Mtaalum Aeleza Kwa Nini Aliwacha Kuoga Miaka 15 Iliyo Pita

Mtaalum Aeleza Kwa Nini Aliwacha Kuoga Miaka 15 Iliyo Pita

David Whitlock, ambaye ni mhandisi wa kemikali za MIT na mwanzilishaji wa AOBiome, ambayo ni kampuni ya clinical-stage microbiome, alieleza safari yake ya kuacha kuoga miaka 15 iliyopita na hanuki vibaya.

Mtaalum huyu alidhibitisha haya kati ya hamu inayo kua ya viini vya ngozi vinavyo linda watu kutokana na vimelea na kuweka mwili ukiwa na afya kwa kutumia kemikali zinazotumika.

Kufuatia mahojiano mwaka wa 2015 alipo sema kuwa watu huchanganya "safi" na "uwezo wa kuzaa", Whitlock hivi majuzi aliiambia The Guardian hivi majuzi kuwa husuuza sehemu ya mwili yake kwa maji inapo chafuka- lakini kamwe hatumii sabuni.

"Ilikuwa jambo geni kwa miezi ya kwanza michache, ila baada ya hapo, nilianza kuzoea. Nikipata sehemu fulani ya mwili wangu imechafuka, nitaiosha sehemu hiyo ila sio kwa kutumia sabuni," alisema.

Kulingana naye, kilicho mfanya aanze njia hii mpya ya maisha ni kuhimiza vijidudu vizuri kuishi juu yake na kwa utengamano; na kula ammonia inayo tokana na jasho yake; na kumpa ngozi isiyo hitaji vitu vingi".

Wakati ambapo jambo hili huenda likahusishwa na siku za hapo awali, Whitlock anaonekana sio mtaalum wa pekee ambaye ana amini kitendo hiki.

Sarah Ballantyne, ambaye ni medical biophysicist, pia ali himiza mtindo huu wa maisha. Alisema anatumia maji pekee kuoga hata baada ya kutoa jasho jingi baada ya kufanya mazoezi mengi.

Kwa upande wake, Sandy Skotnicki, ambaye ni mtaalum wa ngozi huko Toronto, alisema, "hakuna jambo mbaya na kuji suuza."

"Nimeongea na watu wengi ambao hawajatumia sabuni zozote kuoga kwa miaka mingi na wako sawa. Kutoka 1950, tumetoka kuoga siku moja kwa wiki hadi kuoga kila siku. Je, hilo limebadilisha microbiome ya ngozi? Nafikiria jibu ni ndiyo. Na jambo hili lime sababisha ongezeko katika maradhi ya ngozi. Ila jambo hili halija dhibitika kabisa," aliongeza.

Katika mshipa sawa, Jackie Hong, mtangazaji huko Yukon, Kaskazini Mashariki Canada, alisema kuwa hajatumia sabuni kuoga kwa muda wa miaka tisa.

"Natumia mikono yangu kujisugua na kutoa uchafu wowote, ila nimekaa kortini ama kwenye dawati langu siku nyingi, kwa hivyo sio kana kwamba nina uchafu mwingi," alisema.

Hata kama hakuna ishara dhibiti kuwa kuepuka sabuni kunasaidia kutopata maradhi ya ngozi, Whitlock alisema kuwa kuacha kuoga kwake kume kuwa na majaribio ya mafanikio kwake.

Bidhaa zilizo na vijududu na probiotic zilizo tengenezwa kutokana na bakteria iliyo vunwa kutoka kwa shamba za wanyama, alisema zilifanya awache kunuka na kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya ngozi.

Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye The Cable na yaliandikwa na STEPHEN CHARLES KENECHUKWU. Yaka chapishwa na idhini, kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Soma Pia: Umuhimu Wa Vidoli Vya Ngono Vya Wanandoa Na Umuhimu Wake Katika Ndoa

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio