Utafanyaje Ukimpata Mvulana Wako Akiiba Bidhaa Zako Za Urembo?

Utafanyaje Ukimpata Mvulana Wako Akiiba Bidhaa Zako Za Urembo?

Kisa cha mama kumpata mtoto wake wa kiume akiiba bidhaa zake za urembo.

Kumwona mtoto wako akiiba huenda kukawa chanzo cha shaka, ila ukimpata mvulana wako akiiba bidhaa zako za urembo, huenda ukakwazwa kimawazo.

Mojawapo ya shaka ambazo huenda ukawa nazo ni kushangaa kama mtoto wako ana chunguza jinsia yake. Huenda ukajiambia ni jambo asili la ukuaji wake. Lakini mvulana mdogo akijaribu kujipaka mapamba, wakati wote haihusiki na jinsia yake ama jinsia anayo ipenda kingono.

Kwa mfano, ushuhuda wa mama mmoja aliye gundua kuwa mapambo ya midomo aliyo inunua imepotea na kugundua kuwa mwizi alikuwa ni kijana wake wa miaka 15.

Mama huyu wa watoto wawili alishuku kuwa aliye fanya kitendo hiki ni binti yake ama dada yake aliye kuwa akiishi nao. Baadaye, aligundua kuwa aliye fanya hivyo ni mvulana wake.

Mama huyu alimwuliza mwanawe aliye kubali kuwa alifanya hivyo, jambo ambalo hakua ana tarajia, na lina vuma kwa wavulana wengi wanao taka kufanya majaribio na mapambo ya uso.

Jinsi ya kuzungumzo unapo mpata mtoto wako akiiba bidhaa zako za urembo

Kabla ya kitu kingine chochote, jambo moja muhimu linalo paswa kuangaziwa ni jinsi ya kufanya unapo mpata mtoto wako akiiba. Tabia hii haipaswi kupuuzwa.

Hapa kuna baadhi ya vidokezo muhimu kwa wazazi:

  • “Itumie kama nafasi ya kumfunza mwanao,” alishauri Daktari. Ruth Peters, ambaye ni mwana saikolojia wa kliniki katika makala  ya LEO.
  • Hakikisha kuwa ni vitendo vyao tu vilivyo kukasirisha.
  • Kubali kuwa mwanao anaye zidi kukua huenda akafanya mambo bila kufikiria mara mbili.
  • Mpe hiari zinazo wezekana zinazo himiza tabia chanya, kama vile kufanya kazi ili apate pesa za kununua kitu alicho taka sawa na alicho iba.
  • Wakumbushe kuwa, kwa sababu waliiba kitu, hakuwa fanyi kuwa watoto wabaya.
  • Mwelewe ila uwe na msimamo. Kuwa dhabiti kwa msimamo wako kuwa wizi haukubaliki. Na hakuna mwanya wa kujitetea.

Washawishi wa urembo wavulana: Ibuko la urembo lisilo na mbio ya kuisha?

Kwa nini wavulana hawawezi tumia bidhaa za urembo kuboresha ujasiri wao? Baadhi ya vijana wa makamu huenda wakawa wana mambo fiche wanayo wasumbua kama vile acne, upele wa uso na matatizo mengine ya ngozi. Ila leo, kujipaka bidhaa za urembo usoni ni uraibu unao julikana kuwa wa wasichana pekee. Na wavulana huvunjwa moyo kwa kuwa na “u-kike mwingi.”

Wakati ambapo kuna imani za mambo yasiyo kubalika kuhusu bidhaa za urembo, watoto wa leo wanakua katika kizazi ghali zao kisicho na imani za kikale. Kwa mfano, mitindo ya wanawake sio ya wanawake pekee.

Ibuko duniani kote la tamaduni za kikorea na Japanese kumetengeneza njia kwa mivumo zaidi inayo wafaa wake kwa waume hasa katika mitindo na urembo.

child stealing

Chanzo cha picha: BIGBANG’s Youtube page

Wavulana wa mtandao wa Instagram, wana pata mamilioni ya wafuasi. Baadhi ya wakati, huwa kama mtoto wa umri wa miaka 18 James Charles, ambaye wafuasi wake milioni 2 hungoja awafunze kuvalia bidhaa za urembo za uso. Wakati mwingine, huwa watu ambao kazi yao ni kurembesha watu kama Manny Gutierrez, aliye na wafuasi zaidi ya milioni 4.

child stealing

Image source: James Charles’ Instagram

child stealing

Chanzo cha picha: Manny MUA’s Instagram

Vijana hawa washawishi huenda wakawa wanapenda jinsia sawa ama tofauti. Jinsia wanayo ipenda haijalishi kwa wafuasi wao. Kina athiri akaunti yao ni sanaa yao. Kwao, kutumia bidhaa za urembo ni njia yao ya kujieleza.

Tasnia ya bidhaa za urembo za waume pia inaanza kuvuma. Tom Ford ambaye ni mwana mitindo maarufu kwa kazi yake na Gucci na Yves Saint Laurent, ametokea na laini yake ya bidhaa za urembo za waume.

Chapa maarufu ya Clinique imetoa aina ya bronzer, iliyo tengenezwa hasa ya wanaume.

Ukimpata mvulana wako akifanya majaribio na bidhaa za urembo za uso, usiwe na shaka. Ongea na mtoto wako ukiwa umetulia kwa mapenzi na umkumbushe kuwa wakati wote utakuwa naye, kumpa msaada anao hitaji na kumwongoza, kwa njia yoyote ile wanayo amua kujieleza kwa undani wao wote.

Vyanzo: TODAY.com, HuffPost, InStyle

Soma pia: Jinsi Wazazi Wanavyo Weza Kuwalinda Watoto Wao Katika Kipindi Cha Lockdown

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio