Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Zaidi Ya Miaka 35

Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Zaidi Ya Miaka 35

As women enter their thirties, they may experience a rapid decline in their fertility. Women, who are thirty five and are planning to give birth, may have several serious complications.

Kuwa mjamzito ukiwa zaidi ya miaka 35 sio matembezi kwenye mbuga. Kuachiliwa kwa yai hupunguka katikati ya miaka ya thelathini na saizi ya yai pia hupunguka. Haya mabadiliko ya kuachiliwa kwa yai, husababisha mabadiliko kwenye homoni pia.

Pia kuna uwezekano wa kupungua kwa idadi na afya ya mayai inayoachiliwa: ambayo ni sababu kwa nini hupendekezwa wanawake kupata mimba wakiwa chini ya miaka 35.

pregnant over 35

 Ni Changamoto Zipi Zina Husiana Na Kuwa Mjamzito Katika Umri Zaidi Wa Miaka 35?

 Hatari zinazo husiana na umri

Ni kweli kwamba sayansi ya kimatibabu imeendelea na leo kina mama walio na umri wa zaidi ya miaka 35 huwa na ujauzito salama. Ingawaje, kuna athari nyingi zinazotokana na kuchelewesha kujifungua mtoto na nafasi za ujauzito salama na kujifungua mtoto mwenye afya pia hudidimia na wakati na umri.

Imedhibitishwa kisayansi kuwa  kina mama ambao hujaliwa watoto wakiwa katika umri wa miaka thelathini, huwa na nafasi kubwa ya kujifungua mtoto mwenye matatizo. Sababu kuu ya hili huwa miaka ya mama ambayo husababisha yai kujigawanya isivyo kawaida

 Matatizo mengine yanaweza kuibuka

Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Zaidi Ya Miaka 35

Msukumo wa damu mwilini na ugonjwa wa kisukari unaweza kutokea wakati wa ujauzito. Kwa hivyo, wanawake walio na umri wa zaidi wa miaka thelathini wako katika hatari kubwa.

Iwapo wewe ni mjamzito na zaidi ya miaka 35, ni vyema upate utunzi wa mapema kabla ya kujifungua ili upate uaguzi mapema na matibabu.

Kujifungua mtoto aliyeaga (stillbirth) huwa kawaida katika kina mama wa umri wa zaidi ya 35. Kina mama waliokomaa pia wana uwezekano wa kujifungua watoto walio na uzito wa chini (walio na uzito wa chini ya ratili 5.5 wanapozaliwa). Upasuaji pia huwa kawaida kwa kina mama wanaojifungua mtoto wao wa kwanza baada ya miaka 35.

Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Zaidi Ya Miaka 35

Ni vyema kwa mwanamke kupatana na daktari wake ili kupata mashauri. Historia ya kimatibabu ya wazazi wote wawili inaweza kuonyesha hali ambazo zinaweza kuthuru afya ya mama na mtoto.

Pia, ni nafasi ya kuchunguza ujauzito na kupima damu kwa hali kama vile kinga ya rubella na vipimo vya uke vinavyohitajika kabla ya kuwa mjamzito.

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Roshni Mahtani na kwa mara ya kwanza kuchapishwa katika tovuti ya  TheAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Soma pia: A Comprehensive List Of Chemicals To Avoid During Pregnancy

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio