Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Mtoto Kutoa Jasho Akiwa Amelala

Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Mtoto Kutoa Jasho Akiwa Amelala

Ni kawaida kwa wazazi kuwa na shaka wanapo gundua jambo ndogo kwenye mtoto wao, kama kutoa jasho jingi wakiwa wamelala. Ila, hawapaswi kuwa na shaka kwani ni kawaida.

Utaratibu wa usiku umekamilika- mtoto wako amekoga, ako sawa na ana joto na usha mvisha mavazi yake ya kulala. Kisha ameanza kusinzia baada ya kumwimbia nyimbo za kumfanya alale. Kwa utaratibu, unajribu kutoka chumbani chake cha kulala na kurudi baada ya lisaa limoja kumwangalia. Unapo fanya hivi unagundua kuwa mtoto wako anatoa jasho jingi akiwa usingizini. Jambo hili linafanyika wakati wote lakini ni vyema kwa kila mzazi kuelewa kinacho sababisha. Tuna soma zaidi kuhusu mtoto kutoa jasho jingi akiwa amelala.

Huenda mzazi hasa wa mara ya kwanza akawa na shaka nyingi anapo ona mtoto wake akitoa jasho huku amelala. Na kuanza kushangaa kama kuna kitu kinacho msumbua.

Kabla ya kuwasiliana na daktari wako kujua kama jambo hili ni la kawaida. Tuna kufahamisha zaidi kuhusu yote unayo faa kujua.

Sababu za mtoto kutoa jasho akiwa amelala

Habari njema ni kuwa katika visa vingi, sehemu inayo kuwa na maji (ya jasho) nyuma ya kichwa cha mtoto wako unayopata akiwa amelala, sio kitu cha kuwa na shaka nacho. Hapa kuna baadhi ya sababu za kawaida zinazo sababisha.

  1. Mfumo wa neva ambao hauja komaa

kupata mtoto wa kike

Mfumo wa neva una jukumu la kubeba ujumbe kutoka na kupeleka kwa ubongo na uti wa mgongo na kupeleka kwenye sehemu zingine za mwili. Mfumo wetu wa neva pia una dhibiti temprecha ya mwili.

Walakini, mfumo wa neva kwa watoto wachanga hauja komaa bado. Kwa sababu hii, unashindwa kudhibiti joto mwilini mwa watoto wadogo tofauti na kwa watu wazima. Na kueleza kwa nini watoto hutoa jasho usingizini.

2. Kutoa jasho usiku wakiwa usingizini

Jasho ya usiku ni pale ambapo hasa watoto wadogo wanatoa jasho jingi wakiwa wamelala. Na kueleza sehemu yenye jasho jingi unayo pata unapo enda kumchukua mtoto wako baada ya kuamka.

Watoto hutumia wakati mwingi katika hali yao ya usingizi mzito ikilinganishwa na watu wazima. Kwa hivyo watoto wanapo toa jasho wakiwa wamelala inamaanisha wako  katika kipindi cha usingizi mzito.

3. Kuna joto jingi

Mara nyingi, tuna toa jasho kwa sababu tunahisi joto. Vivyo hivyo, sababu rahisi ya kwa nini mtoto wako anatoa jasho ni kwa sababu chumba anacho lala kina joto jingi ama pia mavazi yao yana joto jingi. Kuna wazazi ambao wanapenda kuwavalisha watoto wao nguo nyingi hasa wanapo lala kisha kuwafunikia.

Ni vyema kwa wazazi kuwa makini na hali ya anga, ikiwa kuna joto jingi, epuka kumvalisha mtoto nguo nyingi ama nzito. Hata kama ni vigumu kwa wazazi kwani mngependa mtoto awe na joto wakati wote. Hakikisha kuwa mtoto ana starehe. Kwani joto jingi pia huenda ikamtatiza kupata usingizi na kubaki akiamka baada ya kila dakika mbili.

Wakati ambapo unapaswa kuwa na shaka

mtoto kutoa jasho jingi akiwa amelala

Kama tulivyo taja hapo awali, mara nyingi, mtoto kutoa jasho akiwa amelala huwa jambo la kawaida na hakuna haja ya kuwa na wasi wasi. Lakini hizi ni baadhi ya hali ambazo kutoa jasho jingi huenda kukawa ishara ya:

  1. Ugonjwa wa moyo wa congenital

Mbali na mtoto kutoa jasho jingi akiwa amelala, ukimpata akitoa jasho jingi wakati wa mazoezi madogo kama anapo kula, huenda ikawa ni wakati wa kwenda kumtembelea daktari wa afya ya watoto kwani ni ishara ya ugonjwa wa moyo wa congenital.

Ugonjwa huu husababishwa na moyo kwenye fetusi kukua vibaya. Watoto walio na tatizo hili hutoa jasho zaidi ikilinganishwa na watoto wengine kwa sababu moyo wake unafanya kazi zaidi kuzungusha damu mwilini.

2. Hyperhidrosis

Ukigundua kuwa hata kwenye chumba kilicho na baridi bado mtoto wako anatoa jasho jingi, huenda ikawa ni kufuatia hali inayo fahamika kama hyperhidrosis.

Katika hali hii, mtoto anatoa jasho jingi zaidi ya kiwango kinacho hitajika na mwili kusawasisha temprecha ya mwili ya kawaida. Ni kawaida kwa watu walio na mikono na miguu inayo toa jasho jingi, wana hali hii pia.

Hii sio hali ambayo lazima utibu kutumia madawa. Sio jambo sugu vile. Mtoto anapokua, unaweza mfunza mbinu za kudhibiti jasho kama vile kutumia manukato.

3. Sleep Apnea

Hali hii inapatikana sana kwa watoto ambao hawaja komaa. Hii ni sababu nyingine inayo sababisha watoto kutoa jasho jingi wakiwa wamelala. Ina andamana na rangi ya ngozi ya bluu, sauti kana kwamba kutatizika kupumua na kusimama hadi sekunde 20 anapo pumua na kufanya mwili wa mtoto kufanya kazi sana ili kupumua.

4. Sudden Infant Death Syndrome (SIDS)

mtoto kucheka usingizini

Watu wengi wanapuuza hatari ya mtoto aliye na joto jingi ya mwili. Na kuwafanya waingie katika usingizi mzito ambao huenda ukawa mgumu kuwaamsha na kusababisha SIDS.

5. Hali zingine

Wakati ambapo tunasema mtoto kutoa jasho jingi akiwa amelala ni kawaida na hakuna haja ya mzazi kuwa na shaka. Ikiwa mtoto anatoa jasho jingi, hatupaswi kupuuza jambo hilo. Huenda pia ikawa ishara ya shida na mfumo wao wa neva, matatizo ya mfumo wa kupumua ama matatizo ya geni.

Ikiwa una shaka zozote kuhusu mtoto wako. Ni vyema kuwa upande salama na kumpeleka mtoto wako katika kituo cha afya aweze kukaguliwa kama ana matatizo yoyote. Lakini tungependa kuwa ashiria wazazi kuwa, hali zote tulizo taja hapo juu huwa nadra sana. Kwa hivyo usiwe na shaka nyingi unapo gundua kuwa mtoto wako anatokwa na jasho jingi akiwa amelala.

Chanzo: Babyment.Com

Soma PiaMbadala Bora Wa Maziwa Na Wenye Afya Kwa Watoto Wachanga

Written by

Risper Nyakio