Aina 8 Za Mizio Itakayo Kushangaza

Aina 8 Za Mizio Itakayo Kushangaza

Kuwa na mizio huwa maarufu sana kwa watu wa umri tofauti. Kuna baadhi ya mizio inayo julikana ukiwa mchanga.

Kuwa na mizio huwa maarufu sana kwa watu wa umri tofauti. Kuna baadhi ya mizio inayo julikana ukiwa mchanga. Unapo kula chakula fulani na kina kuharibikia na kusababisha kuumwa na mwili ama upele kwenye uso. Wengine wanapo fahamu mizio yao wakiwa wachanga, wengine hujua wakiwa watu wazima. Baadhi ya mizio huisha kadri mtu anavyo zidi kuzeeka. Huku ukiendelea kufahamu mizio zaidi ukiwa katika uzima wako.

Mizio iliyo maarufu sana huwa kuharibikiwa na vyakula kama vile mayai, maziwa ya ng'ombe, siagi na kadhalika. Mbali na aina hizi zinazo julikana, kuna watu walio na mizio isiyo ya kawaida. Tuna angazia zaidi kuhusu aina hizi za mizio.

Je, mizio huibuka kivipi?

Hata kama kuna uvumbuzi na utafiti mwingi katika nyanja ya matibabu ulio fanyika. Wana sayansi bado hawaja gundua hasa kinacho sababisha aina hii ya mizio.

Mizio hufanyika pale ambapo mfumo wa kinga wa mwili una toa kingamwili zinazo fahamu kitu hicho kama hatari kwa mwili, hata kama huenda kikawa sio hatari. Kwa sababu hii, ngozi yako inaanza kuwasha, unapata sinuses ama kuathiri mfumo wako wa hewa na utumbo.

Ikiwa unadhani kuwa mzio wako wa chakula cha baharini ni m-baya. Tazama mizio hii ya kushangaza diposa ugundue kuwa kuna watu wanao tatizika zaidi.

Orodha ya mizio isiyo ya kawaida

1.Maji

Aina 8 Za Mizio Itakayo Kushangaza

Kuna watu walio na mzio wa maji. Hata kama hali hii ni nadra, watu walio na mzio huu huwa na upele na kuwashwa na ngozi wanapo gusa maji. Walio na mzio huu hawawezi kunywa glasi ya maji ama kujipanguza machozi bila kuwashwa ama kuhisi uchungu. Habari njema ni kuwa, mzio wa aina hii huisha na haukai kwa muda mrefu.

2. Mazoezi

Mzio wa aina hii hufanya mtu kuhisi kujikuna dakika 30 baada ya kufanya mazoezi. Mzio huu huanzishwa na jasho hata kama kuna watu wanao ushuhudia hata bila ya kuvuja jasho. Bahati nzuri ni kuwa, wanao tatizika na mzio huu wana suluhu la kunywa antihistamines.

3. Jua

Vitu kama dawa, kemikali na hali za kimatibabu huenda zikafanya ngozi isiwe na nguvu tosha ya kupambana na jua. Bado wana sayansi hawana uhakika kwa nini baadhi ya watu huwa na mzio wa aina hii wakati ambapo wengine hawana. Ishara za mzio huu ni ngozi kuwa nyekundu, kuwasha, kuuma, kuvuja damu na upele.

4. Shahawa

Wana sayansi wana husisha ugumba miongoni mwa baadhi ya wanandoa kusababishwa na mzio wa shahawa. Kugusana na shahawa husababisha ngozi kuuma na kufura kwa siku chache. Kwa kesi hatari zaidi, walio na mzio wa aina hii hushuhudia athari ya mpigio wa moyo ulio ongezeka na kufura kwa koo. Ni hatari sana kwa maisha yao.

5. Baridi

Kuwa mahali baridi ama badiliko ya hali ya anga kuwa baridi ina sababisha mwili kutoa kiwango kingi cha histamine na kemikali zingine za mfumo wa kinga. Na kusababisha shinikizo la damu kupunguka na huenda mtu aka zirai ama katika visa nadra kufariki.

Pia, mzio huu husababishwa na vinywaji baridi na kumfanya mtu huwashwa, kuwa mwekundu ama kuvimba.

6. Mfuko wa maharagwe

Baadhi ya watu huwa na mzio wa vumbi inayo toka kwenye mfuko wa maharagwe.

7. Shinikizo

Katika mzio wa aina hii, mtu hufura miguu, kugeuka kuwa nyekundu ama kujikuna anapo valia mavazi yanayo m-bana mwili. Na kumfanya ahisi uchungu ama kukosa starehe.

8. Mzio wa dawa

Aina 8 Za Mizio Itakayo Kushangaza

Huu ni mojawapo ya aina iliyo hatari zaidi. Watu walio na mzio huu huwa na matatizo mengi. Una husishwa na viungo vinavyo tumika kutengeneza dawa hizo kama antihistamines zilizo chakatwa badala ya kutumia zilizo asili.

Je, una mzio wowote? Mzio ulio nao ume kuathiri kivipi? Unafahamu aina zingine za mizio ambayo hatuja orodhesha. Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi.

Soma pia:Kulala Sana Kuna Athari Hasi Kwa Afya Yako

Written by

Risper Nyakio