Mitindo Tofauti Ya Kusonga Nywele Za Wamama Wa Afrika

Mitindo Tofauti Ya Kusonga Nywele Za Wamama Wa Afrika

Sukwa ni njia iliyo rahisi na inayofaa kwa wamama. Nywele za ki Afrika zinaweza songwa miundo tofauti. Walakini huenda mama akawa hana wakati mwingi mikononi. Tume tengeneza orodha ya mitindo rahisi ya nywele ya wamama. Habari nzuri ni kuwa haichukui muda mrefu kusongwa.

Hapa Kuna Orodha Ya Mitindo Ya Nywele Ya Wamama:

All up (Shuku) Cornrows

All up shuku braids for mums

Instagram @piumary_braids

Hii ni mojawpo ya mitindo maalum ya wamama. Je, mtoto wako anapenda kukuvuta nywele? Mtindo huu unahakikisha kuwa nywele zako zimeshikwa kwa kitita kimoja juu ya kichwa chako. Ni muhimu kuangalia mikono ya watoto wako kwani inapenda kugusa gusa.

All Back Ghana Cornrows

mitindo ya nywele ya wamama

Instagram @piumary_braids

Mtindo huu ni rahisi na kama jina linavyo ashiria, unasongwa nywele nyeusi. Iwapo hutaki nywele usoni mwako siku zinazo kuwa na joto, huu ndio mtindo unaokufaa.

Crochet braids

Crotchet braids for mums

Instagram @crotchetbraidsbyjc

Mtindo huu ni rahisi na pia hautahisi uchungu unapo songwa. Unahitaji kununua nywele maarufu za crotchet kama mbili ama tatu. Nywele hizi huwa zimetengenezwa kwa mitindo mbali mbali. Unaweza jisonga mwenyewe ama uite msusi akutengeneze. Kwa sababu ni rahisi kusonga, unaweza chukua muda wa lisaa limoja. Unaweza tumia nywele hizi tena.

Dreadlocs

mitindo ya nywele ya wamama

Instagram @ohenhe_la_locs

Rasta maarufu kama locs zinachukua muda kusonga hasi ikiwa ni mara yako ya kwanza kuziweka kichwani mwako.

Kufuatia uwezo wake wa kukaa, unaweza zivalia kwa muda wa miezi hadi minne. Unahitaji kuziosha na kutumia mafuta unayo shauriwa na msusi wako.

Ila, kuna chaguo lingine. Unaweza nunua nywele za crochet zinazo fanana na rasta na uziweke kichwani mwako. Njia hii unachukua muda mfupi na kukuhudumu kwa muda mrefu.

Box braids

box braids for mums

Instagram @piumary_braids

Hii ni mojawapo ya mitindo maarufu zaidi ya kusongwa kwa wamama wengi. Njia za kusongwa mtindo huu ni nyingi sana na unaweza chagua mtindo unao kufurahisha zaidi. Huenda ukapenda nywele fupi, ndefu ama za wastani. Pia unaweza zigawanya kati kati.

 

Pia kuna chaguo la kusongwa nywele konda ama nene na rangi inayo kupendeza zaidi. Iwapo hutaki kushika ziwe kituta kimoja, pia unaweza ziwachilia ama kushika za mbele na kuwacha zingine zianguke.

Side-swept Cornrows

mitindo ya nywele ya wamama

Instagram @piumary_braids

 

Mtindo huu wa nywele za ki Afrika unapendeza. Unaweza kuzishika kwa njia ambayo upande wako wa uso uko wazi.

Brazilian Wool braids

mitindo ya nywele ya wamama

Instagram @brazilianwoolhair

 

Huenda ukakosa kuamini ila, nywele hizi ni nyepesi sana. Pia ni za bei nafuu ikilinganishwa na nywele zingine. Zinapendeza na kuhakikisha kuwa umerembeka. Ila, ni jambo la busara kusongwa nywele moja ikilinganishwa na kusonga zikiwa mbili.

Bob Braids

mitindo ya nywele ya wamama

Instagram @brazilianwoolhairs

 

Mtindo huu ni maarufu sana kwani ni rahisi kusongwa na pia ni mtindo wa hivi sasa. Pia unaweza tumia mtindo huu iwapo ulinunua nywele ndefu na hutaki kuwa na nywele fupi kichwani chako.

 

Mtindo huu ni rahisi, unaowafaa wengi na pia hauhitaji mengi. Kusonga nywele zako huhakikisha kuwa hauna mambo mengi yanayo kukwaza. Itakufanya uwe na furaha zaidi. Unaweza songwa kwa chini ya masaa manne. Urembo wa nywele za ki Afrika una lingana na idadi ya mambo mengi ambayo tunaweza fanya nayo. Ungependa kusonga mtindo upi?

Soma pia: Gorgeous back to school hairstyles for black girls

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio