Kuwa Makini Kuona Mabadiliko Haya Katika Mtindo Wa Kulala Wa Mtoto Wako

Kuwa Makini Kuona Mabadiliko Haya Katika Mtindo Wa Kulala Wa Mtoto Wako

Mbali na kuwa makini na lishe ya mtoto wako na kuhakikisha kuwa anakula vyema, ni vyema kwa mzazi kuhakikisha kuwa ana angalia mtindo wa kulala wa mtoto wake.

Je, umewahi kumsikia mtoto wako akicheka akiwa amelala? Kisha unakimbia kuangalia kama ameamka na kumpata ame tabasamu. Lakini mara nyingi ni mtoto wako huwa anacheka usingizini. Lakini, ni kipi kinacho sababisha watoto kucheka usingizini? Ni kawaida kwa watoto ama huenda wakawa wanaota kuhusu mambo mazuri? Mabadiliko katika mtindo wa kulala wa mtoto wako.

Tuna fahamu zaidi.

Mabadiliko Katika Mtindo Wa Kulala Wa Mtoto Wako: Sababu Za Watoto Kucheka Usingizini

Unafahamu kuwa kama watu wazima, sisi pia hucheka tukiwa tumelala? Huenda ukawa umemsikia mchumba wako akicheka usingizini.

Hakuna sababu hasa kwanini watoto hucheka usingizini wao. Lakini kuna imani chache kwa nini mwanao anafurahikia akiwa amelala.

  1. Ni jambo la kawaida

mtindo wa kulala wa mtoto

Watoto huota na wao huanza mapema wangali tumboni mwa mama zao. Wanaendelea kuota hata baada ya kuzaliwa. Lakini sio lazima iwe wanacheka kwa sababu ya ndoto. Baadhi ya wakati, kucheka ni jambo la kawaida katika mzunguko wa usingizi al maarufu kama usingizi hai.

Katika aina hii ya usingizi, watoto huenda wakafanya vitendo bila kufahamu. Baadhi ya vitendo wanavyo fanya huenda vika sababisha kucheka ama kutabasamu wakiwa wamelala.

Vidokezo: Kuna uwezekano, hata kama nadra, kuwa gelastic seizures zinaweza tendeka kwa watoto wachanga na kusababisha kicheko kisicho na kifani. Huenda kila kipindi kikawa cha angalau sekunde 10 hadi 20, kwa mtoto wa miezi angalau 10.

Ikiwa jambo hili hufanyika sana na kumwamsha mtoto, ikifuatiwa na kuangalia mahali bila kufanya chochote, tafadhali ongea na mtaalum wa watoto.

2. Wana chakata ujumbe

ulezi wa usiku

Siku yote, hasa miezi ya kwanza michache ya maisha ya mtoto, wana shuhudia aina ya kusoma. Kutoka kufungua macho yao, kutabasamu, kulia na kujaribu kufahamu jinsi miili yao inavyo fanya kazi, wakati wote wana chakata ujumbe mpya.

Ongeza mwangaza wa kung'aa na kelele na kuona vitu tofauti kila siku, huenda waka zidishia viungo vyao kazi. Lakini ikifika wakati wa kulala, akili zao zinapata wakati wa kuchakata ujumbe.

Njia moja ya kufanya hivi ni kwa kucheka, ama kulia wakiwa usingizini. Katika miezi hii muhimu ya ukuaji wao, pia wanasoma mengi kuhusu hisia, ambazo hupitishwa kupitia kwa kicheko ama kulia.

Vidokezo: Jaribu kuto waamsha wanapo kuwa wakicheka usingizini kwani huenda kukaingilia katika mzunguko wao wa kulala.

Elewa mzunguko wa usingizi wa watoto vyema

Watoto wana mzunguko wa usingizi ulio mfupi ikilinganishwa na watu wazima. Ikiwa umesahau mfumo wako wa usingizi, hivi ndivyo watu wazima hulala.

Mfumo wetu wa usingizi huwa dakika 90, ambako kwa kila mmoja huwa na hatua tano za usingizi. Za kwanza nne huwa kwa kimombo 'non-rapid eye movement (NREM) na ya tano huwa rapid eye movement (REM).

Kwa watoto, mzunguko wao wa usingizi huwa dakika 30-50. Na huendelea kuongezeka wanapo endelea kukua.

Vidokezo: Kila mtoto ni tofauti na mtindo wa kulala wa kila mtoto pia huwa tofauti. Kwa hivyo, kumbuka kuwa baadhi ya watoto hupata usingizi kwa kasi, wengine pole pole na huenda wakawa kwa usingizi mwepesi kwa hadi dakika 20, kabla ya kuingia kwa usingizi mzito.

Chanzo: WebMD, ResearchGate

Soma pia:Mambo Ya Kufanya Unapo Tatizika Kupata Usingizi Usiku

Written by

Risper Nyakio