Mkojo wa mtu mwenye mimba huwa na homoni ya human chorionic gonadotropin (hCG). Vipimo vya mimba hupima kuwepo kwa homoni hii. Mama anapotunga mimba, placenta yake hutoa hCG.
Mkojo wa mtu mwenye mimba

Ikiwa una mimba, kipimo cha mimba kitadhibitisha kuwepo kwa homoni ya ujauzito siku moja baada ya kukosa kipindi cha hedhi. Vipindi vya kichocheo cha hCG huongezeka maradufu katika wiki ya 8 na 10 na kufika kiwango cha juu zaidi katika wiki ya 10 ya ujauzito. Kisha kuanza kuenda chini hadi mama anapojifungua. Vipimo vya mimba vya kinyumbani vinatumika kufahamu hali ya mama.
Matumizi ya vipimo vya mimba vya hCG
Vipimo hivi ambavyo mara nyingi huwa vya kinyumbani, hudhibitisha iwapo mkojo wa mwanamke una homoni ya mimba ya hCG, na wala havionyeshi viwango vyake. Iwapo mwanamke ana homoni hii kwenye mkojo wake, kipimo kitakuwa chanya. Kudhibitisha kuwa ana mimba.
Hatari za kipimo hiki
Kipimo hiki hakina hatari, mbali na kuonyesha matokeo hasi kipimo kinapofanywa mapema sana. Kipimo huenda pia kikaonyesha matokeo hasi yasiyo kweli kinapotumika muda baada ya urefu wake.
Jinsi ya kufanya kipimo cha mimba

Hakuna matayarisho muhimu yanayohitajika kabla ya kufanya kipimo hiki. Kumbuka kuangazia haya:
- Soma na ufuate maagizo yaliyo kwenye kipimo
- Tumia kipimo kabla ya tarehe ya kuharibika kwake
- Fanya kipimo asubuhi baada ya kuamka
- Epuka kunywa chochote kabla ya kufanya kipimo cha mimba
Kufanya kipimo kutumia mkojo wa kwanza wa siku kunahakikisha kuwa kiwango cha hCG huwa kimekolea. Kunywa maji ama kiamsha kinywa zimua mkojo na kufanya iwe vigumu kidhibiti kuwepo kwa kiwango cha hCG.
Kutofuata maagizo ya kipimo kunaibua hatari ya kupata matokeo yasiyo sahihi. Kufanya kipimo cha mimba mapema sana, kutatoa matokeo hasi hata kama mwanamke ana mimba. Ili kupata matokeo bora, ngoja wiki moja baada ya kukosa kipindi cha hedhi.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Sababu Ya Matiti Kutoa Maji Wakati Wa Ujauzito Ni Nini?