Utafiti: Mtoto Anapo Rusha Mateke Tumboni, Kitendo Hiki Kinamsaidia Kukua!

Utafiti: Mtoto Anapo Rusha Mateke Tumboni, Kitendo Hiki Kinamsaidia Kukua!

Je, mtoto anapo rusha mateke tumboni ni kipi kinacho endelea mwilini mwake? Tazama jinsi kitendo hiki kinavyo kuza ubongo wake!

Kuhisi mtoto wako akirusha mateke kwa mara ya kwanza tumboni ni hatua ya kufurahisha! Na kadri ujauzito wako unavyo zidi kukua, mateke hayo mepesi hubadilika kuwa ngumi na mateke ya nguvu. Mwendo huu baadhi ya wakati huenda ukawa wenye nguvu na kukuamsha usingizini! Je, ushawahi kujiuliza maana ya mtoto kurusha mateke tumboni na kunavyo athiri ukuaji wake?

Mtoto hai tumboni- Nisaidie!

mtoto hai tumboni

Ikiwa mtoto aliye na mwendo mwingi zaidi tumboni anaanza kukutia wasiwasi kuhusu kwa nini ana jikunja tumboni. Huenda ikawa majibu ya somo mpya yatakutuliza. Kurusha mateke hakumpi mtoto njia ya kujinyoosha ama kusema "habari" kwa dunia ya nje, kuna wasaidia kuunda na kutengeneza mifupa na misuli yao.

Kulingana na somo lililo chapishwa kwenye Makala ya Royal Society, kuhusu mwendo wa mtoto hai tumboni. Waligundua haya.

  • Katika wiki 20 hadi 30, mateke huongezeka. Kulingana na scan za MRI, kurusha mateke huongezeka mtoto anapo fikisha wiki 20 hadi 30.
  • Mateke hupunguka katika wiki 35. Watafiti waligundua kuwa mateke yalipunguka katika wiki 35 ya ujauzito. Kwa nini? Kwa sababu hakuna nafasi tosha ya mwendo na kurusha mateke tumboni.
  • Lakini shinikizo huzidi kuongezeka sawa na ukuaji. Walakini shinikizo kwenye misuli ya miguu ya mtoto na misuli huzidi kuongezeka. Na huku kunasaidia fetusi kukua.
  • Mwendo unasaidia watoto tumboni kukua. Somo hili lina sisitiza umuhimu wa mwendo unaofaa kuathiri ukuaji wa fetusi.
  • Jinsi mtoto anavyo songa tumboni kunaweza athiri afya yao wanapo kua. Utafiti zaidi unahitajika kupata picha wazi zaidi za uhusiano kati ya mwendo wa fetusi na afya ya mifupa baadaye maishani, kama vile osteoarthritis.

Je, unaweza chechemua mtoto kurusha mateke tumboni?

bei ya kipimo cha mimba

Kwa sasa kwani unafahamu kuwa mtoto hai tumboni ni kitu chanya. Unapaswa kufanya nini unapo hisi kuwa mtoto wako harushi mateke sana tumboni? Usiwe na shaka kwani mama anaye tarajia anaweza mhimiza mtoto wake kurusha mateke tumboni!

Unaweza jaribu haya:

  1. Lala chini

Unaweza lala kwa upande wako wa kushoto. Kuwa makini kwa hisia za mwendo wa mtoto wako kwa angalau masaa mawili. Unapaswa kuhisi mtoto wako akisonga angalau mara 10. La sivyo, wasiliana na daktari wako.

2. Kula ama ukunywe

Kunywa glasi ya sharubati ya manjano ama maziwa ili kumwamsha mtoto wako. Kutafanya mtoto wako awe na mwendo zaidi.

3. Sikiliza muziki

Kwa njia sawa unavyo weza kumlaza mtoto kutumia muziki, unaweza msisimua kwa chaguo lako la sauti. Wimbo sio lazima uwe na kelele nyingi, la hasha, ila sauti tosha ya kusisimua uwezo wao wa kusikia.

4. Pumua kwa nguvu

Pumzika mama! Kama tulivyo sema, mwendo wa fetusi hutofautiana kwa kila mama na kwa kila ujauzito. Kwa hivyo usiji shinikize kuhisi njia sawa na mama mwingine. Ila, usikawie kumwambia daktari wako kuhusu shaka zozote ulizo nazo.

Soma Pia: Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

Written by

Risper Nyakio