Wanaume Wanapaswa Kuwapa Bibi Zao Kipau Mbele Juu Ya Watu Hawa Watano

Wanaume Wanapaswa Kuwapa Bibi Zao Kipau Mbele Juu Ya Watu Hawa Watano

Kwa mabwana wote, hakikisha kuwa bibi yako ndiye nambari moja katika mambo yote.

Msingi mzuri wa uhusiano wako ni muhimu ili kuwa na ndoa yenye mafanikio. Utaweza vipi kujenga msingi huo? Hakikisha kuwa wakati wote una mthamini na u- mpe bibi yako kipau mbele juu ya watu hawa watano!

prioritize your wife

Mpe bibi yako kipau mbele juu ya watu hawa:

1.  Watoto wenu

Naam, umesikia vizuri, watoto wenu. Kabla ukasirike nasi, tusikize kwanza.

Kwa nini unapaswa kumpa bibi yako kipau mbele kabla ya watoto wenu? Kwa sababu kuwa na uhusiano mwema na wenye afya na bibi yako bila shaka kutafanya uwe na uhusiano mwema na watoto wako. Watoto wenu wakiona kuwa wazazi wao wana penda, wana jali na wana heshimiana, wata fuata mfano wenu hata katika uhusiano wao.

Bila shaka kumpa bibi yako kipau mbele juu ya watoto wenu kunapaswa kutendeka kulingana na kesi, kwani baadhi ya wakati, huenda mahitaji ya watoto wenu yakawa muhimu zaidi kuliko ya bibi yako. Kama ilivyo desturi, shughulika na furaha ya bibi yako na mambo mazuri yata fuata.

prioritize your wife

2. Wanawake wa kufikiria

Ni sawa kufurahishwa na watu maarufu na hata waigizaji. Walakini, kufurahishwa nao kupita mipaka hadi unaanza kuwafikiria mnapo kuwa mkishiriki mapenzi na bibi yako kutazua ugomvi na utakuwa na tatizo kubwa.

Hauhitaji kuwaangalia wanawake wengine ili 'kupata hamu.' Na iwapo unafurahishwa sana na watu maarufu wanaopendeza, utaanza kulinganisha urembo wao na wa bibi yako. Mwangalie bibi yako anaye vutia na anaye kupenda kwa dhati na huyo peke yake ndiye unaye hitaji maishani mwako.

3. Wanawake wengine

Bila hata kusema, haupaswi kuwaweka wanawake wengine mbele ya mahitaji ya bibi yako, hata kama hakuna njama fiche. Bibi yako anapaswa kuwa mwanamke nambari moja maishani mwako na anapaswa kuwa mwanamke anaye kuja mbele ya wanawake wengine.

4. Wakwe zako

Ikiwa kuna ugomvi kati ya bibi yako na wakwe zako, unapaswa kumwunga mkono bibi yako wakati wote. Kwa nini? Kwa sababu yeye ndiye bibi yako. Lakini ukweli ni kuwa, uhusiano na wakwe zako mara nyingi huwa na pande hasi na chanya na hakuna wakati ambapo mambo yote yatakuwa asilimia 100 sawa.

Ndoa yenu ni jambo tofauti na ni muhimu kulenga kuwa na utangamano na uhusiano wa karibu na bibi yako na kufanya ndoa yenu iwe bora zaidi.

Wanaume Wanapaswa Kuwapa Bibi Zao Kipau Mbele Juu Ya Watu Hawa Watano

5. Marafiki wako

Bila shaka marafiki ni muhimu sana maishani mwetu. Kama kiumbe binafsi na pia kama familia, ni vigumu kuishi bila marafiki kwani binadamu hajitoshelezi. Lakini unapo oa, mahitaji yana badilika na maisha yako kuchukua upande tofauti. Baadhi ya wakati, uhusiano wako na marafiki wako huenda ukaathiriwa, haijalishi kipindi ambacho mmekuwa pamoja.

Lakini itazame hivi, ikiwa walikuwa marafiki wa kweli, wanapaswa kuelewa kuwa mambo yame badilika na bibi yako ndiye unapatia kipau mbele. Haimaanishi kuwa umesahau nyakati zenu mlipo fanya mambo ya kufurahisha pamoja.

Chanzo: familyshare.com

 

Written by

Risper Nyakio