Je, ni jambo la kawaida watoto wachanga kulia tumboni mwa mama yao?

Je, ni jambo la kawaida watoto wachanga kulia tumboni mwa mama yao?

Utafiti uliofanyika una ashiria kuwa watoto hulia tumboni mwa mama yao. Hii ni njia mojawapo ya kuwasiliana na watu kabla hawaja zaliwa. Mama anapo ongea na mtoto aliye tumboni pia anaweza kumsikia.

Mtoto wako mchanga huingia duniani akilia. Je, ni jambo la kawaida mtoto kulilia tumboni? Cha kuhuzunisha ni kwamba wao hulia kama utafiti unavyo onyesha. Usi huzunike sana mama, kwani unachohitaji kujua kwa sasa ni kuwa ni jambo la kawaida na sehemu ya ukuwaji wa mtoto wako.

 

Je watoto hulia tumboni? Wataalamu wanasemaje?

mtoto kulilia tumboni

Utafiti mpya uliofanyika katika vyuo vikuu vya Durham na Lancaster. Utafiti huu unaonyesha kuwa watoto wachanga huanza kukuza njia za kuwasiliana nasi wanapokuwa tumboni. Na wanaanza hivi kwa kulia. 

Utafiti huu ulitumia ultrasound na uka gundua nyuso za mtoto tumboni mwa mama. Wadogo hawa pia walionyeshana kukunja kwa mapua na wanja. Utafiti huu pia uli husisha kusoma video za 4D zilizo skaniwa za watoto 8 wa kike na 7 wa kiume tumboni.

 

Daktari Reissland ni mwalimu katika chuo kikuu cha Durham. Kulingana na yeye, kulia ina husika zaidi na akili kukua kuliko inavyo lingana na hisia. Ila utafiti zaidi Unahitajika kudhihirisha haya.

Anasema “Si baina ama mtoto anaweza hisi uchungu, na pia hatujui kama ishara za uso zinahusika na hisia zake. Ni muhimu kwa watoto kuweza kuashiria uchungu punde wanapo zaliwa ili waweze kuwasiliana wanapo hisi usumbufu wowote ule ama uchungu watakao uhisi kwa wanao wabeba.”

Walakini, kuna haja kufanya utafiti zaidi kujua uhusiano kati ya ishara za uso watoto wanapolia na kama wanahisi uchungu.

 

Mtoto kulilia tumboni?: Jinsi ya kuwasiliana na mtoto wako kabla kuzaliwa

Kuji husisha na mawasiliano na mdogo wako inaweza saidia kuskizana na mtoto wako kabla ya kuzaliwa kwake. Hizi ni baadhi ya njia za kuya fanya haya.

 

  1. Kusoma kwa sauti ama kumwongelesha mtoto wako ni njia rahisi ya kukuza mawasiliano ya moja kwa moja. Mtoto wako ataweza kukuskia mapema kutoka wiki 18 kama uwezo wao wa kuskia unakua kikawaida. Kuna uwezekano mkubwa kuwa anapozaliwa ataitambua sauti yako.
  2. Michezo ya kusisimua inayo husisha kujishughulisha kwa stimuli inaweza kuwa njia kuu ya kukuza uwasiliano. Unaweza jaribu kuliguza tumbo lako na ungoje uskie mtoto wako atakacho fanya. Wanaweza rusha mguu kufuatia guso lako. Daktari mstaafu wa wamama kutoka California, Daktari F. Renee Van de Carr anasema kuwa mtoto tumboni anasoma jinsi ya kujibu kwa stimuli tofauti tofauti. Ikiwemo guso.
  3. Muziki pia njia nyingine yenye ufanisi ya kuwasiliana na mtoto wako. Kucheza muziki uliotulia wenye upole inasaidia kuwasiliana na mtoto wako hadi utakapo urudia. Wataalamu wana elimisha kuwa watoto hupunguza wanacho fanya wanapo sikia muziki wa pole pole ila muziki wa sauti ya juu unawafanya kuongeza mipigo yao.

 

Written by

Risper Nyakio