Mambo 6 Muhimu Mama Wote Wanapaswa Kufahamu Kabla Ya Kuwaanzishia Watoto Chakul Kigumu

Mambo 6 Muhimu Mama Wote Wanapaswa Kufahamu Kabla Ya Kuwaanzishia Watoto Chakul Kigumu

Mtoto mchanga anapo jaribu kufikia chakula unacho kula ni ishara kuwa ako tayari kuanza kula vyakula vigumu.

Mama, huenda ikawa mtoto wako aliye kuwa ametulia hapo awali ameanza kunyoosha mikono mnapo anza kula chakula? Huenda hii ikawa ni ishara kuwa mtoto ako tayari kuanza kula chakula.

Inaonekana kana kwamba mtoto wako ana hamu ya chakula mnacho kila na wana jamii wengine. Anakutumia ishara kuwa maziwa ya mama pekee haya toshi.

Hata baada ya mtoto wako kuonyesha hamu yake mpya, mwaka ujao wa maisha yako utakuwa wa kuchosha na wa kufahamu mambo mapya ukibadilika kutoka kwa maziwa ya mama na kula vyakula vigumu.

1. Jambo la kwanza, mtoto kuanza kula chakula kigumu kuna ishara, na wakati bora!

Mambo 6 Muhimu Mama Wote Wanapaswa Kufahamu Kabla Ya Kuwaanzishia Watoto Chakul Kigumu

Kumwanzishia mtoto chakula kwenye lishe yake huanza akiwa na miezi 6. Chakula tofauti na maziwa ya mama. Kuanza kumlisha mtoto maziwa ya ng'ombe inapaswa kuanza baada ya mtoto wako kufika mwaka mmoja.

Wataalum wengi wanasema kuwa wakati bora wa kumwanzishia mtoto chakula kigumu ni kati ya miezi minne na saba.

Mtoto wako kujaribu kufikia chakula chako unapo kula ni ishara kuwa ako tayari kula chakula kigumu. Kabla ya kumwanzishia mwanao chakula kigumu, anapaswa kuwa na uwezo wa kukaa chini bila usaidizi, kupoteza tabia ya kutoa ulimi nje kumsaidia kunyonya chupa ama chuchu na kuweza kushika chakula peke yake.

Kama mtoto wako anafanya vyote hivi kwa urahisi, ako tayari kuanza safari hii mpya ya maisha yake. Kumwanzishia mtoto chakula kigumu kunaweza fanywa kwa njia mbili. Mtoto kuanza, pale ambapo ana jilisha ama njia ya kitamaduni ambapo analishwa kwa kijiko vyakula kama uji.

2. Unamlisha mtoto nini anapokuwa tayari?

Baada ya kusoma makala mengi kuhusu jinsi ya kumwanzishia mtoto chakula kigumu kupata jibu linalo faa kwa swali lako huenda likakutatiza. Unapaswa kuongea na daktari wa mtoto wako kuamua kilicho bora kwa mtoto wako. Haya ndiyo unayofaa kujua kabla ya kuanzia.

Unapo tayarisha orodha ya vyakula vya kumnunulia mwanao, zingatia kununua vyakula vilivyo na wingi wa protini, iron ili kumwongezea iron mwilini. Pia, chakula chake kinapaswa kuwa na wingi wa vitamini C kusaidia mwili wa mtoto kutumia iron anayo pata.

Kwa iron na protini, mpe mtoto wako mboga za kijani, kama vile mchicha na broccoli Pia, hakikisha kuwa unamlisha mayai, nyama, lentils na nafaka za mchele. Jaribu matunda tofauti kama vile mandizi, tufaha, na beets. Viazi vitamu, maharagwe ya kijani, zucchini na karoti.

3. Vyakula vya kuepuka katika kipindi hiki

Mambo 6 Muhimu Mama Wote Wanapaswa Kufahamu Kabla Ya Kuwaanzishia Watoto Chakul Kigumu

Unapo mwanzishia mtoto chakula kigumu, una shauriwa kuepuka asali, njugu na zabibu. Asali huenda ikawa na vitu vya kuhatarisha afya ya mtoto na inapaswa kutengwa kwa miaka ya kwanza michache.

