. All-back cornrows
black girl back to school hairstyles

All-back cornrows. Picha: hairstylehub.com

Mtindo huu ni maarufu sana kwa wanafunzi wa shule. Unaweza amua mtoto wako asongwe zikiwa nene ama konga kulingana na muda unao taka mtindo huu ukae kichwani chake. Tafadhali fahamu kuwa nyembamba zinakaa kwa muda mrefu zaidi ikilinganishwa na nene. Pia, unaweza weka mapambo kwa ncha za nywele zake iwapo shule yao inakubalisha.

4. Kituta cha juu ama nanasi
mitindo ya nywele ya kurudi shuleni

High puff. Chanzo cha picha: depeinados.com

Mtindo huu wa nywele maarufu kama nanasi unapendeza kwa wote, wakubwa kwa wadogo. Wamama wengi hupenda kutumia jeli ya nywele ili zidumu zaidi. Pia, unaweza nunua nywele za kubandika kufanya nanasi ile ya juu ya kichwa kuonekana nene zaidi. Ila ni vyema kwanza kuhakikisha kuwa shule inakubalisha. Mtindo huu bila shaka unamfanya mtoto wako kupendeza zaidi.

5. Mitindo ya kusongwa nywele za kurudi shuleni: Clap

back to school hairstyles

clap hairstyle. Chanzo cha picha: weddingdigestnaija.com

Huu ni mtindo mwingine ambao hauhitaji kazi nyingi na ni bora wa kurudi shuleni. Nywele zinasongwa kutoka pande tofauti na kuunganishwa katika sehemu ya katikati ya kichwa.

6. Threading
mitindo ya nywele ya kurudi shuleni

African hair threading. Chanzo cha picha: Pinterest

Huenda mtindo huu ukawa na uchungu, ila ukipata msusi aliye na uzoefu, mtoto wako hata hisi uchungu. Wazazi wanapenda mtindo huu kwa sababu unadumu kwa muda mrefu.

7.  Twists
mitindo ya nywele ya kurudi shuleni

Twists. Chanzo cha picha: Thirstyroots.com

Mtindo huu unapendeza sana kwa watoto wachanga, hasa iwapo unaweka mapambo kwenye ncha zake. Kumbuka kuuliza iwapo shule ambayo mtoto wako anasomea wanakubalisha mapambo ya nywele.

 Mambo ya kujua kabla ya kuchagua mitindo ya nywele ya kurudi shuleni

Nywele nyeusi zinapendeza na ni za kipekee, na ni vyema kwa kila mzazi kujua kuwa nywele za kila mtoto ni tofauti. Na si vyema kuwalinganisha kwani, mtindo utakao mfaa mtoto mmoja huenda ukakosa kumfaa mwingine.

Haijalishi iwapo unamsonga nywele mwenyewe ama unatafuta msusi na kumlipa akufanyie kazi ile, unapaswa kukumbuka mambo yafuatayo:

  • Osha nywele yake vizuri kabla ya kuweka mtindo wowote; utamsonga tu ikiwa nywele zake safi
  • Iwache kwenye mashine ili ibaki na unyevu na kulinda nywele za mwanao kutokana na kuharibika
  • Hakikisha kuwa ncha zake hazikatiki
  • Baadhi ya shule huwa na mitindo ya nywele hasa ambayo wanakubalisha wanafunzi kusongwa na ingine kupigwa marufuku.
  • Cha muhimu zaidi ni afya ya nywele ya mtoto wako

Kama mzazi, huenda ukawa uwoga wako ni kuhusu kumpeleka mwanao shuleni na nywele safi na za kupendeza. Mitindo hii iliyo bora kwa watoto itakusaidia kutimiza lengo lako.

Huffpost  Pulse NG

Soma pia: What your baby’s time of birth says about their personality

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio