Je, Mshono Wa Bwana Ni Wa Ukweli Ama Ni Imani Tu?

Je, Mshono Wa Bwana Ni Wa Ukweli Ama Ni Imani Tu?

Makala haya yanaelezea zaidi kuhusu mshono wa bwana!

Mtoto wako alikuwa miezi 8 nilipokuwa tayari kurejelea maisha yangu ya mapenzi. Baada ya kipindi kirefu hivyo, singe ngoja bwanangu anipapase tena. Pia yeye alikuwa na furaha kuwa nilikuwa tayari tena. Sisi wote tulitaka kufurahishana baada ya kipindi kikubwa hivyo. Ila, baada ya dakika chache, iligeuka ikawa ndoto mbaya. Huku bwanangu akijaribu kuniingia, nilihisi uchungu mwingi sana kwa uke wangu. Hapo ndipo tuligundua kuwa daktari alikuwa amenipatia mishono mingi ya episiotomy. Naam, alikuwa amenipatia mishono hiyo isiyo julikana ya mshono wa bwana.

Je, Mshono Wa Bwana Ni Wa Ukweli Ama Ni Imani Tu?

Je, mishono ya bwana ni nini?

“Mishono ya bwana” maarufu kama husband stitches kwa kawaida ni mishono zaidi ya episiotomy. Episiotomy inafanyika pale ambapo nafasi kati ya uke wako na sehemu ya nyuma, unapo jifungua.

Mishono zaidi ya bwana inapaswa kufanya uke wako uwe na mkazo zaidi wa “furaha zaidi” kwa mchumba wako wakati wa ngono, unapo shauriwa.

“Mshono wa bwana” umebaki kuwa imani ya mjini… hadi sasa. Wamama wengi wana jitokeza na kushuhudia ukweli kuhusu “mshono wa bwana” ama “daddy stitch,” ambayo kwa kawaida hufanywa bila mama kufahamu ama maarifa yao.

Jambo hili linaaminika kuwa la kijinsia na wengi. Na wakati ambapo jambo hili linafaa kufanywa kumfurahisha mwanamme, mwishowe huleta uchungu mwingi kwa mama.

Episiotomy stitches: Husband stitch is not a myth

Hakuna utafiti unao dhihirisha nambari hasa ya wanawake walio athiriwa. Walakini, wanawake wameanza kujieleza zaidi kuhusu waliyo yapitia.

Kati ya wengine wengi, Alicia Wanstall Burke hivi majuzi aliwaeleza wafuasi wake katika mitandao yake ya jamii kilicho mfanyikia. Alisema: “Habari zenu! Naam, haya yalinitendekea! Sina uhakika kuwa yalifanywa kimaksudi na daktari, ila nilifanyiwa upasuaji wa kutengeneza. Kwa hivyo, hakuna kujifungua kwa njia ya uke kwangu!”

episiotomy stitches

Episiotomy stitches are normal, but not “husband stitches”. Image: Instagram

Raquel Rosario Sanchez pia katika mtandao wake wa Twitter alisema, “Sio imani, nina binamu zangu waliofanyiwa uchungu huu usio hitajika kwa sababu daktari alipenda kuwafurahisha mabwana zao.”

Neve alisema, “Daktari aliye nishona baada ya kujifungua aliniambia hivi bila fiche.”

Venetia Booth alisema kuwa jambo hili lilimtendekea pia. Pia alisema kuwa hospitali haikua na idhini yake na kuwa alifanyiwa upasuaji mwingine kutengeneza hali hiyo.

Nini kinacho tendeka wakati wa episiotomy?

mshono wa bwana

Picha: Instagram

Wakati wa kujifungua, kuna uwezekano wa asili wa uke kuraruka. Ama wakati mwingine, madaktari wanaweza kata kimaksudi tishu zilizo laini ili ujifungue kwa urahisi.

Baada ya kujifungua, kuraruka huku, iwapo kwa asili ama kwa kimaksudi, lazima kushonwe. Hapa ndipo baadhi ya madaktari wanasemekana kuwa wakiongeza mishono zaidi kwa uke ulio na mkazo zaidi, ukiweka akilini kufurahia kwa mwanamme wanapo rejelea ngono.

Wataalum wanasema nini kuhusu jambo hili?

ObGyn Jesanna Cooper, Mkurugenzi mkuu anasema kuwa haijalishi njia ambayo kuraruka huku kwa uke kunatendeka, kuna uwezekano kufanya uke uwe na mkazo zaidi kupitia kwa kushona. Hali ya uke haifai kubadilishwa na mshono kwa sababu ina zaidi ya kufanya na nguvu za sakafu ya pelviki na sio saizi ya kufunguka kwa uke wako.

Kushona kunaweza fanya mlango wa uke wako uwe na mkazo zaidi. Ila, hakuna ushuhuda dhairi kuwa mwanamme atafurahia.

Kutengenezwa kwa uke kuna kusudiwa kurejesha ngozi pamoja ili mchakato wa kupona kwa mwili kuimarike, sio kukaza uke wako.

Ila katika wakati huo huo, hatuwezi puuza wamama hawa ambao wamejitokeza kusimulia hadithi zao za, “mshono wa bwana.” Kwa hivyo, unafikiria nini? Je, jambo hili limekutendekea?

Chanzo: Yahoo Be, Huffington Post, Health Line, You Tube

Soma Pia: These Husbands Have Found Creative Ways To Tackle Their Pregnant Wife Problems

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Abigail na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

 

Written by

Risper Nyakio