Maana Na Sababu Za Mtoto Kujigonga Kichwa Kutumia Mikono

Maana Na Sababu Za Mtoto Kujigonga Kichwa Kutumia Mikono

Huenda mzazi akawa na shaka anapo gundua kuwa mtoto wake ana uraibu wa kujigonga kichwani, ila ni vyema kukumbuka kuwa ni hatua ya ukuaji.

Ni jukumu asili la mzazi kuwalinda watoto wake na atafanya kitu chochote kuhakikisha kuwa mtoto wake ako salama. Kabla ya kutoka hospitalini, wazazi wengi huhakikisha kuwa nyumba haina vitu ama vyombo ambavyo vinaweza kumdhuru mtoto. Na kueka vidoli vinavyo mfaa na kufanya juhudi zote kuhakikisha kuwa hakuna ajali ambayo huenda ikatokea mtoto anapo kuwa akitembea kwenye nyumba. Ila huenda ukaanza kugundua kuwa mtoto wako anajigongesha kichwa. Ni kipi kinacho sababisha mtoto kujigonga kichwa kutumia mikono.

mtoto kujigonga kichwa kutumia mikono

Huenda hata akawa ajigongesha kwenye kuta, sakafu ama kijitanda chake. Jambo hili litamtatiza mzazi yoyote kwani kwa umri huu, mtoto hawezi kuongea kusema kinacho msumbua. Na mzazi ataogopa kuwa huenda mtoto wake akajiumiza vibaya. Mtoto huenda akaanza tabia hii anapokuwa kati ya miezi mitano hadi tisa. Cha kushangaza ni kuwa watoto hawa huwa hawa gongeshi vichwa vyao kwenye vitu kama mito ama godoro, la ni kwa vitu vigumu.

Sababu kuu za mtoto kujigonga kichwa kutumia mikono ni kama vile:

Matatizo ya kulala. Kujigonga kichwa hata kama ni tabia isiyo tarajiwa kwa watoto, ni kawaida sana kwa watoto wadogo. Baadhi ya watoto hufanya hivi kabla ya kulala ama karibia wakati wao wa kulala, huonekana kama tabia ya kujituliza.

Hata kama ni kawaida kwa watoto, bado ni kitendo kinacho waliwaza wazazi wengi. Huku wengine wakilia wanapo jigongesha kichwa, wengine hutoa sauti. Wakati mwingi, kitendo hiki hakifai kukuliwaza sana.

Matatizo ya ukuaji. Huenda sababu ya mtoto kujigongesha ikawa kufuatia matatizo ya ukuaji kama vile autism ama changamoto zingine za kisaikolojia ama neva. Ili kubainisha kujigonga kichwa kwa kawaida na kwa matatizo ya ukuaji, tizama wakati anapo jigongesha kichwa na mara ngapi kwa siku. Iwapo mtoto wako ana afya na hana matatizo yoyote ya ukuaji na kujigongesha kichwa kuna tendeka dakika chache kabla alale, bila shaka huko ni kujigongesha kichwa kwa mwendo na haupaswi kuwa na shaka.

mtoto kujigonga kichwa kutumia mikono

Mambo ya kufanya unapogundua kuwa mtoto wako anajigonga kichwa kwa kutumia mkono.

  • Toa chombo ambacho huenda kikamwumiza anapo fanya hivyo.
  • Weka kijitanda cha mtoto mbali na ukuta, ili asijiumiza kwa ukuta.
  • Weka mito kwa kitanda cha mtoto ili kuhakikisha kuwa hajiumizi na mbao.
  • Ukigundua kuwa tabia hii haipungui ama kuisha, ni vyema kumwona daktari wenu.

Soma pia: Ni Kipi Kinacho Tendeka Mtoto Wako Anapo Kosa Mojawapo Ya Chanjo

Written by

Risper Nyakio