Dalili 4 Za Kukuonya Dhidi Ya Mshtuko Wa Moyo Kwa Wanawake

Dalili 4 Za Kukuonya Dhidi Ya Mshtuko Wa Moyo Kwa Wanawake

Wanawake sawa na wanaume wako katika hatari ya kuugua mshtuko wa moyo na kufahamu dalili zake, itawasaidia kujua wakati wanapo faa kupata matibabu.

Wanawake sawa na wanaume wako katika hatari ya kuugua mshtuko wa moyo ama moyo kusita. Sio watu wengi wanao fahamu dalili za mshtuko wa moyo kwa wanawake. Kufahamu dalili zake kunaifanya iwe rahisi kwako kutibiwa kwa kasi kabla ya hali kukuzidia.

Dalili 4 Za Mshtuko Wa Moyo Kwa Wanawake

dhiki baada ya kujifungua

Unapo ona mojawapo ya ishara hizi za moyo kusita katika wanawake tutakazo angazia, ni vyema kukimbia kwenye kituo cha matibabu bila kusita. Kwani, ingawaje zinaonekana kuwa dalili nyepesi, huenda zikasababisha kifo zisipo tibiwa.

 1. Uchovu usio wa kawaida

Ni kawaida kwa wanawake hasa walio na watoto kuhisi uchovu kufuatia kufanya kazi nyingi siku yote. Walakini, ikiwa unahisi kuchoka kusiko kwa kawaida, huenda ikawa ni jambo la busara kwako kwenda kufanyiwa vipimo. Tuna maanisha nini tunapo ongea kuhusu kuchoka kusiko kwa kawaida?

 • Unahisi umelemewa zaidi kuliko ilivyo kawaida yako baada ya kufanya kazi zako za kawaida za kila siku
 • Hata bila ya kufanya kazi ngumu, unahisi kuwa kifua chako kina fungana. Kazi ndogo kama kutembea ama kutengeneza kitanda chako baada ya kuamka
 • Umechoka lakini bado unaamka masaa yasiyo ya kawaida usiku

2. Jasho baridi, kupungukiwa na hewa, kichefu chefu

Kadri mtu anavyo zidi kuzeeka, kutofanya mazoezi na kuongeza uzito wa mwili kunaweza sababisha kupungukiwa kwa hewa. Katika umri wa ugumba, wanawake hushuhudia vipindi vya joto jingi. Walakini, huenda ikawa ni mshtuko wa moyo ikiwa ni kupungukiwa kwa hewa ama bila maumivu ya kifua sawa na kukimbia mbio za masafa marefu, lakini haujafanya chochote.

Ishara ni kama vile:

 • Kutoa jasho kwa kasi ama kupungukiwa na hewa bila kufanya mengi
 • Kushindwa kupumua kunako zidi baada ya kufanya kazi
 • Kutatizika kupumua unapo lala chini kunako punguka unapo keti
 • Kutoa jasho ya fikira nyingi hata usipo kuwa na mawazo mengi akilini
 • Kutoa jasho ama kutatizika kupumua kunako andamana na ishara zingine kama kuumwa na kifua ama uchovu

3. Uchungu katika sehemu tofauti

Mwili wa binadamu ni mfumo unao unganisha viungo tofauti. Mara nyingi, tatizo katika sehemu moja inaweza sababisha matatizo katika sehemu zingine mwilini.

Katika kesi hii, uchungu ama kukosa starehe kwenye mkono, mgongo, shingo, ama tumbo kunaweza kuwa ishara ya hali ya moyo. Na hasa kama chanzo cha uchungu huo ni vigumu kudhibiti.

Ikiwa uchungu huo una anza na kuzidi, unapo jaribu kufanya kitu na kisha kuisha unapo pumzika, unapaswa kufanyiwa vipimo.

4. Kuumwa na kifua

Hii ndiyo ishara maarufu zaidi ya mshtuko wa moyo kwa wanawake. Huenda ikawa ni shinikizo isiyo na starehe, kufinywa ama uchungu mwingi kwenye sehemu ya katikati ya kifua chako. Kwa dakika chache. Na katika wakati mwingine hupungua na kuisha kabla ya kurudi.

Kujikinga dhidi ya maradhi ya moyo kusita

mshtuko wa moyo

Epuka kufanya mambo haya:

 • Ratibisha kukutana na daktari wako kufunzwa kuhusu athari zako za ugonjwa wa moyo
 • Kukoma kuvuta sigara
 • Fanya mazoezi. Hata mepesi kama vile kutembea kwa angalau dakika 30 kila siku
 • Badilisha lishe ya familia yako iwe yenye afya zaidi

Wakati wa kumwona daktari

 • Unapo ona mojawapo ya dalili tulizo orodhesha za mshtuko wa moyo
 • Wajulishe kuhusu historia ya mshtuko wa moyo kwenye familia
 • Ongea kuhusu mawazo mengi na hali ambazo huenda zikachangia kuwa na tatizo hili

Soma Pia:Vidokezo Muhimu Kwa Wanawake Walio Na Watoto Mapacha

Written by

Risper Nyakio