Kila mtu huogopa sindano na sio staajabu kumwona mtoto akilia baada ya chanjo. Ila watoto wanaweza kuwa hawana ufahamu ila tu baada ya kudungwa. Kuna mambo mengi ambayo yanaweza sababisha mtoto kulia baada ya chanjo.
Mtoto Kulia Baada Ya Chanjo

Mwanzo, chanjo ni dawa ya kibiolojia inayojenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani. Chanjo zimejulikana kama njia bora zaidi za kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Hii ndio njia mojawapo imetumika duniani kote kulinda watoto kutokana na maambukizi kwa kingamwili zao bado sio dhabiti. Pia chanjo zimepunguza vifo vya watoto kwa asilimia kubwa sana.
Ni vyema kukumbuka kuwa kinga kila wakati ni bora kuliko tiba. Ila, mbali na umuhimu wake chanjo pia huambatana na changamoto. Mojawapo ni mtoto kulia baada ya chanjo. Ni mambo yepi yanaweza kumsukuma mtoto kulia baada ya chanjo:
Kwanza kabisa ni uchungu. Kila mtu, mdogo kwa mkubwa huogopa sindano kwani ni chungu. Hii si tofauti kwa mtoto mdogo. Huu uchungu wakati mwingine huendelea ata baada ya sindano kuondolewa. Hivyo unaweza kupata mtoto wako analia ata baada ya sindano. Pia mahali alipodungwa hubaki uchungu kwa wakati. Hivyo ukishika mahali pale utapata mtoto analia.
Sababu nyingine ni kuwa chanjo zingine huweza kusababisha joto jingi mwilini. Kwa vile chanjo huwa sehemu ya vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani,wakati mwingine mwili wa mtoto unaweza pokea ile kingamwili kwa utofauti. Hili husababisha joto jingi mwilini mwa mtoto na kumfanya yule mtoto kulia. Ni bora kuzungumza na daktari wako iwapo mtoto anaanza kuwa na joto jingi.

Wakati mwingine chanjo ama kuwepo kitu mpya mwilini husababisha mwili wa mtoto kutokuwa sawa. Hili si kumaanisha kuwa mtoto anahisi uchungu ama yuko na joto . Mbali utendakazi wa ile dawa una sababisha mtoto kuhisi hayuko shwari. Huko kuhisi hayuko sawa kunaweza kusababisha mtoto kulia.
Pia inaweza kuwa tu sababu za kawaida kama vile njaa ama mtoto ameenda haja. Kwa kuwa njia kuu ya mtoto kujieleza huwa kulia, mzazi wakati mwingine anaweza dhani kuwa chanjo inamdhuru mtoto wake lakini la. Inaweza kuwa makali ya njaa inayomfanya mtoto kusumbua baada ya chanjo. Pia anaweza kuwa anahitaji kubadilishwa tundua.
Chanjo ni sehemu ya maisha ya mtoto na imesaidia kuzuia vifo vya watoto wengi kote duniani. Hakuna cha kueleza athari zingelikuwapo iwapo hakungekuwa na chanjo. Gharama ya matibabu na huzuni ya kuwa na mtoto magonjwa si jambo la furaha. Chanjo zimesaidia pakubwa hivyo changamoto ya mtoto kulia baada ya chanjo ni kitu cha kukubatiwa mbali si kugharibishwa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Mtoto Anapaswa Kupata Chanjo Zipi Angali Mchanga?