Sababu Kwa Nini Mtoto Wako Huenda Akanyongwa Anapo Nyonya

Sababu Kwa Nini Mtoto Wako Huenda Akanyongwa Anapo Nyonya

Unapokuwa na utoaji mwingi wa maziwa ya mama, huenda mtoto wako akanyongwa na maziwa ya mama.

Mtoto wako hunyongwa na maziwa anapokunywa maziwa ya mama zaidi kwenye mdomo wake zaidi ya kiwango anacho weza kumeza. Kiwango kikubwa huenda kikapita kwa mfumo wa kupumua na kusababisha kunyongwa. Ni jambo la kuogofya kwa mama anapo ona mtoto wake akikohoa na kumwaga maziwa huku akiteseka kupumua. Walakini, kuelewa kwa nini inatendeka, kunawezekana kuepuka tatizo hili unapo mnyonyesha mtoto wako. Nini kinacho sababisha mtoto kunyongwa na maziwa?

Kwa Nini Mtoto Wako Hunyongwa Na Maziwa Anapo Nyonya

mtoto kunyongwa na maziwa

Wamama wengi huenda wakashangaa iwapo kuna uwezekano wa mtoto kunyongwa na maziwa? Bila shaka, wanaweza kwa hali tofauti na ni kawaida sana kuliko unavyo weza kudhani. Maziwa mengi na nafasi dhaifu za kunyonyesha ni mojawapo ya sababu kuu kwa nini watoto wengi hunyongwa wanapo nyonyeshwa. Hapa kuna njia mbili kwa nini hii hutendeka:

Utoaji zaidi wa maziwa

Iwapo baadhi ya wamama wanao nyonyesha huamua kuwa na maziwa zaidi ya mama kuliko kukosa ama kuwa na kiwango kidogo cha maziwa, kuna kutoridhika kwa mama na mtoto. Kuwa na kiwango kikubwa cha maziwa kuna maana kuwa lazima utafute nafasi tofauti za kumlisha mtoto wako.

Kutoa maziwa kwa nguvu

Utoaji zaidi wa maziwa pia hufanya utoaji mwingi wa maziwa katika wanawake walio na utoaji wa mbio wa maziwa. Maziwa yanayo toka kwenye chuchu kwa njia ya mbio na kwa nguvu. Angalia ishara hizi kwenye mtoto anapo nyonya:

 • Kunyongwa, kukohoa ama kupumua anapo nyonya
 • Kushika chuchu ili kupunguza utoaji wa maziwa
 • Kujitoa mbali na chuchu mara kwa mara
 • Kutema maziwa mara kwa mara
 • Kutoa sauti anapo nyonya
 • Kukataa kunyonya

Vitu vya kufanya mtoto wako anapo nyongwa na maziwa ukimnyonyesha?

Sababu Kwa Nini Mtoto Wako Huenda Akanyongwa Anapo Nyonya

 

Kuna mbinu za msaada wa kwanza zinazo saidia mtoto aliye nyongwa na maziwa ya mama. Kwa sababu watoto wana mili dhaifu, unapaswa kufanya hivi na tahadhari. Hapa kuna baadhi ya vidokezo wakati ambapo mtoto ananyongwa na maziwa:

 • Mchukue mtoto ukimsitiri kichwa na uweke mkono kwenye kifua chake, huku ukimsukuma mbele kwa upole. Wekelea ngumi kwenye kitovu chake, na mkono huo mwingine juu ya ngumi hiyo na uisukume ndani. Sukuma kwa mbio na kwa nguvu na kisha juu kidogo kwenye tumbo ya mtoto.
 • Mgeuze mtoto juu chini na upige kwa upole kwenye mgongo na kumsukuma kifua mbele na kumpapasa kwenye mgongo ili kufungua mfumo wa kupumua. Sukuma kifua kwa kutumia vidole viwili ama vitatu na uhakikishe kuwa unasitiri kichwa chake kutumia mkono huo mwingine. Endelea hadi aache kunyongwa.

Ni muhimu kujua kuwa iwapo mtoto haponi ama kuzirahi, anapaswa kupelekwa hospitalini bila kusita na kufanyiwa utaratibu unao faa.

Jinsi ya kuepuka mtoto kunyongwa na maziwa

mtoto kunyongwa na maziwa

Kuna njia nyingi ambazo unaweza tumia kudhibiti tatizo la utoaji zaidi wa maziwa kuepuka mtoto kunyongwa na maziwa. Hapa kuna vidokezo muhimu vya kuangazia:

 • Kupunguza utoaji wa maziwa ni njia njema ya kuanza, kwani kutoka kwa viwango vikubwa hutendeka panapokuwa na maziwa mengi kwenye chuchu. Unapokuwa ukinyonyesha kutoka upande mmoja, kwa mfano wa kushoto, kwa kutumia kiganja cha mkono wa kulia, finyilia chuchu ya upande wa kulia ndani na uhesabu hadi tano.
 • Kila mara unapo nyonyesha, tumia upande mmoja kila mara ila chuchu yako iishe maziwa na wapate maziwa yenye ufuta tosha ndiyo wahisi kushiba na waache kunyonya.
 • Hakikisha kuwa mtoto wako anaishikilia chuchu yako vizuri. Mtoto asiye ishikilia chuchu vyema kwa kutumia mdomo huenda aka nyongwa anapo nyonyesha. Maziwa yanayo paswa kwenda kwenye koo yake huenda yaka baki kwenye mdomo wake. Kunyonya vyema kutahakikisha kuwa maziwa yana pita vyema.
 • Utapata kuwa mbinu ya kumnyonyesha mtoto ukiwa ume mwinua inasaidia pakubwa. Maziwa yako lazima yawe dhidi ya msukumo wa chini na uepuke kuyamwaga. Mshike mtoto mikononi unapo kaa kwenye kiti.
 • Tumia mbinu ya chini kumlisha mtoto, inafanya kazi dhidi ya msukumo wa chini. Mama hulala chini kwa mgongo na mtoto juu yake, kwa njia ambayo tumbo ya mtoto inagusa ya mama. Usifanye hivi mara nyingi kwani inaweza athiri mishipi ya maziwa.
 • Kumshika kana kwamba mpira, unapo lala nyuma ni mbinu njema ya kunyonyesha, hasa unapokuwa nje na mtoto.
 • Chuchu nyingine isipokuwa na starehe, unaweza kamua maziwa na kisha uisugue kwa upole kupunguza kuhisi vibaya. Unapo endelea na utaratibu huu, kamua maziwa kidogo, hadi unapohisi yamepungua.

Epuka kuwanyonga watoto unapo wanyonyesha, chukua hatua za tahadhari kabla na unapo wanyonyesha.

Soma pia: Breast milk oversupply: Blessing or burden?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio