Mtoto Mchanga Anapaswa Kuoshwa Mara Ngapi?

Mtoto Mchanga Anapaswa Kuoshwa Mara Ngapi?

Swali la mara unazo paswa kumsafisha mtoto huwa uamuzi wa mzazi. Kulingana na hali ya anga ya mahali unako ishi.

Mara ambazo mtoto mchanga anapaswa kuoshwa ni uamuazi wa mzazi. Kuna watoto wengi ambao wanapenda kuwa kwenye maji. Na kumuosha mtoto wako kunaweza kuwa jambo lenye furaha na la kukupumzisha. Haina maana kuwa unapaswa kumsafisha mtoto wako kila siku. Ikiwa mtoto wako ni mchanga, kumsafisha mara mbili ama tatu kwa wiki kuna tosha kuhakikisha kuwa ni msafi. Ni vyema kukumbuka kuwa ikiwa unaishi mahali ambapo maji ni ngumu, maji nyingi ya mfereji yanaweza kausha na kuharibu ngozi ya mtoto wako. Kwa hivyo uamuzi ni upi? Mtoto mchanga anapaswa kuoshwa mara ngapi?

mtoto anapaswa kuoshwa mara ngapi

Mara unazo paswa kumsafisha mtoto changa. Wataalum wa ugenini wanasema kuwa kumsafisha mtoto mara tatu kwa wiki kumetosha mtoto kuwa safi wiki yote. Lakini hatuna uhakika kuwa waliangalia hali ya anga ya Afrika walipo sema hayo.

Kwa kuyasema hayo, ugumu wa sabuni na maji ngumu yanaweza kausha ngozi ya mtoto wako. Hiki ni kitu usicho taka kitendeke. Kwa hivyo, ni mara ngapi unazo paswa kumsafisha mtoto wako? Huo ni uamuzi wako kama mzazi! Ikiwa unaona ugumu kufanya uamuzi huo, wasiliana na daktari wako akusaidie kujua mara sawa kumsafisha mtoto wako. Tuna angazia jinsi ya kujua wakati ambao haumsafishi mtoto vizuri.

Mtoto mchanga anapaswa kuoshwa mara ngapi: Wakati ambapo hamsafishi mtoto wako inavyo faa

Kuweka mtoto akiwa msafi wakati wote huenda kukawa changamoto kwa wazazi wa mara ya kwanza. Hapa kuna njia 6 za kujua usipo msafisha mtoto vizuri. Fahamu makosa ya kawaida ambayo wamama hufanya wanapo wasafisha watoto wao. Epuka makosa haya na uhakikishe kuwa mtoto wako ana afya na ni msafi.

Kuoga mara kwa mara

Watoto wachang hawafanyi vitu vingi mchana, kwa hivyo hawahitaji kuoga mwili wote kila siku. Kumsafisha mtoto mchanga mara kwa mara kunaweza sababisha ngozi kukauka sana. Kumsafisha mwili wote mara mbili kwa wiki kumewatosha watoto wadogo, lakini hakikisha kuwa sehemu muhimu zina oshwa kila siku. Kumpanguza kwa kutumia maji ya vuguvugu na pamba kuhakikisha kuwa uso na sehemu ya chini ni safi ni wazo bora.

Kuto safisha sehemu ambazo ngozi ime jikunja

Ni muhimu kuhakikisha kuwa ngozi iliyo jikunja ya mtoto ni safi na imekauka, kuepuka uwezekano wa kupata maambukizi. Huenda ikawa vigumu kuweka sehemu hizi zikiwa safi hasa pale ambapo mtoto anaendelea kuwa mnene. Kuwa makini zaidi kwenye sehemu chini ya shingo, maziwa yanaweza mwagikia sehemu hiyo unapo mnyonyesha.

Kutumia bidhaa nyingi

Watoto wachanga huwa na ngozi laini ambayo ni rahisi kuathiriwa na bidhaa za kusafisha zilizo na harufu. Wazazi wanashauriwa kutumia maji peke yake kusafisha mtoto kwa miezi mingi ya kwanza. Ukiamua kutumia shampoo na sabuni kumsafisha mtoto wako, chagua sabuni zilizo tengenezwa za watoto wadogo ambazo hazina harufu. Chagua sabuni asili, kwa mfano za lavender ni bora kutumia wakati wa kulala kumsaidia mtoto kupumzika.

Kuto tunza kitovu inavyo faa

Kutunza kitovuhadi kianguke ni jambo ambalo huwatia uwoga wazazi wengi. Walakini, kutunza sehemu hiyo ni kazi rahisi. Ni vyema kuepuka kuosha watoto wachanga hadi kitovu kianguke, kwa sababu kinapaswa kuwa kimekauka vingi iwezekanavyo. Angalia sehemu hiyo kila siku kwa ishara za kuambukizwa, ambazo ni kama vile, sehemu hiyo kuwa nyekundu, kuwa na harufu mbaya ama povu kutoka kwenye sehemu hiyo. Pia, hakikisha kuwa unapo mvalisha mtoto wako kuwa diaper haigusi kitovu chake kilicho fungwa, na uhakikishe nguo unazo mvalisha hazija mshika na ana starehe zake. Baada ya kitovu kuanguka, mara nyingi baada ya wiki mbili baada ya kuzaliwa, unaweza safisha kitovu na uhakikishe ni kisafi kama sehemu yoyote ile ya mwili.

usafi wa genitali kwa watoto

Kutumia maji yaliyo moto sana

Kuchomeka mtoto akioshwa ni sababu ya kawaida ya majeraha katika watoto. Ni jambo nzuri kuweka kipima joto cha kuoga kwenye bafu unapo msafisha mtoto ambacho hubadili rangi kuonyesha iwapo maji yana temprecha nzuri kumsafisha mtoto ama la. Angalia temprecha ya maji kwa kutumia kiwiko- haipaswi kuwa na joto sana, mbali ya vuguvu. Yasiwe baridi sana kwani huenda mtoto akapata homa ama kuanza kukohoa.

Kuto tayarisha kumsafisha vya kutosha

Ni muhimu kuhakikisha kuwa una kila kitu unacho hitaji cha kumsafisha mtoto kabla ya kumweka kwenye karai ya kumsafisha. Watoto wanaweza zama kwenye hata maji yasiyo mengi, kwa hivyo hawawezi wachwa hata kwa sekunde peke yao ukichukua kitu ulicho sahau. Hakikisha kuwa una taulo ya ziada unapo msafisha mtoto, ikiwa kuna ajali ambayo huenda ikafanyika mkivalia nguo. Kwa sababu hiyo, ni vyema pia kuwa na diapers zaidi na nguo za zaidi unapo mvalisha nguo.

Baadhi ya wazazi wanapenda kutumia kiti cha kuoga kuwacha mikono yote iwe huru kumsafisha mtoto. Hili ni wazo bora, lakini ni muhimu kukumbuka kuwa mtoto huyo bado anahitaji kuangaliwa wakati wote anapo tumia mojawapo ya viti hivi. Ni matumaini yetu kuwa makala haya yata kusaidia kujua mara unazo paswa kuosha mtoto mchanga. Fuata vidokezo tulivyo angazia na pia uhakikishe kuwa unamsafisha mtoto wako kwa njia inayo faa bila kuwacha sehemu muhimu. Pia hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako mara kwa mara ikiwa una maswali.

Kumbukumbu: Web MD

Soma pia: Je, Ungependa Usaidizi Wa Kupanga Ratiba Ya Lishe Ya Wiki Moja?

Written by

Risper Nyakio