Mtindo Ibuka Wa Palazzo Pants Nchini Kenya

Mtindo Ibuka Wa Palazzo Pants Nchini Kenya

Mtindo maarufu wa kuvalia suruali zilizo pana kwenye sehemu ya miguu umekuwa mtindo ibuka hasa mwaka uliopita na mwaka huu. Kwa kawaida palazzo pants zinavaliwa sana majira ya joto. Yana nafasi tosha hivi kwamba suruali hizi hazim bani sehemu yoyote ya mwili. Kwa hivyo kunapokuwa na joto, zinakukubalisha kufanya kazi yako vizuri bila kubanwa ama kuhisi kana kwamba mwili una joto jingi zaidi. Nyenzo zinazo tumika kutengeneza suruali hizi huwa rahisi na kwa sababu hii, suruali hizi hazivaliwi majira ya baridi.

Palazzo pants zilijulikana kw asana miaka ya 1960 na 1960 ambapo mtindo huu uliibuka. Waigizaji mashuhuri kama vile Greta Garbo na Katharine Hepburn walikuwa miongoni mwa wanawake wa kwanza kuvalia suruali za mtindo huu.

palazzo

Ila nini hasa kilicho sababisha kuibuka kwa mtindo wa palazzo pants?

Baadhi ya hoteli na watu walikuwa dhidi ya wanawake kuvalia suruali kama za wanaume. Ili wakubalike na waendelee kuvalia mifuto, wanawake hawa walipata suruali zilizo kuwa ndefu, kana kwamba rida la wanawake na bado kutimiza hamu yao ya kuvalia suruali.

Tuna angazia njia tofauti za kuvalia mtindo huu

Rangi tofauti (color block)

Kwa wanawake jasiri wasio ogopa kutumia rangi tofauti. Kuna mtindo maarufu unaojulikana kama color block, ambapo unavalia rangi tofauti.  Iwapo una palazzo pant ya rangi ya kijani, unaweza valia blousi ya rangi tofauti nay a kuvutia kama vile kinjano ama nyekundu.

palazzo pants

Rangi sawa (monochrome)

Kwa mtindo huu wa kuvalia rangi sawa, hasa huwa muhimu sana iwapo unavalia kwenda pahala rasmi kama vile ofisini. Unavalia suruali ya palazzo yenye rangi sawa na blausi yako.

Ankara

Katika mtindo wa aina hii, unavalia pant yako na blausi ya ankara. Mtindo maarufu sana katika Afrika ambapo unatengeneza nguo zako na nyenzo za kiafrika.

ankara palazzo

Huenda ukawa na maswali mengi kama vile ni wanadada wa umri upi wanao valia suruali za aina hii. Usiwe na shaka, mtindo huu unavaliwa na wanawake wa umri wowote ule. Kutoka wenye umri mdogo, wastani hadi wa makamo. Hauna thibiti la umri. Cha kufurahisha zaidi na mtindo huu ni kuwa unaweza valia kuenda mahala popote. Kutoka kuenda kanisani, darasani iwapo wewe ni mwanafunzi, kazini, pwani ama matembezi yako.

Kwa hivyo usiwe na shaka, hakikisha kuwa una palazzo pants kwenye nguo zako!

Written by

Risper Nyakio