Zabibu na njugu ama matunda magumu ama ya umbo la duara huenda yakam kaba koo. Lakini njugu zina wingi wa virutubisho kwa hivyo unaweza mpa zikiwa kama poda. Kuwa mwangalifu kuona kama ana mzio kwa vyakula unavyo mwanzishia.

4. Mpe mtoto wako anuwai ya kuchagua

Kumwanzishia mtoto wako vyakula vingi tofauti angali mchanga kunasaidia kuhimiza ulaji wenye afya na kuepuka watoto wanao chagua vyakula. Kwa hivyo, usimkubalishe kula chakula anacho kipenda tu!

Hayo yakiwa yame semwa, ni muhimu kumwanzishia vyakula vipya kila chakula katika wakati wake ili uweze kuona matokeo yoyote ya mzio kwa chakula fulani.

5. Kuongezea maziwa kwa chakula kigumu

Mambo 6 Muhimu Mama Wote Wanapaswa Kufahamu Kabla Ya Kuwaanzishia Watoto Chakul Kigumu

Katika miezi ya kwanza ya kumlisha chakula kigumu, unahitajika kuongeza maziwa ya mama kwenye chakula cha mtoto. Unapo tayarisha lishe zake, tia akilini viwango vya maziwa na vya chakula kigumu anacho kila. Kama sharti la kijumla, watoto wa miezi 6-12 wanaweza kunywa 500-750 ml za maziwa kila siku.

6. Kubadilisha kutoka kwa maziwa ya mama hadi kwa maziwa ya ng'ombe/freshi ama ya UHT

Maziwa ya ng'ombe haya shauriwi hadi pale ambapo mtoto anafikisha mwaka mmoja kwa sababu itakuwa vigumu zaidi kuya chakata na huenda yaka sababisha shinikizo kwenye maini ya mtoto wako ambayo bado hayaja komaa.

Hayana virutubisho vyote vinavyo hitajika kama vile iron na vitamini C, na huenda mtoto wako akawa na ukosefu wa iron mwilini. Lakini punde tu mtoto wako anapo fikisha mwaka mmoja, na anapata lishe iliyo sawasishwa, unaweza anza kumpa maziwa ya ng'ombe.

Kumbuka vidokezo hivi unapo mwanzishia mtoto wako maziwa ya ng'ombe.

  • Itachukua muda kwa mwanao kuzoea maziwa ya ng'ombe kwani formula ina ladha zaidi.
  • Njia nyingine ya kufanya mabadiliko haya yawe rahisi zaidi ni kwa kuwafanya wawe na furaha ya kunywa maziwa. Kwa mfano, nunua kikombe spesheli ambacho watakuwa wanatumia kunywa maziwa na uwaonyeshe jinsi inavyo sisimua kutumia kikombe hicho!
  • Pia, ni vyema kupasha joto maziwa kabla ya kumpa mwanao. Ikiwa ulikuwa ume yahifadhi kwenye friji, yatakuwa na baridi zaidi ikilinganishwa na maziwa ya formula ama maziwa ya mama.
  • Unapo mwanzishia maziwa freshi, hakikisha kuwa anakula vyakula kutoka familia zote, mboga, nafaka, matunda na nyama.
  • Usisahau kuwapa Vitamini D kwani watoto katika umri huu watahitaji kiwango zaidi cha ufuta.

Huo ni ujumbe mwingi, wote ambao unapaswa kuweka akilini na kukumbuka baada ya mtoto wako kuanza kula chakula. Lakini usiwe na shaka, kwani mara tu unapo anza kumlisha mtoto wako chakula kigumu, yote mengine yatafuata kwa njia asili na kwa urahisi. Na kuzidisha utangamano kati yako na mtoto wako mchanga.

Vyanzo: Common Weaning Concerns

Why Formula Instead of Cow's Milk?

Soma Pia:Vyakula Vya Lactogeni Vya Kumsaidia Mama Kuongeza Maziwa

Written by

Risper Nyakio