Je, Nifanyeje? Mtoto Wangu Anampenda Mfanyakazi Wangu Zaidi!

Je, Nifanyeje? Mtoto Wangu Anampenda Mfanyakazi Wangu Zaidi!

Ni rahisi kwa mtoto anaye baki na mfanyakazi kila siku kumzoea zaidi na kuwa na uhusiano wa karibu naye kuliko anavyo kuwa na mamake mzazi. Ila hili halifai kuwa jambo la kumhuzunisha mama.

Je, nifanyeje iwapo mtoto wangu anampenda mfanyakazi zaidi ya anipendavyo? Ni mtanziko na jambo la wasi wasi linalo wa kumba wa mama wengi. “Inafaa nimkubalie mtoto kuwa karibu sana na mfanyakazi?” “Mtoto amekua na uhusiano wa karibu na mfanya kazi, je nifanyeje,” ama pia, “mtoto wangu anampenda mfanya kazi zaidi yangu!” Haya ni baadhi ya maswali na wasi wasi unao ibuka miongoni mwa akili zetu zisizo na usalama.

Mama kutoka nchi ya Singapore, Biddy Low, pia aliye pokea mawaidha mengi kuhusu suala hili alipo jifungua mtoto wake wa kike kwa jina Talia.

 

Marafiki walimpa mawaidha na kumpendekezea kuwa hastahili kumkubalisha kuwa huru sana na mfanya kazi.

Mawaidha mengine yalikuwa ya kugusia kwa ujuu na kupendekeza kuwa yeye binafsi ndiye aliye paswa kumuosha na kumpikia mwanawe. Ushauri mwengine ulikua wa undani na kupendekeza kumfunza bintiye kumwagiza mfanyikazi ili mtoto ajue kuwa mfanyakazi sio mmoja wa familia.

Walimuonya kuwa kama hangefuata ushauri, “Mtoto wangu angekua karibu na mfanya kazi zaidi ya vile alivyo kwangu, na cha kuhuzunisha zaidi, angemuita mama na wala sio mimi.”

Wakati huu ambapo bintiye amekua wa umri, huku nchini ya Singapore ninapo ishi, wa mama wanali angazia tatizo hili.

 

“Mtoto kuskizana zaidi na mfanya kazi, nifanyeje?”

Soma jibu hili la mama kutoka nchi ya Singapore

Katika makala yake kwenye mtandao wa facebook, Mummy Biddy ana taja kila ushauri alioupata kuhusu kupambana na uhusiano kati ya bintiye na mfanya kazi na kusema anavyo hisi kuhusu ushauri huo kwa sasa. Haya ni majibu yake:

  1. Mtoto wako anapaswa kukupenda wewe pekee na familia yako.”

Mtoto wangu ana mapenzi ya kutosha ya kumpa yeyote anaye mpenda. Na pia yeyote yule anaye ipenda na kuitunza familia yake.

  1. Itakuwaje iwapo atamwita mfanya kazi mama?

Yeye ni mtoto. Anamwita babake “mama” na pia anafikiria upepo una uhai. Sio jambo kubwa vile kwa mtoto mchanga kuyatumia maneno kiholela holela.

Nina weza kuwa na tatizo iwapo anataka kuondoka kwangu na kutunzwa na mtu mwingine anaye faa kuniliko, lakini kabla ya hilo kutendeka, sina shida anapokuwa na matatizo la kuwatambulisha watu.

 

  • Mfanyakazi si miongoni mwa familia na mtoto anafaa kuelewa hilo.

 

Nafikiria kujaza akili za mtoto mchanga na mawazo ya ki tamaduni, na hadhi za kifamilia katika nyumbani mwao ni mbaya zaidi kuliko kumwita mama. Kwa hivyo mtoto hafai kumpenda mfanyakazi zaidi ya ampendavyo mzazi wake.

 

Nina shukrani kwa usaidizi ninao weza kupata, na ninaonyesha furaha yangu kwa vitendo. Nina taka mtoto wangu kumuona mfanyakazi kama familia kwani, anapo ishi nasi, yeye ni mmoja wetu.

 

  • Mtoto wako anapaswa kumpenda mamake peke yake.

 

Nafikiria kuwa mtoto anahitaji zaidi yangu ili kuwa na maisha mema. Kwa lolote lile, niko sawa kuwa miongoni mwa watu kumi bora maishani mwake. Sawa Liao.

“Talia Talia, sitaki kukupa upendo ambao hakuna mwengine yule anaye weza kukupa. Kwa sababu nita aga dunia kabla yako. Kutaendaje baada ya hapo?

Ninacho kutakia ni uwe na uwezo wa kupeana na kupokea upendo zaidi ya ule babako nami tunao kupa. Na uendelee kujenga jina na urithi tunao utengeneza pamoja.

Majibu yake ni ya kupendeza na kufurahisha kwa kweli.

Wa mama wapendwa, acha kuwa na hofu kuwa mtoto wako atakuwa na ushirikiano wa karibu na mfanya kazi wako. Ni ishara kuwa anamchunga ipasavyo. Una bahati kuwa wakati ukiwadia na hutakuwa tena, atakuwa mikono mizuri na kuwa mwanao ako salama na anapendwa hata usipo kuwa karibu. Sio jambo mbaya iwapo mtoto wako anampenda mfanyakazi wako zaidi.

Furahia mtoto wako kwa kuweza kuwa na uhusiano mzuri na watu wazima wengi maishani mwake, huenda ikawa ni wazazi wake, ndugu zake, babu zake ama wafanya kazi. Ina ashiria kuwa ni mtoto mwenye mapenzi na anaye pendeza kwa watu.

 

Read Also: Sex Education: Helping Your Kids Through Their Adolescence

 

Written by

Risper Nyakio