Njia 10 Bunifu Za Kusuluhisha Tatizo La Mtoto Anaye Kataa Chakula

Njia 10 Bunifu Za Kusuluhisha Tatizo La Mtoto Anaye Kataa Chakula

Wazazi wengi hukumbana na tatizo la watoto wadogo kukataa chakula ama kuchagua chakula watakacho kila. Ni vyema kwa wazazi kuwa wapole katika kipindi hiki.

Usikate tamaa kwa sababu mtoto wako anakataa kula chakula, ama anachagua chakula atakacho kila. Kuwa mvumilivu. Kuwafanya wapende chakula kinacho wafaa ni safari ndefu lakini ni muhimu kuisafiri ili kutatua tatizo la mtoto kukataa chakula.

Lisa Leake ambaye ni mwandishi wa kitabu bora zaidi cha siku 100 za chakula ana suluhu za kukusaidia kutatiza tatizo hili na kuwafanya watoto wako wafurahie chakula kilicho bora kwao.

1.Fanya mabadiliko madogo

vibanzi, chips

Badala ya kula vyakula vilivyo chakatwa, chagua vilivyo na afya zaidi. Lisa ana shauri kula vitu kama mandizi badala ya vibanzi vya mandizi.

2. Wape mtazamo wa kwanza wa kupendeza

Ikiwa ungependa wapende chakula kinacho wafaa, lazima uhakikishe kuwa unawaanzishia chakula vizuri. Kwa mfano, kaanga viazi vitamu kwenye mafuta ziwe vibanzi. Ama uongezee sauce ya siagi kwenye samaki. Watafurahia chakula hiki zaidi wakati ujao.

3. Waruhusu wachague viungo wanavyo taka

Wape uhuru wa kuchagua matunda na mboga mnapo enda kununua. Kwa njia hii, utam himiza mtoto anaye chagua chakula kula vyakula vyenye afya.

Ama, unaweza wafunza jinsi ya kukuza baadhi ya vyakula kama vile nyanya kwenye shamba iliyo nyumba ya jiko ama nyumba yenu.

4. Watunze watoto wako

Hii ni mojawapo ya njia bora za kuwa himiza watoto wale vyakula vyenye afya. Wanapo maliza kufanya kazi uliyo wapatia, wapongeze kwa kuwapatia tunda ama maziwa. Kwa njia hii, unawahimiza kula vitu vyenye afya na vitakavyo saidia miili yao ikilinganishwa na vitamu tamu vilivyo chakatwa.

5. Mtoto Kukataa Chakula: Kuwa wazi nao kuhusu 'kuficha mboga'

Kama mzazi mwingine yule, ni jambo la kawaida kuficha mboga kwenye chakula cha mtoto wako. Kwa sababu akiona mboga fulani ndani, huenda akakosa kula chakula hicho. Wajuze umuhimu wa kula mboga na wasio ogope kwani ni muhimu sana kwa afya yao.

6. Wahusishe katika mapishi

tofauti kati ya ulezi wa kiafrika na umarekani

Wafunze watoto wako wangali wachanga jinsi ya kushika mboga, kukupitishia unapo pika na kukusaidia na vitu vingine unapokuwa jikoni ukipika. Bila shaka wata kula kwa sababu walisaidia katika matayarisho.

7. Sharti la kuuma mara moja

Ikiwa mtoto wako anakataa chakula kipya, mwambie aonje mara moja kisha umwachilie aende akacheze. Hata anaweza kunywa maji ama maziwa baada ya kumeza.

8. Usiwape shinikizo sana

Hata kama huenda ikawa vigumu, jaribu usi sukume sana kula hadi pale wanapo chukia chakula hicho zaidi. Kuwasukuma sana kutabadili mtazamo wao wa chakula hicho kuwa hasi.

9. Waanzishie chakula kipya mara tofauti

Usiongeze vyakula vipya, vyote kwa pamoja. Hakikisha kuwa kila mara, unawapa chakula aina fulani. Kwa njia hii, utajua iwapo wana kifurahia ama la.

10. Dhibiti matarajio yako

Usi amini kuwa kuigeuza familia yako na watoto wako kupenda chakula chenye afya itakuwa rahisi. Lakini fanya juhudi za kujaribu. Kwa uvumilivu na kuto kata tamaa, utaanza kushuhudia matunda ya juhudi zako.

Soma Pia:Jinsi Ya Kutengeneza Chakula Chenye Afya Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja

 

Written by

Risper Nyakio