Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Mama Aliye Choka Amlalia Mtoto Kwa Bahati Mbaya Na Kusababisha Kifo Chake

3 min read
Mama Aliye Choka Amlalia Mtoto Kwa Bahati Mbaya Na Kusababisha Kifo ChakeMama Aliye Choka Amlalia Mtoto Kwa Bahati Mbaya Na Kusababisha Kifo Chake

Kisa cha mtoto aliye laliwa kwa bahati mbaya na mama na kuaga dunia kimeibua shaka nyingi kuhusu ushauri ambao mama hupata. Soma zaidi kuhusu kisa hiki.

Kifo cha mtoto aliye laliwa kwa bahati mbaya na mama wakati ambapo alikuwa ana nyonyeshwa kimefanya wakunga waulize maswali kuhusu ushauri wa kunyonyesha ambao wazazi hupata.

Baada ya uchungu wa uzazi mrefu na wa kuchosha, mama wa mara ya kwanza Ann Bradley alikuwa ana tatizika kumnyonyesha mtoto wake mchanga. Baada ya kuona alivyo kuwa akitatizika, madaktari walimweleza kuwa ni sawa kunyonyesha mtoto wake akiwa kitandani.

Daktari huyo alizidi kumfunza Ann mbinu ya kunyonyesha akiwa amelala kwa upande. Kabla ya kutoka, alimweleza kuhusu usalama wa kitandani na kwa nini kutumia kitanda kimoja na mtoto haku shauriwi ili mama huyu afahamu hatari.

Kwa huzuni, Ann alipo amka asubuhi, alipata mtoto wake bila uhai.

Rambi Rambi zetu kama Africaparent kwa Ann na familia yake kufuatia kumpoteza kijana wao. Tuna elewa jinsi uchungu wa uzazi na kujifungua kunachosha, na kuwa ajali kama hizi hutendeka, na sio lawama ya mtu yeyote.

Mtoto aliye laliwa kwa bahati mbaya na mama- kisa ambacho kinge epukika

importance of a bedtime routine

Wakati ambapo watu huenda wakawa na haraka kumlaumu mama kwa kumlalia mtoto na kusababisha kifo chake, John Pollard alikuwa na mtazamo tofauti.

Baada ya ajali hii ya kuhuzunisha, aliiandikia hospitali kuibua shaka kuhusu ushauri ambao wakunga huwapatia mama. Hakubaliani kuwa mama aliye jifungua anapaswa kubaki peke yake kitandani na mtoto mchanga, hasa akiwa amechoka kutokana na uchungu wa uzazi wa muda mrefu.

Kifo cha mtoto huyu ni jambo ambalo lingeweza kuepukwa. Lakini kwa huzuni nyingi, alikufa kwa sababu ya vitu vingi, kama bronchopneumonia ambayo haikuwa ime dhibitika na kufungana kwa mfumo wa kupumua.

Unapaswa kunyonyesha kitandani ama la?

Kwa wamama wengi, kunyonyesha kitandani kumesaidia pakubwa hasa kunapofanywa kwa njia inayofaa. Kuna saidia utoaji wa maziwa na kudhibiti viwango vyake mtoto wako anapokuwa karibu. Pia, unaweza kulala vya kutosha na mwanao pia atahisi salama.

Lakini sehemu muhimu zaidi ya kunyonyesha mtoto wako kitandani ama la ni kufahamu kuwa unapaswa kufanya uamuzi wenye maarifa.

Ikiwa ume amua kunyonyesha kitandani, fanya juhudi za kufanya kitendo hiki kwa usalama iwezekanavyo.

Hapa kuna vitu muhimu mnavyo paswa kutimiza kama mama na mtoto kabla ya kunyonyesha kwa kitanda:

Mama Aliye Choka Amlalia Mtoto Kwa Bahati Mbaya Na Kusababisha Kifo Chake

Kwa wamama:

  • Unahitaji kuwa hauvuti sigara kwa sasa na hata wakati wa ujauzito
  • Pia, unahitaji kuwa hauchukui dawa za kulevya, pombe ama dawa zinazo kufanya ulale. Usiwahi nyonyesha ukiwa umechoka
  • Ikiwa una nywele ndefu sana, zifunge ili zisi shike mtoto kwenye shingo
  • Mzazi ambaye hulala usingizi mrefu ama mwenye uzito mwingi wa mwili anapaswa kuepuka kunyonyesha akiwa amelala
  • Hakuna mtoto mwingine anaye paswa kuwa kitandani

Kwa watoto:

  • Watoto wanapaswa kuwa na nguvu, sio wagonjwa, wala walio zaliwa na uzani mdogo ama walio zaliwa kabla ya kukomaa
  • Hakuna mavazi ya kulala yenye nyuzi ama za kufungwa

Mama, tuna waletea hadithi kama hizi sio kwa nia ya kukuepusha kulala huku ukinyonyesha ama kulala na mtoto. Badala yake, kukujuza hatari zake na ili kuhakikisha usalama kwako na mtoto wako huku ukiendelea kunyonyesha na kulala kitandani kimoja naye.

Chochote unacho amua kufanya, hakikisha kuwa unafanya juhudi za kuhakikisha kuwa umepatia usalama kipau mbele kupunguza hatari zozote.

Vyanzo: Kellymom, The Sun

Soma Pia:Baba Kuwasomea Watoto Hadithi Za Wakati Wa Kulala: Kwa Nini Ni Bora Kwa Ukuaji Wa Mtoto Wako!

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Parenting
  • /
  • Mama Aliye Choka Amlalia Mtoto Kwa Bahati Mbaya Na Kusababisha Kifo Chake
Share:
  • Vipimo Rahisi Vya Mimba Vya Kinyumbani Visivyo Hitaji Fedha

    Vipimo Rahisi Vya Mimba Vya Kinyumbani Visivyo Hitaji Fedha

  • Jinsi Ya Kufanya Kipimo Cha Mimba Kwa Usahihi

    Jinsi Ya Kufanya Kipimo Cha Mimba Kwa Usahihi

  • Mimba Ya Bahati Mbaya Ama Usiyo Tarajia: Huenda Likakufanyikia

    Mimba Ya Bahati Mbaya Ama Usiyo Tarajia: Huenda Likakufanyikia

  • Huzuni Nyingi Baada Ya Kijana Wa Miaka 15 Kuwapatia Wasichana 16 Mimba

    Huzuni Nyingi Baada Ya Kijana Wa Miaka 15 Kuwapatia Wasichana 16 Mimba

  • Vipimo Rahisi Vya Mimba Vya Kinyumbani Visivyo Hitaji Fedha

    Vipimo Rahisi Vya Mimba Vya Kinyumbani Visivyo Hitaji Fedha

  • Jinsi Ya Kufanya Kipimo Cha Mimba Kwa Usahihi

    Jinsi Ya Kufanya Kipimo Cha Mimba Kwa Usahihi

  • Mimba Ya Bahati Mbaya Ama Usiyo Tarajia: Huenda Likakufanyikia

    Mimba Ya Bahati Mbaya Ama Usiyo Tarajia: Huenda Likakufanyikia

  • Huzuni Nyingi Baada Ya Kijana Wa Miaka 15 Kuwapatia Wasichana 16 Mimba

    Huzuni Nyingi Baada Ya Kijana Wa Miaka 15 Kuwapatia Wasichana 16 Mimba

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it