Ni kawaida kwa mjamzito kuwa na tumbo dogo. Hakuna wakati haswa ambapo tumbo huanza kuonekana katika ujauzito. Kuwa na tumbo ndogo huenda kukamfanya mama ahisi kana kwamba hana mimba. Baadhi ya wanawake huingia kwenye muhula wa pili wa mimba na bado mimba haionekani. Jambo ambalo linaweza kumfanya mama apate wasiwasi. Kila mwili wenye mimba huwa tofauti, ni muhimu kwa mama kutokuwa na hofu. Iwapo anazingatia ushauri wa daktari wake na daktari kuhakikisha kuwa mtoto anakua ipasavyo, sio chanzo cha shaka.
Baadhi ya wanawake hutarajia mimba yao kuanza kuonekana kati ya mwezi wa tatu na wa nne. Kuna sababu ambazo huenda zikamfanya kuwa na mimba isiyo onekana sana.
Sababu za mjamzito kuwa na tumbo dogo

Mimba ya kwanza. Wanawake walio na mimba ya mara ya kwanza huenda wakachukua muda kabla ya ujauzito wao kuanza kuonekana. Kwa wanawake walio kuwa na mimba tena, itaanza kuonekana mapema kwani misuli yao imenyooshwa na mimba ya hapo awali.
Mama kuwa mrefu. Wanawake warefu huwa na mimba ndogo ikilinganishwa na wanawake wafupi, wajawazito warefu wana nafasi zaidi ya mtoto.
Mjamzito kuwa na misuli yenye nguvu. Mimba kwa wanawake walio na misuli yenye nguvu zaidi huchukua muda kabla ya kuanza kuonekana.
Uzito wa kupindukia. Kwa wanawake walio na uzito wa kupindukia, tumbo ya mimba huchukua muda zaidi kabla ya kuanza kuonekana.
Sawa na watoto, mimba huja na shepu na saizi tofauti. Ikiwa mama anakula, kunywa, kufanya mazoezi na kwenda kliniki inavyotakikana, na tumbo ingali dogo. Asiwe na shaka, ikiwa mtoto wake anakua vyema kulingana na kila hatua, sio chanzo cha shaka. Wanawake waliokuwa wamezoea kufanya mazoezi makali hapo awali pia huenda wakawa na tumbo dogo. Kwani misuli yao ina nguvu na kukaza mimba kuonekana mapema.
Wanawake wanaokuwa wamebeba watoto wadogo wana nafasi kubwa ya kuwa na mimba dogo. Sababu za kuwa na mtoto mdogo ni kama vile:

Mama kutumia vileo na sigara. Utumiaji wa vitu hivi una athari hasi kwa ukuaji wa fetusi na kuongeza nafasi za mama kuwa na mimba ya mtoto mdogo.
Matatizo ya placenta. Placenta huwa na jukumu kubwa kwa maisha ya mtoto. Placenta inapofeli kutimiza majukumu yake, mtoto hupoteza chakula na hewa kwenye uterasi na kuifanya iwe vigumu kwake kukua ipasavyo.
Matatizo ya fetusi. Ikiwa fetusi haina usawa wa geni ama ina maambukizi, haitakua ipasavyo na mama atakuwa na mimba dogo.
Ikiwa mjamzito kuwa na tumbo dogo kunamtia wasiwasi, ni vyema kufanyiwa ultrasound kuhakikisha kuwa mtoto anakua ipasavyo.
Chanzo: WebMD
Soma pia: Ukuaji Na Maendeleo Ya Fetusi: Mama, Tarajia Haya Katika Mimba Ya Miezi 6