Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Je, Mtoto Hulia Akiwa Tumboni Mwa Mama Katika Mimba?

2 min read
Je, Mtoto Hulia Akiwa Tumboni Mwa Mama Katika Mimba?Je, Mtoto Hulia Akiwa Tumboni Mwa Mama Katika Mimba?

Watoto hulia wakiwa tumboni mwa mama ila mama hawezi kusikia. Hata ingawa mtoto hulia tumboni huwa hatoi machozi anapolia hadi anapofikisha wiki nne baada ya kuzaliwa.

Katika mwanzo wa muhula wa pili wa ujauzito, mwanamke huenda akaanza kuhisi mtoto akicheza tumboni, kubingirika, na kurusha mateke. Lakini je, mtoto hulia tumboni? Hata kama wanawake wengi wajawazito hawahisi mwendo huu, utafiti una pendekeza kuwa mtoto huanza kulia tumboni muda kabla ya kuzaliwa. Kana kwamba anajitayarisha kwa hatua kubwa ya kuzaliwa.

Mtoto hulia tumbo? Sayansi ina haya ya kusema

mtoto hulia tumboni

Uzinduzi na ukuaji wa teknolojia za kisasa katika nyanja ya afya unatuwezesha kuweza kuangalia kinachoendelea kwenye uterasi na jinsi ambavyo fetusi inakua. Katika baadhi ya video na picha za uterasi, uso wa mtoto anayelia umeonekana. Baada ya watafiti kutumia sauti ya juu kuona jinsi ambavyo fetusi itakavyofanya. Mama anapokuwa kwenye mazingira yenye kelele nyingi, fetusi hutoa sauti kubwa inayodhihirisha kukosa starehe.

Utafiti zaidi uliofanyika na timu ya Reissland, iliyoangalia kwa umakini mwendo wa fetusi katika muhula wa pili na wa tatu kupitia kwa vipimo vya ultrasound kuona usemi wa usoni. Wa kulia na kucheka kudhihirisha kuwa usemi wa usoni unaonekana baada ya mtoto kuzaliwa huanzia mtoto angali tumboni.

mtoto hulia tumboni

Mama hawezi kusikia mtoto anapolia kwani amezingirwa na amniotic fluid. Hakuna ushahidi bayana kuwa kulia kwa fetusi kuna sababishwa na uchungu na kukosa starehe. Kulingana na watafiti, usemi wa uso wa fetusi unawasaidia kufahamu matatizo ya kiafya ambayo mtoto anaweza kuwa nayo akiwa tumbo. Usemi wa uso ni muhimu kwani unasaidia katika utangamano wa mtoto na mazingira yake baada ya kuzaliwa. Mtoto anapolia baada ya kuzaliwa, mama anafahamu kuwa kuna kasoro mahali.

Hata hivyo, usemi wa usoni katika watoto hukomaa baada ya kuzaliwa na kuanza kuingiliana na watu. Watoto huanza kutabasamu na watu wanapofikisha umri wa miezi 8. Na kicheko cha kitoto katika miezi mitano, lakini nyuso hizi huanza kukua wangali tumboni mwa mama. Hata ingawa mtoto hulia tumboni, huwa hatoi machozi anapolia  hadi anapofikisha wiki nne baada ya kuzaliwa.

Soma Pia: Vidokezo 5 Vya Kupata Mimba: Kuongeza Nafasi Za Kupata Mtoto Kirahisi

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Je, Mtoto Hulia Akiwa Tumboni Mwa Mama Katika Mimba?
Share:
  • Majina 50 ya Wasichana ya Kipekee na Yanayopendeza Zaidi

    Majina 50 ya Wasichana ya Kipekee na Yanayopendeza Zaidi

  • Sababu 3 Kuu Za Maumivu Ya Tumbo Katika Mimba

    Sababu 3 Kuu Za Maumivu Ya Tumbo Katika Mimba

  • Ukweli Kuhusu Kufanya Mapenzi Ukiwa Na Mimba

    Ukweli Kuhusu Kufanya Mapenzi Ukiwa Na Mimba

  • Majina 50 ya Wasichana ya Kipekee na Yanayopendeza Zaidi

    Majina 50 ya Wasichana ya Kipekee na Yanayopendeza Zaidi

  • Sababu 3 Kuu Za Maumivu Ya Tumbo Katika Mimba

    Sababu 3 Kuu Za Maumivu Ya Tumbo Katika Mimba

  • Ukweli Kuhusu Kufanya Mapenzi Ukiwa Na Mimba

    Ukweli Kuhusu Kufanya Mapenzi Ukiwa Na Mimba

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it