Najua kama wewe ni mzazi umekimbia kumtuliza mdogo wako baada ya kumsikia akilia ila ukampata bado amefumba macho. La kushangaza sana. Lakini hauko peke yako. Hili ni jambo ambalo hutokea kwa wakati mwingi sana. Ila kwa nini mtoto kulia usingizini?
Mtoto Kulia Usingizini

Kwa wakati mwingi mzazi anapopata mtoto analia kama bado yuko usingizini huwa hajui lakufanya. Hili tukio humwacha mzazi na maswali mengi kama vile iwapo mtoto anaota, yuko njaa ama anahisi vibaya. Na jinsi ya kumrejesha ili aendeleze usingizi. Kuelewa nini chanzo cha mtoto kulia usingizini itakusaidia wakati mwingine utajipata kwa hali hii.
Jambo la kwanza ni kuwa hili hutendeka wakati mtoto anapobadilisha kutoka kwa aina moja ya usingizi hadi nyingine. Kwa kawaida binadamu huwa na aina mbili za usingizi. Ulio mzito na usio mzito ila mtoto huchukua muda mrefu kwa usingizi usio mzito. Wanapobadilisha kutoka kwa usingizi mmoja hadi mwingine utapata wanalia.
Sababu nyingine kuu kwa nini mdogo wako anaweza kuwa analia kama bado yuko usingizini ni njaa. Mdogo wako huhitaji masaa mengi ya kula na wakati mwingine haya masaa huingiliana na masaa ya kulala. Iwapo atahisi njaa kwenye usingizi ataanza kulia. Hivyo kunyonya kutahakikisha kuwa amerudi usingizini wake.
Kulia kwenye usingizi pia ni ishara kuwa mtoto ana machovu mengi ama hapati usingizi wa kutosha. Kama tu mtu mzima, iwapo mtoto hana ratiba nzuri ya kulala anaweza kuwa na wakati mgumu kupata usingizi mzito. Hivi utamskia mdogo wako akilia usingizini. Hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata usingizi wa kutosha usiku na mchana. Pia ratiba itamwezesha kupata mapumziko ya kutosha.

Mdogo wako anaweza kuwa anaota meno. Meno huweza kuwasumbua watoto kwa wakati. Kwa vile hawawezi kuongea huzungumza kupitia kilio. Wakati mtoto anaota meno huwa hana starehe. Huku kusumbuka huweza kuwasilishwa kama kilio.
Sababu zingine zinaweza kuwa mtoto ana tundua chafu ama yuko na maumivu. Mtoto anapohisi hayuko sawa jambo la kwanza huwa kulia. Kama mzazi ni vyema kuhakikisha kuwa mahali mtoto anapolala ni pakavu na pia kubadilisha tundua mara anapoenda haja. Pia hakikisha mtoto hahisi joto nyingi. Haya mambo husababisha mtoto kulia usingizini.
Mtoto kulia usingizini huwa sio jambo la dharura. Ingawaje kila mzazi atakuwa na hofu mara ya kwanza, ama iwapo hana habari ya chanzo chake. Lakini ni matumaini yetu hili orodha litapunguza wasiwasi wakati mwingine mtoto atalia kwenye usingizi.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Mambo Ya Kufanya Unapo Tatizika Kupata Usingizi Usiku